Innocent Kirumbuyo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,641
- 4,457
Hello
Mimi ni ndugu yenu innocent kirumbuyo kwa miaka miwili nimekuwa nikiweka story biashara ya viatu
1) Biashara ya viatu inaweza kukutajirisha
2) Utajiri uliojificha kwenye viatu vya mtumba
Nafarijika sana kwa kupokea maoni mengi na mawazo jinsi watu walivyo badili mitazamo yao na maisha yao kupitia mandiko yangu.
Cha pili Kipekee kabisa niwapongeze jamii forum kwa ili jukwaa limekuwa muhimili wetu wakubadili maisha yetu na jamii kwa ujumla kwasababu kupitia jamii forum nimekutana na watu wengi sana na muhimu sana kwenye maisha yangu.
OK
Niende kwenye mada moja kwa moja
Ni mwaka sasa toka nilivyoandika uzi kuhusu biashara ya viatu vya mtumba
3) Utajiri uliojificha kwenye viatu vya mtumba
Na leo niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuwapa mrejesho na wapi nilipo paka sasa
Kwa kweli kila fursa uja na changamoto yake miezi miwili tu baada ya kuandika ule uzi
Nasikitika kusema nilivunjiwa magoli yangu yote na serikali kwasababu atukuwepo sehemu rasmi.
Pamoja na yote ayo sikufa moyo nilikuwa na akiba ya milioni moja (1000000).
Nikifikiri kitu gani cha kufanya na hiyo milioni
Ilinibidi niende kwanza kwenye maeneo machinga waliopelekwa kufika kule kwa kweli biashara ilikuwa ngumu sana wiki linapita aujauza pea ata moja nikaona huu ni ujinga
Nilichukuwa uwamuzi wa kuuza banda langu nikaanza kutembeza viatu mtaa kwa mtaa.
Kutembeza ni ngumu kidogo ila ilikuwa afadhali kwasababu kwa siku nauza ata pea mbili hadi tano.
Kwaiyo kidogo hali ikawa nzuri
Ndio siku moja nilipokea simu ya dada moja akiomba nimtafutie mtu anapangisha banda lake liliopo mjini mitaa ya lumumba Kwa laki moja kwa mwezi kwa mwaka Niliona kama ni fursa imekuja kwangu
Niliongea na mke wangu tukashauriana tupachukuwe hapo nikaenda kumuomba yule dada anifanyie milioni moja kwa mwaka yule dada akakubali
Nilimlipa pesa yake nikapewa banda ila sikuwa na pesa ya mtaji
Ikabidi niuze simu yangu ya mkononi nikauza na simu ya mke nikapata pesa kidogo nikaagiza mzigo Dar.
Baada ya kuagiza mzigo dar kwa kweli mimi na wife tulikuwa tunafanya kazi kwa juhudi sana baada ya mwezi moja tulianza kupata matokeo kwasababu tulianza kuona mabadiliko makubwa sana
Baada ya miezi 3 nikawa na mtaji kabisa na pesa za kutosha kwa kweli maisha yalikuwa yanaenda vizuri kabisa
Kuna siku mke wangu akaniambia Kuna eneo la mbele yetu linauzwa ni zuri na kubwa sana.
Na mimi kwakeli nilivyoliona lile eneo lilikuwa zuri sana ikabidi niongee na mwenye eneo akaniuzia lile eneo
Mara moja
Nikaanza kulijenga kwasababu lilikuwa eneo wazi tu nilijenga kwa kipindi kifupi kisha nikaamisha mzigo wangu
Kule nilipokuwa nimekodi ikabidi nimtafute mtu wa kunirudishia kodi ya miezi yangu iliyokuwa imebaki
Nilipata mtu akanirudishia kodi yangu miezi 6 nikamuachia pale mimi na mke wangu tukawa tunakomaa na pale tuliponunua
Nikiri tu kwa muda mfupi nimeona mafanikio makubwa sana paka naagiza mzigo paka wa milioni mbili na zaidi
Naona kabisa mafanikio makubwa mbeleni
Nakaribisha maoni ushauri na maswali kuhusu hii biashara
Pia nipo tayari kumsaidi mtu yeyote kufanya hii biashara viatu
Kama upo Mwanza nakukaribisha mitaa ya lumumba karibu na vunja bei ndio eneo banda langu lipo hapo tutabadilishana mawazo kama unatamani kufanya biashara ya viatu kwa vitendo nitakuelekeza BUREEE KABISA
ASANTE SANA
Moja goli langu lilovunjwa na serikali hapa ndio eneo nililoanzia na kukusanya mtaji.

Upvote
54