Jinsi Bakhmut na Kherson zinavyo andaa mashambulizi yajayo (counteroffensives) ya Ukraine

Status
Not open for further replies.

Six Stars

Member
Joined
Dec 8, 2021
Posts
14
Reaction score
102
Msimu huu wa kiangazi, kuna harufu ya counteroffensive inanukia nchini Ukraine, kwani matukio yanayotokea Kherson na Bakhmut yanatazamiwa kusambaa kote nchini na kuunda mkondo wa mashambulizi yajayo.

Ukraine-CO-training.jpg

Askari wa Ukraine wakati wa mafunzo kwenye mstari wa mbele katika eneo la Donetsk, Ukraine, Jumamosi, Aprili 15, 2023.

Twende taratibu, tarehe 22 Aprili vyanzo mbalimbali vilibainisha kwamba Ukraine ilikuwa imechukua nafasi kadhaa upande wa Dnipro River (au Dnieper) kutoka eneo la Kherson kando ya mto upande wa mashariki na kusini mwa mji huo, baada ya miezi kadhaa ya mvutano wa pande mbili. Siku iliyofuata tuliona ramani inayoonyesha baadhi ya nafasi izo zilizodhibitiwa na Ukraine upande wa pili wa mto.

isw-barros-Dnipro.jpg

Tathmini iliyotajwa hapo juu ya tarehe 22 Aprili
ISW-May7-Kherson.png

tathmini kufikia mchana wa tarehe 7 Mei

Wiki mbili zilizopita, wakati eneo kubwa la uvamizi karibu na mto liliporudi kwenye mikono ya Ukraine, Ukraine imepanua na litaendelea kupanua uwepo wake upande mwingine wa mto katika eneo pana zaidi linalotangamana magharibi kote kwenye sehemu ya benki ya Dnipro inayopatikana upande wa kusini/mashariki ya mji wa Kherson. Urusi haionyeshi uwezo wa kushambulia katika eneo hili kwa miezi kadhaa. Namna pekee ya kufanya shambulizi hapo ni kwa kunyofoa vikosi kutoka maeneo mengine, jambo ambalo litakuwa na athari mbaya na halitatokea kwa kuwa sehemu kubwa ya vikosi vya Urusi vipo mashariki, na kwa kuzingatia kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye anatuhumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai anaipa kipaumbele eneo la mashariki.

kwa kuzingatia hoja hii, ni wazi kwamba, kwa umakini wa Putin huko Bakhmut, hakujakuwa na shughuli yoyote muhimu ya kijeshi ya Urusi mahali popote nje ya mashariki mwa Ukraine kwa miezi mingi kwa sababu Urusi haina uwezo wa kufanya shambulizi kama hilo mahali pengine, na ramani za udhibiti zinaonyesha wazi hali hii. Kumbuka sijaandika uwezo wa mashambulizi yenye mafanikio, bali uwezo wa kufanya mashambulizi tu, kwani hata uwezo huo huko mashariki umekuwa wa kusikitisha na wa hasara kubwa ya maisha na rasilimali, na maendeleo yanapatikana kwa kasi ya kobe, hasa katika eneo la Bakhmut ambapo hakuna faida yoyote kubwa ya muda mrefu ya kimkakati kwa Urusi zaidi ya kujidhoofisha na kuyafungulia njia mashambulizi toka Ukraine. Kwa msururu wa matukio ya hofu kubwa kati ya mkuu wa Wagner Yevgeniy Prigozhin, kiongozi wa kivita wa Chechen Ramzan Kadyrov, na uongozi wa jeshi la Urusi, inaonekana Warusi wamegundua hilo na wanapambana kujaribu kukabiliana na kitisho hiki kinachozidi kadri muda unavyokwenda. Wote ni sehemu ya jeshi lililounganishwa kisheria kwa nadharia, lakini kwa vitendo, wote wanafanya kazi nzuri katika kuonyesha matatizo mabaya ya jeshi la Urusi ambalo ni bidhaa ya miongo miwili ya sera ya Kremlin chini ya mkono mgumu wa kijeshi wa Putin.

