MORIO15
Member
- Oct 13, 2016
- 32
- 48
Figo zina jukumu kubwa katika mwili, siyo tu kuchuja uchafu kwenye damu ili kuepukana nao, pia kuratibu madini yaliyomo ndani ya damu, shinikizo la damu na kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu.
Figo huwa zinakaa karibu na tumbo mbele ya ukuta wa mgongo na ziko mbili kila upande wa uti wa mgongo. Zinapata damu kutoka kwenye mishipa ya ateri moja kwa moja kutoka kwenye mshipa mkuu wa aota na kuirudisha damu hiyo moja kwa moja kwa mishipa ya veini kwenda kwenye vena cava.
Figo zina uwezo wa kufuatilia kiwango cha umaji maji wa damu, kuongezeka kwa madini kama vile sodiamu na potasiamu na tindikali kwa mwili mzima. Huchuja uchafu wa vyakula vilivyosharabiwa mwilini. Uchafu mkubwa unaochujwa mwilini ni pamoja na urea ya nitrojeni (blood urea nitrogen-BUN) na creatinine (Cr).
Damu inaposhuka kwenye figo, vichocheo vyake huamua kiasi cha maji kiende kuwa mkojo kulingana na uwingi wa madini yaliyomo ndani ya damu. Kwa mfano, kama mtu anaharisha au ameishiwa na maji kutokana na ugonjwa mwingine, figo huzuia maji yaliyopo yasiende kuwa mkojo na hapo mkojo huwa wa njano.
Lakini kama maji yako mengi mwilini, mkojo huwa na maji na msafi. Kazi hiyo hufanywa na homoni inayoitwa renin ambayo huzalishwa na figo ikiwa ni sehemu ya uratibu wa shinikizo la damu na hali ya mwili.
Figo pia huzalisha homoni ya ‘erythropoietin’ ambayo huchochea uti wa mgongo kuzalisha chembechembe nyekundu za damu. Kuna seli maalumu katika figo ambazo huratibu kiwango cha hewa ya oxygen ndani ya damu. Kama kiwango hicho kitashuka ‘erythropoietin’ huongezeka na kuchochea uzalishaji wa chembe nyekundu za damu.
Baada ya figo kuchuja uchafu, mkojo huzalishwa na kupelekwa kwenye kibofu kupitia mrija wa ureta. Hutunzwa hapo ukisubiri mtu, mnyama akojoe.