Jinsi gani unavyoweza kutumia makampuni/ viwanda kujitengenezea fursa/ kipato na kutimiza ndoto zako

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2019
Posts
491
Reaction score
1,010
Kutokana na changamoto tuliyonayo ya ukusefu wa ajira huku ongezeko kubwa la wahitimu wa nyanja tofauti tofauti likizidi kila mwaka.

Niukweri ulio wazi kuwa hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kuwaajiri wahitimu wake wote ispokuwa nchi za wenzetu wamewekeza zaidi katika teknolojia (technology ) hivyo wengi wao wakijitengenezea vipato kupitia teknolojia.

Ukosefu wa ajira umetengeneza kundi kubwa la wahitimu wanaolandalanda mitaani na kushinda mitandaoni bila kujua nini hatima ya maisha yao ya badae huku wale walobahatika kufanikiwa katika nyanja tofautitofauti wakiwacheka na kuwabeza wakisahau kuwa hata wao mika 5,10 au 15 nyuma walipita wanapopita wenzao sasa.

Zana ya kujiajiri imekuwa ni lugha rahisi anayoweza kuitumia mtu yeyote kumwambia mwenzake bila kuhusisha uhalisia wa neno na mazingira halisi.

Hakuna kijana anaependa kuwa maskini, hakuna kijana anaependa kumtegemea mwingine, hakuna kijana anaependa kuwa chini ya mtu. Kila kijana anatamani kuwa bossi wa mwenzie, kila kijana anataka kuishi maisha bora na kuwa na uhuru wa kifedha bali kinachomtesa ni jinsi yakupata mtaji na connection ya fursa.

Wakuu hebu turudishe kumbu kumbu zetu nyuma miaka 5,6,8 ,10 au 15 na wengne hata zaidi ya 20 tukumbuke tulipomaliza coz, kipindi ambacho tulikuwa mtaani tukitafuta upenyo wakupitia kufikia malengo. Wengi tulishughulika na shughuli tofauti tofauti zilizotupa mitaji au kutufungulia fursa kubwa zaidi na kufika tulipo leo ili kumtia moyo na kumuhamasisha kijana wa leo kwa vitendo huku akijifunza kitu kupitia story hizo.

Miongoni mwetu kuna ambao uwepo wa viwanda na makampuni katika maeneo tunayoishi ulipelekea kubadili maisha yetu. Hebu wakuu fungukeni mlitumiaje makampuni na viwanda kupata fursa, mitaji, ujuzi na connection na vilichangiaje Mafanikio yako ya sasa.

Je kijana anawezaje kutumia makampuni na viwanda kupata mtaji, ujuzi, fursa na kujikwamua kiuchumi.?

Kijana anawezaje kuwa balozi wa kampuni? Anawezaje kutengeneza business partner na kampuni? Kijana anawezaje bila mtaji wowote kuitumia kampuni kupata pesa?
 
Nimekuja hapa mbio mbio nikijua kuna mbinu za kujikwamua kupitia viwanda kumbe ni story tu.
 
Kampuni au kiwanda chochote kinategemea mauzo,kwa elimu uliyonayo jaribu kuwatafutia wateja kwenye bidhaa zao..kama unaweza kufikia asilimia fulani ya mauzo wanaweza wakakupatia uwakala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…