Katika eneo la kusini kati, tangu Ukraine iliporejesha upande wa kaskazini/magharibi wa Dnipro huko Kherson Oblast kutoka kwa Urusi katika nusu ya kwanza ya Novemba, Urusi hata hakujaribu kurudisha kitu upande huo wa mto. Wakati huo, ilibainika kuwa wanajeshi wengi wa Urusi waliobaki walikuwa katika hali mbaya, waliochoka, na kupewa rasilimali kidogo, na asilimia kubwa ya rasilimali za Urusi tangu wakati huo zimeelekezwa kuelekea Bakhmut. Ingawa wanajeshi wa Urusi wanajitahidi kujiweka vizuri upande wa kusini/mashariki wa Dnipro, haitarajiwi kuwa wanajeshi bora na vifaa vya Urusi vitakuwa miongoni mwao kutokana na Urusi kuwa na lengo lake mashariki mwa Ukraine na idadi kubwa ya vifo vya kushtua iliyopata.

Kwa sababu Urusi sasa imeenea kwa wembamba kote Ukraine baada ya kupata hasara kubwa na bado inaendelea na shughuli za mashambulizi kwa kiasi kikubwa bila mafanikio mashariki, haiwezekani kutarajia kufanya mengi kwa upande kujilinda kwa kina, kwa sababu ngome zinahitaji askari halisi na wengi. Kuna picha za satelaiti kutoka mwezi Februari hadi mwishoni mwa Aprili zinaonyesha kituo kikubwa cha kijeshi cha Urusi huko Crimea kimepungukiwa na askari pamoja na vifaa.

Kwenye ukingo wa kusini/mashariki ya Dnipro, wanajeshi wa Ukraine, kama kawaida yao, wanatumia faida kubwa ya silaha zenye usahihi wa kushambulia vifaa vya kijeshi vya Kirusi katika eneo hilo na maeneo yaliyo mbali kama Crimea na Melitopol katika Oblast ya Zaporizhzhia jirani, hivyo kufanya nafasi nzima ya Urusi kuwa dhaifu kwa shambulio la mwisho, kama walivyofanya kabla ya kuwafukuza Urusi kutoka kingo ya kaskazini/magharibi ya Dnipro mwezi Novemba. Ni muhimu pia kuzingatia kuwa Dnipro ndiyo kizuizi cha mwisho kati ya wanajeshi wa Ukraine na Crimea, kwani, na nafasi zao mpya upande wa Dnipro, wanajeshi wa Ukraine sasa wapo maili sitini kutoka mpaka wa Crimea kaskazini.

Jenerali wa zamani wa Marekani, Mark Hertling, ameonyesha mara kwa mara kuwa Ukraine inalazimika kuhamisha wanajeshi na vifaa kwa umbali mfupi wa ndani ikilinganishwa na Urusi, ambayo inalazimika kufanya hivyo kwa umbali mrefu zaidi wa nje, kufanya kazi hiyo kuwa rahisi zaidi kwa Ukraine na ngumu zaidi kwa Urusi. Hii inamaanisha, katika awamu ya kukabiliana na mashambulizi inayokuja, itakuwa rahisi kwa Ukraine kuhamisha wanajeshi na vifaa vyao kwa haraka ili kuishangaza Urusi na kuendelea kuifanya iwe katika hali ya kutotulia, huku Urusi ikiwa na shida ya kuimarisha au kuhamisha, na njia ndefu ya kusafirisha inayoweka hatarini kuweza kushughulikiwa na HIMARS, M777s, Caesars, na silaha zingine za usahihi ambazo Urusi haina.

Urusi sasa ina tatizo linalofanana kabisa na moja ambalo liliwakabili kwenye mashambulizi ya Ukraine msimu uliopita na kupoteza maeneo: Urusi ina chaguo mbaya pekee, na marekebisho yoyote itakayofanya yataambatana na gharama kubwa. Licha ya yote, Urusi haiperform vyema katika medani ya vita popote ndani ya Ukraine, kwani kama nilivyotangulia kueleza, mashambulizi yake ya ardhini yanasonga mbele kwa gharama kubwa sana katika maeneo machache tu au yanashindwa kabisa. Hii inamaanisha kwamba ikiwa Urusi itahamisha wanajeshi au kuzitumia nguvu zake za ziada kutoka eneo moja kwenda lingine ili kuimarisha nafasi zake (katika kesi hii, nafasi zake zilizobaki katika Kherson Oblast), itajifanya kuwa dhaifu na yenye hatari kwenye uwanja wa kwanza ilikopunguza rasilimali. Lakini ikiwa haitafanya hivyo, itadhuru uwezekano wake wa kupunguza athari yoyote inayofuata kutoka kwa Kherson, ambayo Ukraine inaweza kupanga wakati wake kulingana na kile Urusi inafanya na haifanyi kuhusu kuhamisha na kuimarisha. Yote hayo, Ukraine inaweza pia kuwa inajiandaa kwa shambulio lingine la nyongeza? ambapo Urusi haitegemei, kama ilivyotokea katika eneo la Kharkiv mwishoni mwa msimu wa joto wakati Urusi ilikuwa inatarajia pigo la nguvu kutokea Kherson, ambalo bado liliikuja baada ya Urusi kupata hasara kubwa ya watu, vifaa, na eneo kutoka kwa mashambulizi ya Ukraine katika mstari wa Kharkiv.

