Jinsi cia alivyo iba teknolojia ya ussr

Jinsi cia alivyo iba teknolojia ya ussr

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,261
Reaction score
9,733
CIA, MWIZI WA DARAJA LA KWANZA.

Tarehe 25, Mei mwaka 1961, aliyekuwa raisi wa taifa la Marekani kipindi hicho John. F Kennedy alihutubia bunge la Congress ambapo aliweka lengo la Marekani kumpeleka binadamu wa kwanza mwezini katika kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe hiyo.

Hiki kilikuwa ni kipindi cha vita baridi kati ya Marekani na USSR, na vita hiyo ilikuwa imehamia katika mbio za kiteknolojia za anga za juu kila mmoja wao akijaribu kudhihirishia mwenzake kuwa yeye ndiye mbabe wa teknolojia hiyo.

Kama inavyofahamika USSR ndiye aliibuka kidedea kwa kuwa wa kwanza kurusha chombo kilichofanikiwa kuweka satellite ya kwanza ijulikanayo kama Sputnik I katika anga za juu.

Tukio hili lilifanyika tarehe 4, mwezi wa 10 mwaka 1957, na bado USSR akawa wa kwanza kumpeleka binadamu wa kwanza anga za juu , mwana anga huyu anajulikana kwa jina la Yuri Gagarin, hilo lilifanyika mwaka 1961, tare 12 mwezi wanne.

Mafanikio haya ya USSR yalizidi kuipa kihoro Marekani na kujiona wako nyuma ya USSR na kuhisi kwamba watadharaulika mbele ya jamii ya kimataifa maana Marekani ilikuwa ikijinasibu kuwa mbele kwa kila kitu, kuanzia uchumi, elimu, teknolojia n.k.

AIBU ISIYO SAHAULIKA.

Kutokana na mafanikio yalionyeshwa na USSR, huku Marekani akizidi kuonekana kwamba yuko nyuma kapigwa bao na mpinzani wake, zilifanyika juhudi za haraka ili marekani naye apeleke chombo anga za juu apate kuhudhihirishia ulimwengu kuwa hayuko nyuma wala USSR siyo mbabe wa teknolojia kama ambavyo watu akiwemo raia wa Marekani wenyewe walivyoanza kuamini.

Hivyo wakaja na Project Vanguard ambayo iliharakishwa ili wapate kurusha rocket yao itakayobeba satellite na kuipeleka kuiweka katika mzunguko anga za juu. Project hii iliwahishwa ikawa mapema kuliko muda waliokuwa wamejiwekea, lengo tu ni kutaka kujibu mapigo ya USSR aliyekuwa akiwapa kihoro na kuwafanya waonekane si lolote si chochote katika teknolojia ya anga za juu.

Tarehe 6, Dec, mwaka 1957, mbele ya camera za Tv za Marekani, mamiliion ya raia wa Marekani na dunia kwa ujumla wakiwa mbele ya TV zao tayari kushuhudia chombo cha Marekani kikirushwa kupeleka satellite anga za juu, ili kudhihirishia ulimwengu kuwa hata wao Marekani siyo taifa la mchezo katika teknolojia ya anga za juu.

Lakini mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa, sekunde chache tu baada ya rocket kuwashwa, ulitokea mlipuko mkubwa na moto mkubwa ulitawala anga. Rocket ya Marekani na satellite iliyobeba vyote vililipuka katika mlipuko huo.

Hii ilikuwa ni aibu sana kwa Marekani, na waliadilika dunia nzima kwasabau tukio lilikuwa live ili wapate kujinasibu na kuionyesha dunia kuwa USSR si lolote si chochote mbele ya teknolojia yao.

Rais J.F Kennedy baada ya hili tukio alinukuliwa akiwapongeza na kukiri wazi wazi kuwa USSR wako mbele yao katika teknolojia hiyo.

MKAKATI WA KUPORA TEKNOLOJIA YA USSR

Kutokana na mafanikio ya USSR katika teknolojia ya kuruhswa vyombo anga za mbali, USSR ilianza kutamba mbele ya Marekani huku ikizidi kutangaza kuanza mikakati ya kurusha vyombo zaidi anga za juu.

Hili lilizidi kuwatia hofu wa Marekani hasa ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni kipindi cha vita baridi na waliogopa kuwa USSR inaweza kutengeneza satellite ambayo itakuwa inachunguza anga la Maekani na kutishia usalama wa taifa hilo.

