Mkuu
Kimbori kwa waislam ni hivi
HUKUMU ZA KUMWOSHA MAITI
Ni fardhi juu ya kila Mwislamu kumwosha maiti huyo, na kutengeneza mazishi yake yote, lakini wakishajitokeza watu kumshughulikia huyo maiti basi kwa wengine fardhi hiyo huondoka.
- Ni haramu mwanamke kuoshwa na mwanamume, au mwanamume kuoshwa na mwanamke, lakini mke ana weza kumwosha mume hata kama wapo wanaume, na mume anaweza kumwosha mke hata ikiwa wapo wanawake wa kumwosha.
- Mwanamume anaweza kumwosha mtoto wa kike asiyezidi miaka mitatu, na pia mwanamke anaruhusiwa kumwosha mtoto wa kiume asiyezidi miaka mitatu.
- Ikiwa hakuna mwanamume wa kumwosha mwanamume, wanawake walio karibu naye kwa ujamaa na damu wanaweza kumwosha, kama mama, dada, shangazi, mama mdogo (dada wa mama yake). Vivyo hivyo ikiwa maiti mwanamke na hakuna mwanamke wa kumwosha huyo maiti, basi majamaa waliokaribu naye kwa ujamaa na damu wanaweza kumwosha kama baba, ndugu, na mtoto wake na wale ambawo ni haramu kumuoa, kwa kisheria wanaitwa "MAH-RAM".
- Mtoto aliyezaliwa kwa kuharibika mimba, ikiwa mimba iko chini ya miezi minne (bado hakukamilishwa umbo lake) huyu hana haja ya kuogeshwa (kumuosha GHUSLI), ni lazima aviringishwe katika kitambaa na akazikwe. Lakini mimba ya miezi minne au zaidi (aliyekamilika umbo lake), lazima aogeshwe na kuvikwa sanda kama desturi.
- Mwenye kumwosha maiti lazima awe mwislamu, tena Shia, na awe amebalehe, mwenye akili, na ajue namna ya kumwosha maiti.
- Ni fardhi kumwosha Mwislamu hata akiwa wa madhehebu nyingine, lakini utamwosha kwa mujibu ya Madhehebu ya Shia lthnaasharia tu.
- Mwosha maiti anapomwosha maiti anuwie kama ninafanya kazi hii Qurbatan llal-Laahi Taala, na vitu vyote avitumiavyo kwa kumwosha maiti viwe vya halali, si vya kunyang'anya au kuiba hata maji na mahala atumiapo wakati wa kumwosha maiti pawe pa halali.
SUNNA ZA KUMWOSHA MAITI
- Awekwe mahala palipo juu, kama kitanda, au baraza n.k. na mahala pa kuwekea kichwa chake painuke zaidi kuliko miguu.
- Alazwe chali, miguu na nyayo zielekee Qibla (kama tulivyotaja katika mambo ya hali ya 'IHTIDHARI'.
- Maiti avuliwe nguo zote kwa upande wa chini (miguuni) hata ikibidi itatuliwe (ichanwe) lakini kwa idhini ya warithi wa maiti.
- Aoshwe chini ya sakafu, au banda au hema asioshwe chini ya mbingu.
- Uchimbwe "UFUO" wa kuingia maji ya kuoshea.
- Mwili wake wote uwe wazi isipokuwa utupu wake.
- Ufunikwe utupu wake hata ikiwa mkoshaji au watu wanaomuosha ni miongoni mwa wale wanaoruhusiwa kumwangalia.
- Mkoshaji apitishe mkono wake juu ya tumbo la maiti kwa taratibu lakini ikiwa maiti mwenye mimba ambaye mtoto pia amekufa tumboni hairuhusiwi kufanya hivyo.
- Mkoshaji asimame upande wa kulia wa maiti.
- Aanze kuosha upande wa kulia wa kichwa cha maiti.
- Mkoshaji aoshe mikono yake mara tatu hadi begani kwa kila 'GHUSLI' tatu.
- Mwoshaji anapokuwa anaosha kiwiliwili cha maiti anatakiwa aseme hivi: "Ewe Mola! Hiki ni kiwiliwili cha mja wako mwenye imani (Mumin) na umetoa roho yake kutoka kiwiliwili chake, na umetenga kati yao, basi msamehe kwako." Hasa wakati anapomgeuza.