Kama kwenye mashambulizi ya awali, inategemea hesabu rahisi: idadi ya askari wa Urusi ni dhaifu pande zote za hesabu na kimsingi imebaki kuchagua wapi pa kupoteza, kwa kasi na madhara gani kwa kuhamisha rasilimali kutoka sehemu moja kwenda nyingine pia mambo mengine kwenye hesabu hayako vizuri kwa Urusi na yanazidi kuwa duni ikilinganishwa na nguvu bora za Ukraine, haswa morali, mafunzo, silaha, vifaa, uwezo unaopungua ikilinganishwa na uwezo unaokua, jinsi wanavyoperfom na uongozi.

Kuna uzi nilibainisha mwishoni mwa mwaka jana kwamba vita hii kitambo imebaki katika hatua mbili zinazobadilishana: hatua ya kwanza ni mashambulizi ya Ukraine (counteroffensives) na hatua ya pili ni maandalizi yake. Iwe hii ni mwisho wa hatua ya pili au mwanzo wa ya kwanza, bado haijulikani, lakini hilo halibadilishi maana kubwa ya Ukraine kuvuka Dnipro na kushindwa kwa Urusi kuchukua Bakhmut kikamilifu, kama inavyoonyeshwa na mzozo wa umma wa Prigozhin / Kremlin kwa upande wa pili. Kile Ukraine itakachofanya na lini upande wa kusini/mashariki mwa Dnipro - na jinsi Urusi itakavyojibu hilo - litakuwa na athari kote Ukraine. Pia ukiangalia kampeni ya Bakhmut imekuwa na athari kubwa kwa Urusi inayopoteza watu na rasilimali huko na kuathiri juhudi zake kila mahali Ukraine. Hapa tunaona kwamba Ukraine inaelewa jinsi ya kugawanya, kusaidiana na kufanya operesheni zake tofauti tofauti kwa wakati mmoja kwenye mstari wa mbele na maeneo tofauti, wakati Urusi haijui, kitu ambacho kinafanya Ukraine ashinde na Urusi ashindwe katika vita hivi vibaya.

Kilicho wazi ni kwamba Ukraine kujiimarisha kwenye ukingo wa mashariki/kusini wa Dnipro ng'ambo ya jiji la Kherson kunaweka maeneo mengine ya Oblast ya Kherson pamoja na Oblast ya Zaporizhzhia na Peninsula ya Crimea katika hatari siku za usoni.. Sehemu za Zaporizhzhia Oblast zilizokaliwa na Warusi, Kherson Oblast kwa ujumla ni tambarare ngumu za pwani ambazo ni vigumu kulinda, na ni oblast ya mwisho kati ya vikosi vya Ukraine kusini na Donetsk Oblast kwa mashariki ambapo mapigano makali yamekuwa yakitokea, Zaporizhzhia ni kizingiti cha mwisho ambacho Ukraine itahitaji kuikomboa kabla ya vikosi vyake kusini kuungana na vikosi vinavyopigana kwa nguvu mashariki mwa nchi (ikiwa ni pamoja na Bakhmut). Kwa upande mwingine, hilo linaweza kuruhusu Ukraine kufanya mashambulizi yasiyotarajiwa na kuwashinda Warusi kwenye sehemu za mashariki mwa Donbas na hadi mpaka wa Urusi. Hivyo, maendeleo haya kwenye mto Dnipro na Bakhmut na athari zake zinaweza kuwa na matokeo makubwa katika maeneo mengine muhimu ya Ukraine hivi karibuni na kubadilisha mikakati na hesabu za vita nzima.
 
Vita Vinavyopiganwa na Urusi Ni Vya Enzi za Zamani Sasa hivi Vita Ni Akili na maarifa Mengi So putini kila hotuba Anayo toa Anakumbusha Enzi ya Sovieti kuvishinda Vikosi Vya Ujerumani Sasa hii imekula Kwake na Anakesi ya Kujibu The Heague Yani Halali Usingizi Mtamu Mwisho Wa Siku pale pale Kremlin Atafungwa Jela anazowafunga Wapinzani wake Kisiasa ??
 
