Jinsi elimu yetu ilivyovurugwa na utandawizi

Capital

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,468
Reaction score
1,063
Wandugu wana JF

nilikuwa napitia kitabu cha binti yangu anayesoma darasa la nne kwenye kishule flani jina nalihifadhi... nimevutiwa kuangalia kitabu hiki baada ya kumuuliza maswali rahisi lkn akashindwa. nimegundua yafuatayo:

1. Mtu aliyeandika kitabu hiki hafahamu vema alichokiandika.

2. Uidhinishwaji wa kitabu ili kitumike kwa watoto wadogo wa darasa la nne inaonesha dhahiri umegubikwa na sintofaharm kwani kitabu kimejaa makosa tena ya wazi, na mtunzi wa kitabu alikopi na ku paste..

3. Kitabu kimeandikwa kwa lugha ngumu na hata content ni ngumu kuweza kueleweka na mtoto wa darasa la nne, ukiachilia mbali lugha kuwa ya kingereza. hii syllabus ni ya kidato cha kwanza na si darasa la nne

4. Walimu wanaofundisha hili somo yumkini hawana uelewa hata kidogo kuweza kuwafundisha watoto wakaelewa. moja ya tatizo ni lugha, "walimu" wengi ktka hivi vishule hawajui kiingereza na mwajiri huwataka waongee na wafundishe kwa lugha hiyo tuu. sasa pale mwalimu lugha inapokuwa shida, huishia kuwaambia watoto ku copy yaliyomo ndani ya kitabu bila maelezo yoyote.

nimepiga picha baadhi ya maeneo kweye hiki kitabu ambako kwa mtazamo wangu naona iko shida
 

Attachments

  • IMG442.jpg
    402.9 KB · Views: 81
unalipomuuliza maswali rahisi akashindwa?so hapo tatizo la author wa kitabu au huyo dogo jinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…