expter
New Member
- Nov 30, 2020
- 2
- 9
Habari wanajukwaa wenzangu.Ni matumaini yangu kila mmoja yu buheri wa Afya.
Mimi ni kijana niliyemaliza kidato Cha nne miaka kadhaa iliyopita lakini isivyobahati sikufaulu yaani nilifeli kidato Cha nne. Baada ya matokeo nilikuwa na huzuni sana kwani nilikuwa napenda sana kusoma na darasani nilikuwa nafanya vizuri.
Baada ya muda wakati natapatapa sijui Cha kufanya nilikutana na rafiki yangu ambaye alikuwa akisoma Chuo kwa kipindi hicho ndipo aliponiambia kuwa Chuo alichokuwa anasoma Kinahitaji D nne tu ili ujiunge kwa ngazi ya cheti.
Basi nilijiunga na Chuo kwa kuwa nilikuwa na hizo D nne.Kwa wakati huo Mama pamoja na wajomba walisaidia Ada japo ilipatikana kwa shida sana, Kwani kipindi hicho ndo kipindi ambacho nilimpoteza Baba ambaye alifariki nikiwa kidato Cha nne.
Nilifanikiwa kumaliza (Certificate)Astashahada katika Chuo Cha Biashara katika fani ya Ugavi na Ununuzi lakini kwa kipindi chote nilichokuwa hapo Chuo sikufarahia Wala kukipenda nilichokuwa nasoma.Nilisoma kwa kuwa matokeo ndo yalinilazimisha kusoma kozi hiyo.
Baada ya hapo nilijiunga na Diploma (Stashahada) katika fani hiyohiyo lakini sikumaliza kwa kuwa ilikuwa changamoto kupat Ada.
Niliamua kuacha Chuo na kuingia mtaani kutafuta pesa.
Nilipata kazi kwa Wahindi na malipo niliyokuwa nalipwa yalikuwa madogo sana yalikuwa hayatoshelezi mahitaji yangu.
Niliacha hiyo kazi na baadae nikapata kazi kwa waarabu katika kampuni moja ya Gesi Lahaula!! Hapa ndo ilikuwa Bora ya Muhindi,kwani hapo ndo sikulipwa kabisa Bora hata kwa Muhindi nililupwa kidogo.
Niliamua kuacha kazi hiyo na kurudi mtaani.
KUCHUKUA BODABODA YA MKATABA
-wakati nipo mtaani nilijenga urafiku na waendesha Bodaboda ndipo mmoja wapo akaniambia kuwa Kuna jamaa ameshidwa mkataba amerudisha kwa Boss. Nilijilipua na KUCHUKUA BODABODA hiyo kwani kwa kipindi hicho Sikuwa mzoefu na Biashara hiyo.
KURUDI SHULE
Baada ya kuendesha Bodaboda miezi kadhaa niliona mambo yameenza kukaa sawa nilitamani kurudi SHULE kama nilivyosema awali nilikuwa napenda sana kusoma.Hapo sikutaka tena kuendelea na Chuo badala yake nilienda kurudia mtihani wa kidato Cha Nne.Nilijiunga na moja ya kituo Cha nikaanza kusoma huku Ada nikilipa kutokana na kazi yangu ya BODABODA. wakati wote huo nilikuwa nimepanga na nalipa Kodi kupitia kazi yangu ya BODABODA
KUFAULU MITIHANI YA KIDATO CHA NNE
- Baada ya kurudia mitihani ya kidato Cha nne namshukuru Mungu nilifaulu kwa vizuri kwani safari hii nilipata Division 2 ya kwanza
KIDATO CHA SITA
-Nilisoma kidato Cha 5&6 kwa mwaka mmoja na KUFAULU tena kwa Daraja la Pili
KUMBUKA wakati wote nasoma nilikuwa na pikipiki ya mkataba yaani nilikuwa napeleka laki1 kila baada ya siku 10 kwa miezi 13
Nilimaliza mkataba na pikipiki ikiwa yangu .
KUJIUNGA NA CHUO
Nilijiunga na Chuo lakini awamu hii nilienda kusoma Education kwani nilikuwa napenda kuwa mwalimu toka zamani na hapa nilisoma kwa furaha kwani nilisoma nilichokuwa napenda
Nawakumbusha tu Ada na matumizi yote nilikuwa napata kupitia kazi yangu ya BODABODA
MAFANIKIO
Nimemaliza Chuo mwaka huu na nimepata mtaji kupitia kazi yangu ya BODABODA, ambapo naleta korosho kutoka shamba Mtwara na kuziuza rejareja kupitia mitandao ya kijamii
KUENDELEA NA BODABODA
Ila ya kwanza baada ya kumaliza mkataba baada ya muda niliuza na kununua ya kwangu.
- Licha ya kuwa nimeingia katika Biashara ya Korosho lakini pikipiki sijaacha kwani hunisaidia katika delivery
Pia Sasa Bado naendelea na BODABODA lakini kutokana na mabadiliko ya teknolojia Sasa naendesha Pikipiki mtandao(Bolt&Paisha) leongo langu nikuweza kukuza mtaji wangu zaidi.
AJIRA
Kwa kweli sitamani kuajiriwa kwani nafurahia maisha ya kujiajiri.Kuhusu kazi yangu ya UALIMU nimenunua Eneo ambalo malengo yangu ni kujenga shule yangu mwenyewe na ujuzi wangu nitaenda kuutoa hapo.
MALENGO YANGU
Nikuwekeza katika Biashara ya mafuta ya Alizeti na Sasa nimeanza kununua baadhi ya vifaa vya mashine ili niwe na mashine yangu mwenyewe ambayo nitaifunga na kuwekeza katika mkoa ambao hupatikana zao hilo

Upvote
11