Msimu huu wa kiangazi, kuna harufu ya counteroffensive inanukia nchini Ukraine, kwani matukio yanayotokea Kherson na Bakhmut yanatazamiwa kusambaa kote nchini na kuunda mkondo wa mashambulizi yajayo.

View attachment 2620490
Askari wa Ukraine wakati wa mafunzo kwenye mstari wa mbele katika eneo la Donetsk, Ukraine, Jumamosi, Aprili 15, 2023.

Twende taratibu, tarehe 22 Aprili vyanzo mbalimbali vilibainisha kwamba Ukraine ilikuwa imechukua nafasi kadhaa upande wa Dnipro River (au Dnieper) kutoka eneo la Kherson kando ya mto upande wa mashariki na kusini mwa mji huo, baada ya miezi kadhaa ya mvutano wa pande mbili. Siku iliyofuata tuliona ramani inayoonyesha baadhi ya nafasi izo zilizodhibitiwa na Ukraine upande wa pili wa mto.

View attachment 2620492
Tathmini iliyotajwa hapo juu ya tarehe 22 Aprili
View attachment 2620502

tathmini kufikia mchana wa tarehe 7 Mei

Wiki mbili zilizopita, wakati eneo kubwa la uvamizi karibu na mto liliporudi kwenye mikono ya Ukraine, Ukraine imepanua na litaendelea kupanua uwepo wake upande mwingine wa mto katika eneo pana zaidi linalotangamana magharibi kote kwenye sehemu ya benki ya Dnipro inayopatikana upande wa kusini/mashariki ya mji wa Kherson. Urusi haionyeshi uwezo wa kushambulia katika eneo hili kwa miezi kadhaa. Namna pekee ya kufanya shambulizi hapo ni kwa kunyofoa vikosi kutoka maeneo mengine, jambo ambalo litakuwa na athari mbaya na halitatokea kwa kuwa sehemu kubwa ya vikosi vya Urusi vipo mashariki, na kwa kuzingatia kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye anatuhumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai anaipa kipaumbele eneo la mashariki.

kwa kuzingatia hoja hii, ni wazi kwamba, kwa umakini wa Putin huko Bakhmut, hakujakuwa na shughuli yoyote muhimu ya kijeshi ya Urusi mahali popote nje ya mashariki mwa Ukraine kwa miezi mingi kwa sababu Urusi haina uwezo wa kufanya shambulizi kama hilo mahali pengine, na ramani za udhibiti zinaonyesha wazi hali hii. Kumbuka sijaandika uwezo wa mashambulizi yenye mafanikio, bali uwezo wa kufanya mashambulizi tu, kwani hata uwezo huo huko mashariki umekuwa wa kusikitisha na wa hasara kubwa ya maisha na rasilimali, na maendeleo yanapatikana kwa kasi ya kobe, hasa katika eneo la Bakhmut ambapo hakuna faida yoyote kubwa ya muda mrefu ya kimkakati kwa Urusi zaidi ya kujidhoofisha na kuyafungulia njia mashambulizi toka Ukraine. Kwa msururu wa matukio ya hofu kubwa kati ya mkuu wa Wagner Yevgeniy Prigozhin, kiongozi wa kivita wa Chechen Ramzan Kadyrov, na uongozi wa jeshi la Urusi, inaonekana Warusi wamegundua hilo na wanapambana kujaribu kukabiliana na kitisho hiki kinachozidi kadri muda unavyokwenda. Wote ni sehemu ya jeshi lililounganishwa kisheria kwa nadharia, lakini kwa vitendo, wote wanafanya kazi nzuri katika kuonyesha matatizo mabaya ya jeshi la Urusi ambalo ni bidhaa ya miongo miwili ya sera ya Kremlin chini ya mkono mgumu wa kijeshi wa Putin.

Katika eneo la kusini kati, tangu Ukraine iliporejesha upande wa kaskazini/magharibi wa Dnipro huko Kherson Oblast kutoka kwa Urusi katika nusu ya kwanza ya Novemba, Urusi hata hakujaribu kurudisha kitu upande huo wa mto. Wakati huo, ilibainika kuwa wanajeshi wengi wa Urusi waliobaki walikuwa katika hali mbaya, waliochoka, na kupewa rasilimali kidogo, na asilimia kubwa ya rasilimali za Urusi tangu wakati huo zimeelekezwa kuelekea Bakhmut. Ingawa wanajeshi wa Urusi wanajitahidi kujiweka vizuri upande wa kusini/mashariki wa Dnipro, haitarajiwi kuwa wanajeshi bora na vifaa vya Urusi vitakuwa miongoni mwao kutokana na Urusi kuwa na lengo lake mashariki mwa Ukraine na idadi kubwa ya vifo vya kushtua iliyopata.

