Jinsi gani naweza pata angalau 300,000

Jinsi gani naweza pata angalau 300,000

Sister Abigail

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2020
Posts
2,886
Reaction score
9,088
Habari,

Je, unaweza nishauri nifanye kitu gani naweza pata angalau 300,000 ndani ya muda sio mrefu sana?

Nahitaji kuanzisha biashara ndogo ntayoimudu maana nahisi kuchokwa nyumbani. Umri unaenda sana na ulemavu umenikwamisha sana, najiona ka ng'ombe yani. Sina boyfriend, sina mchumba, nimeishia form 4, sijasoma zaidi.

Michezo naogopa maana marejesho ntakosa yakanikuta mazito, maana sina chanzo cha mapato. Betting sijui pia naogopa michezo ya Bahati nasibu, ntaliwa tu.

Nimefanya udalali wa magari na nyumba ila nliambulia padogo sana, ni mgumu kwangu.

Kitu gani naweza fanya kupata hiyo amount? Penye wengi hapakosekani litalofaa.
 
Back
Top Bottom