Jinsi Ex wangu alivyoniharibia binti yangu inaniuma sana

Rafiki wa mama au uncle akaamua kula na yai kabisa
 
Nivosoma uo mstari wa mwisho nimecheka mpaka mavi ya ng'ombe amekuja kuchungulia simu.
 
Huyo kama ni mtoto wangu namfukuza kwangu na ninakata undugu nae yeye na mama yake kabisa.
 
Kuna dalili za wazi kabisa kwamba huyo binti alikuwa anaenjoy 'uhuru' usio na mipaka huko kwa mama yake hivyo kupofusha reasoning ya akili yake.
 
Mwanzo wa story yako tumefanana, mimi dogo wa kiume, mama yake alifanya kama huyo wa kwako alivyofanya, tofauti mimi sikuwa na kazi na ndo nilikuwa nimemaliza shule mwaka wa pili tu mtaani, nilichukia wanawake wote na siwaamini moaka leo, ni kipindi ambacho bila neema ya Mungu unaweza kuua au ukajiua, dogo sasa yuko form two anasonga mbele hivyo hivyo ila cha moto nilikiona.

Sometimes wanawake ni wajinga sana hasa hawa walugulu.
 
Daah ila binafsi huwa inaniumiza kuona binti mdogo anajifungulia nyumbani huku hana ramani yoyote na aliezaa nae, nae ni walewale ama lah hamtaki kabisa.

Wazazi jitahidini kuwapa elimu dunia watoto wenu hasa wa kike. Akiingia mtaani mwanaume wake wa kwanza ndie ataanza kumpa elimu ya mahusiano tena kwa kujipakulia minyama ili ale vizuri.
 
Oh ni stori ya kusikitisha sana,lakini ungejaribu kumrekebisha huyo binti yako
 
Hivyo unavyojisikia, ndivyo alivyojisikia baba wa huyo mzazi mwenzio.

Imagine huyo kijana anakuja kumjulia hali binti yako halafu anasema amezaa nae na hawezi kumuoa.

Mkuki kwa nguruwe....
Pole sana, Familia.
 
mwanamke hana akili kabisa anamuacha mtoto wa kike kwa rafiki yake wa kiume?
Itakuwa Alikuwa anajua kila kitu kuwa mwanae anatoka na Huyo Jamaa wa mama wa uswahilini ndio walivyo na usikute alikuwa Anapewa pesa na Huyo Jamaa so ikawa ameamua kubariki hayo mahusiano, hapo hakuna cha kumuacha wala nini mchezo mzima ulikuwa upo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…