Kwa sababu Urusi sasa imeenea kwa wembamba kote Ukraine baada ya kupata hasara kubwa na bado inaendelea na shughuli za mashambulizi kwa kiasi kikubwa bila mafanikio mashariki, haiwezekani kutarajia kufanya mengi kwa upande kujilinda kwa kina, kwa sababu ngome zinahitaji askari halisi na wengi. Kuna picha za satelaiti kutoka mwezi Februari hadi mwishoni mwa Aprili zinaonyesha kituo kikubwa cha kijeshi cha Urusi huko Crimea kimepungukiwa na askari pamoja na vifaa.

Kwenye ukingo wa kusini/mashariki ya Dnipro, wanajeshi wa Ukraine, kama kawaida yao, wanatumia faida kubwa ya silaha zenye usahihi wa kushambulia vifaa vya kijeshi vya Kirusi katika eneo hilo na maeneo yaliyo mbali kama Crimea na Melitopol katika Oblast ya Zaporizhzhia jirani, hivyo kufanya nafasi nzima ya Urusi kuwa dhaifu kwa shambulio la mwisho, kama walivyofanya kabla ya kuwafukuza Urusi kutoka kingo ya kaskazini/magharibi ya Dnipro mwezi Novemba. Ni muhimu pia kuzingatia kuwa Dnipro ndiyo kizuizi cha mwisho kati ya wanajeshi wa Ukraine na Crimea, kwani, na nafasi zao mpya upande wa Dnipro, wanajeshi wa Ukraine sasa wapo maili sitini kutoka mpaka wa Crimea kaskazini.

Jenerali wa zamani wa Marekani, Mark Hertling, ameonyesha mara kwa mara kuwa Ukraine inalazimika kuhamisha wanajeshi na vifaa kwa umbali mfupi wa ndani ikilinganishwa na Urusi, ambayo inalazimika kufanya hivyo kwa umbali mrefu zaidi wa nje, kufanya kazi hiyo kuwa rahisi zaidi kwa Ukraine na ngumu zaidi kwa Urusi. Hii inamaanisha, katika awamu ya kukabiliana na mashambulizi inayokuja, itakuwa rahisi kwa Ukraine kuhamisha wanajeshi na vifaa vyao kwa haraka ili kuishangaza Urusi na kuendelea kuifanya iwe katika hali ya kutotulia, huku Urusi ikiwa na shida ya kuimarisha au kuhamisha, na njia ndefu ya kusafirisha inayoweka hatarini kuweza kushughulikiwa na HIMARS, M777s, Caesars, na silaha zingine za usahihi ambazo Urusi haina.

Urusi sasa ina tatizo linalofanana kabisa na moja ambalo liliwakabili kwenye mashambulizi ya Ukraine msimu uliopita na kupoteza maeneo: Urusi ina chaguo mbaya pekee, na marekebisho yoyote itakayofanya yataambatana na gharama kubwa. Licha ya yote, Urusi haiperform vyema katika medani ya vita popote ndani ya Ukraine, kwani kama nilivyotangulia kueleza, mashambulizi yake ya ardhini yanasonga mbele kwa gharama kubwa sana katika maeneo machache tu au yanashindwa kabisa. Hii inamaanisha kwamba ikiwa Urusi itahamisha wanajeshi au kuzitumia nguvu zake za ziada kutoka eneo moja kwenda lingine ili kuimarisha nafasi zake (katika kesi hii, nafasi zake zilizobaki katika Kherson Oblast), itajifanya kuwa dhaifu na yenye hatari kwenye uwanja wa kwanza ilikopunguza rasilimali. Lakini ikiwa haitafanya hivyo, itadhuru uwezekano wake wa kupunguza athari yoyote inayofuata kutoka kwa Kherson, ambayo Ukraine inaweza kupanga wakati wake kulingana na kile Urusi inafanya na haifanyi kuhusu kuhamisha na kuimarisha. Yote hayo, Ukraine inaweza pia kuwa inajiandaa kwa shambulio lingine la nyongeza? ambapo Urusi haitegemei, kama ilivyotokea katika eneo la Kharkiv mwishoni mwa msimu wa joto wakati Urusi ilikuwa inatarajia pigo la nguvu kutokea Kherson, ambalo bado liliikuja baada ya Urusi kupata hasara kubwa ya watu, vifaa, na eneo kutoka kwa mashambulizi ya Ukraine katika mstari wa Kharkiv.

