Jinsi gani ya Kuanzisha kiwanda kidogo cha Sukari?

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
1,026
Reaction score
1,749
Wadau Habari Za wakati huu!

Niende moja kwa moja kwenye maada, nimekuwa nikifanya survey katika maeneo flani huko mikoa ya nyanda za juu kusini na kugundua kuwa kuna malighafi nyingi ya miwa. Hivyo nimepata wazo la kuanzisha kiwanda kidogo cha sukari.

Hivyo naomba wenye ujuzi na hatua za kuanzisha kiwanda hiki wanipe mwongozo ili niufanyie kazi.

Ningependa pia kujua gharama za mashine na mambo mengine.

Karibuni kwa michango na maoni.
 
Yaani nimesubiria wajitokeze lakini hawaji ...
Tatizo ni moja ... unaposikia neno MAMLAKA ... Ujue ni kikundi cha kuweka kauzime kwenye shughuli fulani inayo husiana na ...
Hapa anza kwa kutafuta vikwazo vinavyoweza kujitokeza toka mamlaka ya sukari nchini .. then Mamlaka ya Chakula na Dawa ...
 
Katika survey yako, malighafi ya miwa uliyoiona na kuigundua ni miwa kwa aina/mbegu zipi ...maana miwa ya kukamuliwa sukari sio hii tunayotafuna inatembezwa na wachuuzi, lakini pia uzani/ujazo upoje? Maana unaweza kuta na ukashangaa miwa tani 1 kuzalisha sukari kilo 200/250 tu ..nadhani ukianzia wizara ya viwanda, wizara ya biashara, ya chakula kote huko unaweza pata taarifa zaidi ingawa jiandae kwa urasimu, au tafuta mtu mwenye ngozi ya kung'ara awe partner wako muwe mnaongozana huko ( itasaidia kukurahisishia milolongo ingawa si ajabu ukaombwa hongo) , pia tembelea kituo cha uwekezaji katika kanda yako ( TIC zonal/regional office)
 
Mkuu usiogope tafuta eneo nzuri angalau acres 100+ la kwako then panda miwa taratibu , huku ukiwa unatafuta machines za ku process. TFDA and TBS watakupa malekezo nini ufanye uweze kuiweka sokoni sukari yako
 
Maarifa hutafutwa Mkuu, usikate tamaa kama uko serious!
Tunaweza tusikujibu humu kwa vile nasi tunaweza tusiwe na uelewa wa kutosha. Mimi cha kukusaidia tafuta mawasiliano ya Chuo cha Sukari cha Taifa (National Sugar Institute). Chuo hiki kipi Kidatu, kilipo kiwanda cha sukari Kilombero (kwa sasa Illovo). Kuna kikundi cha akina mama kiliwahi patiwa mafunzo pale, wakawa wanatengeneza sukari yao. Naamini utapata pa kuanzia.
 
Hapo kwenye URASIMU, sijui nani katuloga.....suala la rushwa hapo halikwepeki kabisa...tunakwamishana kweli....
 
Asante sana mdau kwa mchango wako! Nitayafanyia kazi mawazo yako! Barikiwa sana!
 
Hapo kwenye URASIMU, sijui nani katuloga.....suala la rushwa hapo halikwepeki kabisa...tunakwamishana kweli....
Ni kweli mkuu hili suala limeota mizizi sana! Sasa hivi polisi wameongezeka sana kwenye patrol za doria na barabarani, lakini wakikukamata na kosa lolote utasikia haya tuongee! Ukiwashikisha pesa tu, uko huru! Kwa hiyo hapo utaona lengo si kuthibit uhalifu bali kuufanya uhalifu kuwa kitegauchumi chao binafsi! Dawa ni kuwafanya kama Sabaya, unwapa alafu badaye unawageuzia kibao!
 
Maarifa hutafutwa Mkuu, usikate tamaa kama uko serious!
Tunaweza tusikujibu humu kwa vile nasi tunaweza tusiwe na uelewa wa kutosha. Mimi cha kukusaidia tafuta mawasiliano ya Chuo cha Sukari cha Taifa (National Sugar Institute). Chuo hiki kipi Kidatu, kilipo kiwanda cha sukari Kilombero (kwa sasa Illovo). Kuna kikundi cha akina mama kiliwahi patiwa mafunzo pale, wakawa wanatengeneza sukari yao. Naamini utapata pa kuanzia.
Asante sana mkuu! Umenivusha pakubwa mno! Mawazo yako nitayafanyia kazi, Barikiwa sana mdau!
 
Mkuu usiogope tafuta eneo nzuri angalau acres 100+ la kwako then panda miwa taratibu , huku ukiwa unatafuta machines za ku process. TFDA and TBS watakupa malekezo nini ufanye uweze kuiweka sokoni sukari yako
Asante sana mkuu, mawazo yako nitayafanyia kazi!
 
Ni kweli mkuu hili suala limeota mizizi sana! Sasa hivi polisi wameongezeka sana kwenye patrol za doria na barabarani, lakini wakikukamata na kosa lolote utasikia haya tuongee! Ukiwashikisha pesa tu, uko huru! Kwa hiyo hapo utaona lengo si kuthibit uhalifu bali kuufanya uhalifu kuwa kitegauchumi chao binafsi! Dawa ni kuwafanya kama Sabaya, unwapa alafu badaye unawageuzia kibao!
ni kweli....ila ishi ukitengeneza marafiki sio maadui.....ukiamua kumpa mpe....songa zako mbele.....ila nikuunge mkono kwa wazo lako.....hizi kitu zisikukatishe tamaa hata kidogo bro....pigania unachokiamini...
 
Sawa mkuu nimekupata!
 
Maarifa hutafutwa Mkuu, usikate tamaa kama uko serious!
Tunaweza tusikujibu humu kwa vile nasi tunaweza tusiwe na uelewa wa kutosha. Mimi cha kukusaidia tafuta mawasiliano ya Chuo cha Sukari cha Taifa (National Sugar Institute). Chuo hiki kipi Kidatu, kilipo kiwanda cha sukari Kilombero (kwa sasa Illovo). Kuna kikundi cha akina mama kiliwahi patiwa mafunzo pale, wakawa wanatengeneza sukari yao. Naamini utapata pa kuanzia.
Nipo interested na hii taarifa honestly, umenifumbua macho

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom