DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Tunashuhudia mengi sana kwenye kampeni ikiwemo wagombea wote kutumia njia tofauti tofauti kuweza ku wafikia wapiga kura.
Mikutano ya hadhara ni njia moja na kwa haraka haraka imeweza kuunganisha mikusanyiko mikubwa sana ya watu. Kama kawaida si kitu cha ajabu kwa wagombea ku mwaga ahadi na sera kwenye mikutano ya hadhara lakini tuji ulize swali moja: Tofauti na kuomba kura kwa wananchi.
Je, Wagombea wana thamini mikusanyiko ya watu au wana tumia fursa hio kusema chochote? Ahadi zingine zina tekelezeka ila mengine yanayo pokelewa kwa shangwe, vigelegele na nderemo haya ni ya ku furahisha umati.
Wengi wanaweza kusema kwamba midahalo na mikutano na vyombo vya habari sio njia sahihi na pekee ya kupata wagombea sahihi lakini mikutano ya hadhara na mambo yanayojadiliwa yanakosa umakini ambao unaweza kumtofautisha mgombea mmoja na mwingine kwa sera.
Mwisho kabisa ningependa kupongeza shirika la ITV kwa kuandaa mahojiano na wagombea wa urais katika kipindi chake cha dakika 45.
Mpaka sasa hivi Mhe Tundu Lissu na Prof Ibrahim Lipumba wameishahudhuria. Ingekuwa vyema sana kama mgombea wa CCM ambaye ndio Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Joseph Pombe Magufuli angeweza kutueleza kwa undani zaidi yale yote aliyoyapanga kwa ajili ya miaka mitano ijayo.
Jumatatu njema,
Tafakari.