Kama kwenye mashambulizi ya awali, inategemea hesabu rahisi: idadi ya askari wa Urusi ni dhaifu pande zote za hesabu na kimsingi imebaki kuchagua wapi pa kupoteza, kwa kasi na madhara gani kwa kuhamisha rasilimali kutoka sehemu moja kwenda nyingine pia mambo mengine kwenye hesabu hayako vizuri kwa Urusi na yanazidi kuwa duni ikilinganishwa na nguvu bora za Ukraine, haswa morali, mafunzo, silaha, vifaa, uwezo unaopungua ikilinganishwa na uwezo unaokua, jinsi wanavyoperfom na uongozi.

Kuna uzi nilibainisha mwishoni mwa mwaka jana kwamba vita hii kitambo imebaki katika hatua mbili zinazobadilishana: hatua ya kwanza ni mashambulizi ya Ukraine (counteroffensives) na hatua ya pili ni maandalizi yake. Iwe hii ni mwisho wa hatua ya pili au mwanzo wa ya kwanza, bado haijulikani, lakini hilo halibadilishi maana kubwa ya Ukraine kuvuka Dnipro na kushindwa kwa Urusi kuchukua Bakhmut kikamilifu, kama inavyoonyeshwa na mzozo wa umma wa Prigozhin / Kremlin kwa upande wa pili. Kile Ukraine itakachofanya na lini upande wa kusini/mashariki mwa Dnipro - na jinsi Urusi itakavyojibu hilo - litakuwa na athari kote Ukraine. Pia ukiangalia kampeni ya Bakhmut imekuwa na athari kubwa kwa Urusi inayopoteza watu na rasilimali huko na kuathiri juhudi zake kila mahali Ukraine. Hapa tunaona kwamba Ukraine inaelewa jinsi ya kugawanya, kusaidiana na kufanya operesheni zake tofauti tofauti kwa wakati mmoja kwenye mstari wa mbele na maeneo tofauti, wakati Urusi haijui, kitu ambacho kinafanya Ukraine ashinde na Urusi ashindwe katika vita hivi vibaya.

Kilicho wazi ni kwamba Ukraine kujiimarisha kwenye ukingo wa mashariki/kusini wa Dnipro ng'ambo ya jiji la Kherson kunaweka maeneo mengine ya Oblast ya Kherson pamoja na Oblast ya Zaporizhzhia na Peninsula ya Crimea katika hatari siku za usoni.. Sehemu za Zaporizhzhia Oblast zilizokaliwa na Warusi, Kherson Oblast kwa ujumla ni tambarare ngumu za pwani ambazo ni vigumu kulinda, na ni oblast ya mwisho kati ya vikosi vya Ukraine kusini na Donetsk Oblast kwa mashariki ambapo mapigano makali yamekuwa yakitokea, Zaporizhzhia ni kizingiti cha mwisho ambacho Ukraine itahitaji kuikomboa kabla ya vikosi vyake kusini kuungana na vikosi vinavyopigana kwa nguvu mashariki mwa nchi (ikiwa ni pamoja na Bakhmut). Kwa upande mwingine, hilo linaweza kuruhusu Ukraine kufanya mashambulizi yasiyotarajiwa na kuwashinda Warusi kwenye sehemu za mashariki mwa Donbas na hadi mpaka wa Urusi. Hivyo, maendeleo haya kwenye mto Dnipro na Bakhmut na athari zake zinaweza kuwa na matokeo makubwa katika maeneo mengine muhimu ya Ukraine hivi karibuni na kubadilisha mikakati na hesabu za vita nzima.
Siku zote mavamizi huwa hayafanikiwi, nchi nyingi zina uhuru wake Russia atatupwa alikotoka tuu
 
Hata mimi Urusi inanishangaza.

Ila kinachonishangaza zaidi;
Hawa NATO wanashindwa nini kumkimbiza na kumfurusha kutoka huko Ukraine mtu dhaifu kiasi hiki!?
Inashangaza kwa kweli

Jamaa wa nyeto walikua na uwezo wa kupeleka ndege km buku kumi ndani ya Ukraine na kutangaza no flai zon

Baada ya muda wangewapa URUSI shart la kuondoka ndan ya Ukraine ndan ya masaa mawili

Jibu atakalotoa URUSI mim sijui
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom