Miaka zaidi ya 10 huko nilipohitimu chuo, nilikuwa nafahamiana na jamaa fulani muwest ambaye nilikuwa namuuziaga computer maana wakati nasoma chuo nilikuwa nanunua computer huko Kkoo na kuuza chuo na mtaani kwa order.
Sasa nilipomaliza chuo jamaa tulikuwa tumezoeana alikuwa ana pesa si haba na alikuwa ananiambia kuwa yeye yuko kwenye mradi maalum chini ya UN unideal na mambo ya mashule.
Jamaa alikuwa ana stationery ambapo alikuwa anatoa huduma za stationery ikiwemo internet café, masuala ya printing, na kuuza vifaa pia. Pia kipindi hicho Max malipo ilikuwa kwenye peak maana huduma nyingi zilikuwa hazijawa intergrated kwenye mobile money, basi naye alikuwa anatoa huduma hiyo.
Sasa bwana, baada ya kumaliza chuo nikiwa kitaa sina mchongo wowote, jamaa alikuwa ananiaminia kwamba ninajua computer kichizi. Akawa anaiambia kwanini nisiwe ninaenda pale nasaidizana na dada anayefanya kazi pale maana vitu vingi vinampiga chenga.
Mimi nikaona si haba ngoja niwe ninaenda pale kupoteza muda walau jioni ninaondoka na 5000 au 10000 kuliko kukaa tu sina lolote.
So, nikawa ninaenda pale mara kwa mara ninafanya kazi baadae tukakubaliana na jamaa kuwa anikodishe ile stationary, yani internet café na huduma kitakachobaki kikiwa chake ni vitu vya kuuza. So mimi nitakuwa namlipa kaisi fulani kila siku.
Fresh nikaichukua niakwa natoa huduma napata wateja kweli. Ila pale, yalikuwa makutano yeye na hao wawest wenzake. Walikuwa wanakuja nje kuna vile viti vimeshikana vya ofisi kwenye kibaraza wanaketi pale wanakuwa wanazungumza.
TUKIO LA KWANZA
Mimi nilikuwa na sikills za photoshop, nakumbuka siku moja wakanifuata. Wakaniambia mwenzako fulani hana kitambulisho na inabidi asafiri, so wanataka ni photoshop leseni ya ufaransa ili aitumie kuonyesha pale airport wakati akiondoka, yani kwamba akitoa passport wakitaka kitambulisho cha ziada awaonyeshe leseni.
Wakanipa sample nikaitengeneza na kuiprint. Basi walivyokuwa wananisifia mimi ndivyo kichwa kinajaa. Wala sikuwa naweza kwamba nafanya uhalifu. Jamaa akanitoa buku 20,000. Kesho yake akasafiri alikuwa anaenda U.K, so alisafiri akaondoka.
Basi wakawa wanakuja Wawest kila mara pale wengine wanakuja wamechoka baada ya miezi kadhaa mtu keshanunua ghali kapanga nyumba. Nikawa najiuliza hawa jamaa vipi mbona mimi niko hapa wao kila siku wanatoka faster.
TUKIO LA PILI
Nakumbuka ilikuwa kile kipindi Obama alipokuja Tanzania. Siku hiyo nimekaa yule jamaa mwenye ile stationery akaja. Mara baada ya muda ikapaki Benz kali, kateremka jamaa amevaa yale mavazi ya kinajeria akaja mle stationery wakasalimiana na jamaa. Basi wakazungumza, halafu baadae jamaa akanifuata akaniambia kuna kitu jamaa anataka nimtengenezee.
Basi si wakanionyesha cheque fulani ya Bank nadhani iko huko Nigeria siikumbuki jina. Wakawa wanataka nibadilishe tarakimu kwenye ile cheque. Mimi kama kawaida nikaiscan nikaingiza kwa photoshop nikaedit tarakimu. Wao wamenizunguka full kunisifia jamaa alikuwa anapenda kusema Eeeh walaaa huyu aliyekuwa amevaa kinaija.
Nikabadilisha details kama aliyokuwa anataka baada yah apo nikaiprint kwa print ya Epson ikatoka fresh.
Kisha akanipa Flash akaomba nimprintie document mbili. Nashangaa kuprint zimeandikwa top secret yani mfano wa zile nyaaka za serikali ya marekani.
