mwanateknolojia
JF-Expert Member
- Nov 17, 2014
- 1,026
- 1,749
Wameungana na TIRDO wanawaza usingiziSIDO na TEMDO ni uzi wenu huu jamani, niungeni mkono mwekezaji mzawa!
Hapo kwenye URASIMU, sijui nani katuloga.....suala la rushwa hapo halikwepeki kabisa...tunakwamishana kweli....Katika survey yako, malighafi ya miwa uliyoiona na kuigundua ni miwa kwa aina/mbegu zipi ...maana miwa ya kukamuliwa sukari sio hii tunayotafuna inatembezwa na wachuuzi, lakini pia uzani/ujazo upoje? Maana unaweza kuta na ukashangaa miwa tani 1 kuzalisha sukari kilo 200/250 tu ..nadhani ukianzia wizara ya viwanda, wizara ya biashara, ya chakula kote huko unaweza pata taarifa zaidi ingawa jiandae kwa urasimu, au tafuta mtu mwenye ngozi ya kung'ara awe partner wako muwe mnaongozana huko ( itasaidia kukurahisishia milolongo ingawa si ajabu ukaombwa hongo) , pia tembelea kituo cha uwekezaji katika kanda yako ( TIC zonal/regional office)
Asante sana mdau kwa mchango wako! Nitayafanyia kazi mawazo yako! Barikiwa sana!Katika survey yako, malighafi ya miwa uliyoiona na kuigundua ni miwa kwa aina/mbegu zipi ...maana miwa ya kukamuliwa sukari sio hii tunayotafuna inatembezwa na wachuuzi, lakini pia uzani/ujazo upoje? Maana unaweza kuta na ukashangaa miwa tani 1 kuzalisha sukari kilo 200/250 tu ..nadhani ukianzia wizara ya viwanda, wizara ya biashara, ya chakula kote huko unaweza pata taarifa zaidi ingawa jiandae kwa urasimu, au tafuta mtu mwenye ngozi ya kung'ara awe partner wako muwe mnaongozana huko ( itasaidia kukurahisishia milolongo ingawa si ajabu ukaombwa hongo) , pia tembelea kituo cha uwekezaji katika kanda yako ( TIC zonal/regional office)
Ni kweli mkuu hili suala limeota mizizi sana! Sasa hivi polisi wameongezeka sana kwenye patrol za doria na barabarani, lakini wakikukamata na kosa lolote utasikia haya tuongee! Ukiwashikisha pesa tu, uko huru! Kwa hiyo hapo utaona lengo si kuthibit uhalifu bali kuufanya uhalifu kuwa kitegauchumi chao binafsi! Dawa ni kuwafanya kama Sabaya, unwapa alafu badaye unawageuzia kibao!Hapo kwenye URASIMU, sijui nani katuloga.....suala la rushwa hapo halikwepeki kabisa...tunakwamishana kweli....
Asante sana mkuu! Umenivusha pakubwa mno! Mawazo yako nitayafanyia kazi, Barikiwa sana mdau!Maarifa hutafutwa Mkuu, usikate tamaa kama uko serious!
Tunaweza tusikujibu humu kwa vile nasi tunaweza tusiwe na uelewa wa kutosha. Mimi cha kukusaidia tafuta mawasiliano ya Chuo cha Sukari cha Taifa (National Sugar Institute). Chuo hiki kipi Kidatu, kilipo kiwanda cha sukari Kilombero (kwa sasa Illovo). Kuna kikundi cha akina mama kiliwahi patiwa mafunzo pale, wakawa wanatengeneza sukari yao. Naamini utapata pa kuanzia.
Asante sana mkuu, mawazo yako nitayafanyia kazi!Mkuu usiogope tafuta eneo nzuri angalau acres 100+ la kwako then panda miwa taratibu , huku ukiwa unatafuta machines za ku process. TFDA and TBS watakupa malekezo nini ufanye uweze kuiweka sokoni sukari yako
ni kweli....ila ishi ukitengeneza marafiki sio maadui.....ukiamua kumpa mpe....songa zako mbele.....ila nikuunge mkono kwa wazo lako.....hizi kitu zisikukatishe tamaa hata kidogo bro....pigania unachokiamini...Ni kweli mkuu hili suala limeota mizizi sana! Sasa hivi polisi wameongezeka sana kwenye patrol za doria na barabarani, lakini wakikukamata na kosa lolote utasikia haya tuongee! Ukiwashikisha pesa tu, uko huru! Kwa hiyo hapo utaona lengo si kuthibit uhalifu bali kuufanya uhalifu kuwa kitegauchumi chao binafsi! Dawa ni kuwafanya kama Sabaya, unwapa alafu badaye unawageuzia kibao!
Sawa mkuu nimekupata!ni kweli....ila ishi ukitengeneza marafiki sio maadui.....ukiamua kumpa mpe....songa zako mbele.....ila nikuunge mkono kwa wazo lako.....hizi kitu zisikukatishe tamaa hata kidogo bro....pigania unachokiamini...
Nipo interested na hii taarifa honestly, umenifumbua machoMaarifa hutafutwa Mkuu, usikate tamaa kama uko serious!
Tunaweza tusikujibu humu kwa vile nasi tunaweza tusiwe na uelewa wa kutosha. Mimi cha kukusaidia tafuta mawasiliano ya Chuo cha Sukari cha Taifa (National Sugar Institute). Chuo hiki kipi Kidatu, kilipo kiwanda cha sukari Kilombero (kwa sasa Illovo). Kuna kikundi cha akina mama kiliwahi patiwa mafunzo pale, wakawa wanatengeneza sukari yao. Naamini utapata pa kuanzia.