Mtanzania2020
JF-Expert Member
- May 23, 2020
- 817
- 1,752
Supatech: Sumit Shah ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Dukaan, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliufahamisha umma ya kwamba amefanya mabadiliko makubwa kwenye idara ya huduma kwa wateja ndani ya kampuni hiyo.
Dukaan ni kampuni kutokea nchi India ambayo inajihusisha na mauzo mtandaoni kama ilivyo kampuni nyingine ambazo huwa kama daraja la wanunuzi na wateja kukutania na kununua bidhaa.
Sumit Shah aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kusema alianzisha mfumo wa akili bandia, mfumo ambao ulisaidia kupunguza takribani asilimia 85 ya gharama za uendeshaji wa idara ya usaidizi kwa wateja ndani ya kampuni hiyo.
Matumizi ya akili bandia ndani ya kampuni ya Dukaan, ilikuwa ni sababu ya kupunguza karibu asilimia 90 ya wafanyakazi kwenye idara hiyo, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.