Nikawa naweza hawa jamaa hizi documents wanaenda kuzifanyia nini. Any way mimi sikufuatilia na wala mawazo yangu hayakuwa kwamba kile kitendo ninashiriki uhalifu. Jamaa akanipa nadhani kama 50,000 wakasepa.
TUKIO LA TATU
Hili sasa ndilo limepelekea mimi kuandika haya matukio.
Siku moja jamaa akawa anaieleza jinsi vijana wanavyokula Maisha. Akawa anaiambia yani wanachofanya wao wana mtu anadeal na dhahabu, kazi yao ni kutafuta clients online unawaconnect naye halafu wakishauza wewe unakula pesa nzuri tu. Akawa ananiambia vijana wanaokuja ndio maana baada ya muda ninaona washamiliki magari wanaishi kwenye mapartment.
Akawa anasema si unajua wewe unajua sana kutumia computer na mtandao lakini haukufaidishi, wewe tutaftie clients wa dhahabu supplier wetu anazo za kutosha.
Nikasema haya si ndio mambo. Nikazama internet search sana, nikaja nikaconnect na mkaburu mmoja. Nikamweleza issue nzima ilivyo. Bahati nzuri kumbe jamaa yuko hapa hapa TZ wakati huo ana siku 2 ndo anaondoka.
Jamaa akanipa miadi niende tukutane tuzungumze business. Sasa mimi hapo kazi yangu ilikuwa kuwaconnect jamaa. NIkawapa namba. Nakumbuka siku hiyo asubuhi wakaja pale stationery wamevaa kiofisa. Wakaniaga wanaenda onana na huyo mkaburu.
Mimi huku naona hapa nishatoboa na mimi nasubiri warudi wanipe majibu. Baada ya saa kadhaa wakarejea. Wakasema deal halijaenda fresh, jamaa anawambia kuwa kama mzigo upo inabidi wasafiri nao wampelekee south wakati wao wanataka biashara iishe hapa hapa. Mara wakawa wanasema wakienda south itakuaje kama akiwapangia mchongo akawapiga au kuwaua.
So, wakasema huyu client hafai niwataftie mwingine. Hapo muda wote mimi sijashutuka kuwa jamaa hawana cha dhahabu wala nini.
Nikasema haina namna. Nikasema tena kwenye internet baadaye nikaibuka na jamaa mbagladesh. Nikamweleza kila kitu fresh. Jamaa mwisho akasema kama mzigo upo yeye yuko tayari kununua ila ana mtu wake TZ yuko shinyanga angependa kwanza aje aone.
Sasa mimi si najua mzigo upo nikamwambia fresh, akaomba namba nikampatia baadaye nikapigiwa namba na huyo mtu. Basi nikamwambia ngoja nongee na wadau ndio watapanga siku ya kuja kuona mzigo.
Kwenda kuwaeleza majamaa, naona baada ya kusikia kuna mtu TZ hawako interested kabisa. Mara wakaanza sikia usitatuaftie watu ambao wako TZ au wenye watu TZ. Sisi tunataka client ambao wako nje hawana watu TZ.
Sasa nikaanza jiuliza maswali hawa majamaa mbona wanachagua wateja. Nikaanza kutafakari matokio, ndipo nikaconclude kuwa nina deal na mayohoo boys na wanataka kunigeuza chambo. Maana mimi kwanza nilikuwa watu nawapa namba zangu, picha zangu pasipo kujua kuwa hao jamaa hawana dhahabu wala nini kama angepigwa mtu ningeachiwa msala matata sana.
Kuanzia siku hiyo nikaacha kuwataftia wateja wakawa wakiuliza nakwambia sijapata.
Ila jambo moja ambalo nmeligundua, victims wa hawa wa west ni madada. Wapo wawest wengi wanaishi wamepangiwa na madada kwa kuwapa ahadi kuwa biashara zao zina shida zikiwa sawa watarudisha fadhila na dada anaanza kutoa pesa akiwa anajua anainvest kumbe anapigwa.
Baadaye niliamua kuachana na ile stationery maana niligundua ninaweza siku moja kuja kamatwa kuwa ninahusika nao.
Imepita muda sana nasikia wengine walishafariki kwa natural deaths hapa hapa na wengine walishaondoka maana wapopo huwa hawakai sehemu moja.