Faith Athanas
New Member
- Sep 8, 2022
- 3
- 1
Faith Athanas
Elimu inasababu ya kutoa ujinga na kuingiza uelewa na maarifa kwa binadamu. Lakini je elimu hiii je inatoa ujinga kama inavyotakiwa katika taifa letu?
Binti huyu wa miaka 24 alipenda sana kusoma alisoma na akasoma inavyotakiwa ,lakini kumbe alisoma kitu ambacho alilazimishwa na wazazi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa familia lakini ilikuwa sio lengo lake kusoma alichosoma, binti huyu alisoma kwa kwenda kuwafurahisha wazazi wake kwasababu ilikuwa ni ndoyo yao yeye asome alichosoma lakini je ni ndoto zake kusomea alichosoma?
Binti huyu alipomaliza degree yake ya Ufamasia akirudi nyumbani na kuchukua cheti chake alichofaulu kwa alama za juuu sana na kwenda kuwapa wazazi wake na kuwaambia "Wazazi nimemaliza nilichotakiwa kumaliza na kusoma" wazazi wake hawakuelewa kabisa walijua ni furaha yake tu kumaliza shule na kwasababu ilikuwa furaha yao kwahiyo hawakujua kitu kibaya kilichoendelea na uchungu alizokuwa nao binti yao kutokupata kile alichokitaka.
Ndipo alipowaambia wazazi wake kwamba wazazi nina furaha kusoma kitu ambacho ilikuwa ni ndoto yenu lakini sasa naomba mniache nikasome kitu ambacho ilikuwa ni ndoto yangu mlioifahamu lakini mlilazimisha nisome mlichokitaka, Kiukwel wazazi wale waliumia sana zaidi ya kawaida kwasababu walijua ndoto alizokuwa nazo ni kitu ambacho lilikiwa ni cha mda mfupi tu kumbe haikuwa hivyo,binti yule aliwaachia wazazi wake cheti na kuondoka zake.
Turudi kwenye elimu yetu ya kitanzania,wazazi wanakuwa na ndoto zao juuu ya watoto wao na sio kitu kibaya kabisa lakini wanatakiwa watambue kwamba inabidi watoto wao wanabidi wasome kitu ambacho wanapenda na ni uwezo wao kwasababu kama wanaweza kusoma kitu ambacho wamelazimishwa vyema kabisa na kufaulu, hiii inamaana kwamba hicho ambacho watasoma kwa kupenda wao wenyewe watafanya vizuri sana kwasababu hamna kitu kizuri kama kufanya kitu kutoka moyoni na sio kulazimishwa kwasababu ukilazimishwa huwezi fanya kitu kwa ufanisi mzuri.
Kama taifa tunatakiwa kuelimisha wazazi hawa kwamba wakiacha mtoto asome kitu ambacho anapenda kusomea anaweza kuwa zaidi ya walivyomtegemea kwa ndoto zao juuu yake, mifumo ya kulazimisha mtu kusoma kozi na masomo ambayo hajaipenda imeshapitwa na wakati kwasababu ndio kwanza tunatengeneza watu wavivu wa kufikiri na kujaribu kazi kwa kuwa hawana moyo kabisa na wanachosoma.
Mifumo ya elimu pia inabidi kubadilika Ili kumpatia huyu anaepaswa kusoma uwezo wa kusoma vizuri kile kitu ambacho ana penda kutoka moyoni,mifumo ya nadharia inabidi ifikie mwisho Ili kuleta manufaa katika Taifa letu na Jamii yetu kwa ujumla.
Kinachoaminika ni kwamba mtu akifanya anachopenda atajitoa kwa hali na mali Ili akifanye kitu hicho kwa ufanisi wa asilimia mia lakini alilazimishwa ni kweli atafanya kwa visingizio vingi sana kwasababu hapendi kile anachoendelea kukifanya.
Madaktari pia wanasema watu wengi wanapata msongo wa mawazo na kupoteza uhai kwasababu ya kufanya kitu nje ya kitu ambacho lilikiwa ni wazo lake.
Mifumo hiii ikibadilika basi tutafika mbali sana, ufanisi utaongezeka,misongo ya mawazo itapungua hivyo Afya ya akili itaimarika ,amani utaongezeka na tutafika mbali sana kama taifa na Jamii kwa ujumla.
Mwisho.

Upvote
2