USSR kutaka kuonyesha uwezo wao wakaanzisha matembezi ya maonyesho kuonyesha teknolojia yao na uwezo wao katika Nyanja mbalimbali ikiwemo viwanda na uzalishaji, kilimo pamoja na teknolojia ya anga za juu.

Maonyesho hayo yalipofika Marekani, CIA wakaona hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuiba teknolojia ya USSR wapate mbinu anazotumia katika teknolojia yake waweze nao kuboresha vyombo vyao wapate kufanikiwa katika mashindano hayo.

Kwakuwa engine ya Lunik chombo ambacho kilitumika kupeleka satellite ya Sputnik I katika anga za juu ilikuwa ni moja ya kati ya vitu vilivyoletwa katika mamonyesho, CIA wakapanga mkakati ni jinsi gani wanaweza kupata taarifa za ni jinsi gani engine hiyo ilivyotengenezwa na inafanyaje kazi.

Lakini hofu yao ikawa ni juu ya engine hiyo kama ni engine halisi au ni mfano wa engine, maana walihisi USSR haiwez kuwa wajinga kiasi cha kwamba walete engine halisi katika maonyesho hayo, tena katika nchi ya mahasimu wao.

Katika kuhudhuria kwenye maonyesho hayo, waligundua kuwa ni kweli engine ile ni halisi japo baadhi ya vifaa vya umeme na kielektroniki vilikuwa vimeondolewa na walipata kujua taarifa za juu kuhusu mfumo wa engine ile lakini taarifa hizo zilikuwa hazijitoshelezi kuweza kuwasaidia kutengeneza engine yao hivyo walipaswa kuja na mkakati mwingine ambao utawawezesha kuweza kuwa na uwezo wa kuwa na hiyo engine kwa ukaribu zaidi.

Hivyo CIA walipanga mkakati wa kuiba engine hiyo na kuisoma mfumo wake kasha kuirudisha mahali pake, pasipo USSR kujua. Mkakati huu ulikuwa mgumu maana engine ilikuwa inalindwa muda wote na haikuwa rahisi hilo zoezi kufanikiwa.

LUNIK MIKONONI MWA CIA

CIA walikuja na plan mbili

Mosi, waliona njia moja wapo ni kuingilia msafara wakati engine hiyo inasafirishwa kwa gari kutolewa katika maonyesho kupelekwa kituo cha treni ambapo itahifadhiwa kwa ajili ya kupandishwa treni kesho yake kupelekwa mji mwingine.

Pili, ni kuiba hiyo engine wakati itakapo fikishwa kituo cha treni ili wqafanye kazi yao ya kuichunguza na kuirudisha kabla USSR hawagundua.

Katika plan hizo mbili, waliona plan ya kwanza ndiyo nzuri hivyo waliamua kutumia plan ya kwanza.

Jambo la kwanza walilolifanya ni kuhakikisha gari litakalo beba engine ya Lunik kutoka katika maonyesho kuipeleka kuihifadhi katika kituo cha treni, linachelewa kuondoka ili liondoke likiwa la mwisho na hilo na hili liliwawezesha kujua kama intelijensia ya USSR ilikuwa ikilinda msafara wa Lunik wakat wa kuisafirisha, jambo ambalo walikuja kugundua hakukuwa na ulinzi wowote wakati wa kusafirisha Lunik kutoka katika maonyesho kwenda kituo cha treni.

Hivyo waliamua kuchukua hatua kwa kuingia kwenye gari ambalo lilibeba Lunik na kumlazimisha dereva aliyekuwa akiliendesha kutoka kwenye gari , kasha wakaweka dereva mwingine na Yule dereva wa awali akapewa rushwa na kupelekwa hotelini kula raha ambako alimalilzia usiku akiwa na vimwana, ambapo Lunik iliondolewa kwenye gari na kupelekwa aktika jingo la karibu lililoandaliwa kwa kazi ya kuichunguza.

Kwa kutumia wataalamu, CIA wwalifungua na kuitenganisha ile engine wakapiga picha kila kifaa, na kukusanya taarifa kwa kadri walivyoweza usku kucha bila kuacha alama yyte itakayoonyesha kuwa engine hiyo ilifunguliwa.

Ilipofika sa kumi asubuhi, kazi ilikuwa imekwisha engine imefungwa vizuri, ikapakiwa kwenye gari husika nna dereva wa awalli alirudishwa tayari kwa engine kupelekwa kituo cha treni na kuifadhiwa kama inavyotakiwa.

Saa moja kamili afisa aliyetakiwa kuhakikisha kila kitu kiko sawa alifika kituoni, na alikuta gari lililobeba engine ya Lunik lipo likiwa na engine kama kawaida hivyo hakushtuka kuwa kuna jambo lisilo la kawaida lililotokea na hawakuweza kuhisi chochote, wakapakia mizigo yao kwenye treni na kuelekea mji mwingine kuendelea na maonyesho.

Kwa wizi huu Marekani iliweza kutengeneza engine bora zaidi zilizoiwezesha nao kuweza kurusha satellites na binadamu kwa mafanikio kwenda anga za juu.

HITIMISHO

Imeandikwa kutoka na vyanzo mbalimbali vya mtandao baada ya CIA kuachia mafaili yao ya siri kama ambavyo sheria inavyowataka kuacha mafaili flani kila baada ya muda flani.

Luna_2_Soviet_moon_probe.jpg
 
Attachments

  • SP.jpg
    SP.jpg
    9.5 KB · Views: 193
  • GAZ.jpg
    GAZ.jpg
    250.9 KB · Views: 179
  • FA.jpg
    FA.jpg
    7.8 KB · Views: 172
Hapo inasemekana hakuna cha USSR wala USA the men behind all space technology were stolen Hitler scientists.
Marekani waliwaiba wanasayansi wa Hitler mwaka 1945 Bila kujua urusi wameshafanya hayo kitambo mwishoni mwa ww2
Na njia za chini kwa chini mafaili, wanasayansi na mitambo ilisafirishwa kwa siri hadi Moscow na red army.
Kikosi maalumu cha us pia kilikuwa kazini kuwatafuta popote walipojificha wanasayansi wa Hitler.
 
Operation Paperclip
 
View attachment 520644
Wote ni wezi tu,chanzo cha technology yote hiyo ni wanasayansi wa ujerumani ambao wote USSR na US waliwaiba kipinf cha mwisho wa vita ya pili ya dunia.Technology zote za kijeshi wanazoringa nazo Russia na US kwa sasa ni Research findings za Wajerumani.Hakuna jipya hapo,So wote ni wezi wa daraja la kwanza.
 
Saivi files zinaibwa kimtandao zaidi,,Udukuzi
 
Wote ni wezi tu,chanzo cha technology yote hiyo ni wanasayansi wa ujerumani ambao wote USSR na US waliwaiba kipinf cha mwisho wa vita ya pili ya dunia.Technology zote za kijeshi wanazoringa nazo Russia na US kwa sasa ni Research findings za Wajerumani.Hakuna jipya hapo,So wote ni wezi wa daraja la kwanza.
Ila aisee wajeruman wanaonekana ni shida Sana japo sasa hiv wametulia tu ila nazan bado wana tabia za babu yao Hitler
 
Hizo ni tech za Wajerumani, Wanasayansi smart na Nguli kabisa, Ndio tujifunze kuwq sayansi haikufanyi u lead dunia kuna kitu kinaitwa Management na Ujanja ujanja unakufikisha pazuri, Ukiwa stable financialy, Viva US leo uko apo ulipo sio kupitia wazawa no ni Wajerumani na Waisrael ndio wametumika kukufikisha apo
 
Wote ni wezi tu,chanzo cha technology yote hiyo ni wanasayansi wa ujerumani ambao wote USSR na US waliwaiba kipinf cha mwisho wa vita ya pili ya dunia.Technology zote za kijeshi wanazoringa nazo Russia na US kwa sasa ni Research findings za Wajerumani.Hakuna jipya hapo,So wote ni wezi wa daraja la kwanza.
Yaani Hitler angemiliki nyuklia cjui dunia ingekuwa imekwisha...au wana sayansi wake walikuwa wanachelesha kutengeneza bom hilo kwa makusudi maana walishamuona hamnazo kichwani[emoji16] [emoji16]
 
Jamaa alikuwa na kila sifa na uwezo wa kutawala dunia sema walimuwahi,vinginevyo duhh
Jamaa angetawala miaka kibao
 
Back
Top Bottom