- Asitangaze mwoshaji aibu yoyote aliyoiona mwini mwa maiti.
UTARATIBU WA KUMWOSHA MAlTI
(a) Baada ya kusafishwa mwili wake wote kwa sabuni (au kitu kingine) na kuondoshwa uchafu wa aina yo yote kama (madawa, marhamu au mafuta) ndipo huyo mwoshaji Mwislamu atamwosha ghusli tatu (mara tatu kuoshwa). Ni sunna kabla ya kuanza kumwogesha maiti ghusli tatu, atamwosha mikono yake mara tatu, kwa kila ghusli.
(b) Kwa mara ya kwanza, atachanganya katika maji ya kumwoshea maiti kidogo SIDRI (majani ya mkunazi) kwa kutia katika pipa la maji anachochotea maji ya kumwoshea huyo maiti (atayafikicha yale majani yapate kutoa harufu), wala asitie majani mengi hata maji yawe mudhafu. Baada ya kumaliza ghusli ya kwanza atakisuza kile chombo (pipa) kuondoa harufu ya Sidri.
(c) Na kwa mara ya pili atamwosha kwa maji yaliyochanganishwa na 'Kaafuri' (Karafu maiti) kidogo tu, wala asitie nyingi hata maji yakawa mudhafu. Tena atasuza pipa baada ya kumaliza ghusli ya pili ili kuondoa harufu ya Kaafuri.
(d) Na kwa mara ya tatu atamwosha (ghusli) kwa maji haya ya kawaida yaliyo safi bila ya kuchanganywa na cho chote, na hii ndio mara ya mwisho. Ni sunna mwoshaji katika muda anapomwosha maiti awe anasoma, "AFWAN AFWAN".
HADHARI: Taratibu zote za kuosha ni lazima zifuatwe na kama si hivyo GHUSLI ya maiti hubatilika na ni lazima uanze upya kwa utaratibu ule ule tuliyoueleza.
Kwa hivyo huyo maiti wa Ki-Islamu baada ya kuoshwa ghusli tatu hizo kama tulivyoeleza, sasa atakuwa ametaharika, Mwislamu yo yote akimgusa wakati huu, hakuna haja ya kuoga kwa yule mwenye kumgusa, lakini
ikiwa baada ya kutoka roho na kupoa mwili, na kabla hajapewa (maiti) hizo ghusli tatu, akimgusa tu kwa mwili (si juu ya nguo) basi kwa kila mwenye kumgusa ni fardhi juu yake aoge "ghusli massul Mayyit", (ghusli ya kumgusa maiti). Na ghusli (kuoga) hiyo ni faradhi kwa mujibu wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.) tu.
NAMNA YA KUMWOSHA MAITI
Baada ya kusafishwa mwili wote wa yule maiti hapo (yule mwoshaji) atanuia kuwa, namwosha (huyu maiti) ghusli ya kwanza kwa maji yaliyochanganyishwa na majani ya mkunazi kama tulivyoeleza huko nyuma.
(a) Kwanza ataanzia kwa kummwagia maji kichwani (maji yafike hadi utosini kwenye ngozi) masikio, pua, mdomo, macho na shingo pia aoshe. Ahakikishe kilmara anapomwosha, maji yafike sehemu zote za mwili wake.
(b) Tena upande wa mbele wa kulia kutoka begani chini ya shingo na pote kulia hadi kwenye nyayo tena baadaye amlaze ubavu amwoshe sehemu ya nyuma kama alivyomwosha sehemu ya mbele ya kulia.
(c) Baadaye atamwosha upande wa mbele wa kushoto na baadaye upande wa nyuma kama alivyomwosha upande wa kulia.
(d) Utupu wa maiti lazima uoshwe anapokoshwa kila upande (maana yake kwa kila mwosho (ghusli) ataosha utupu mara mbili). Ni haramu kuangalia utupu wa maiti na mwoshaji akiangalia ametenda dhambi, lakini ile ghusli haibatiliki.
(e) Mwoshaji wakati anapoosha utupu wa maiti Iazima aviringe kitambaa au avae mfuko wa kitambaa mkononi, ni haramu kupeleka mkono upekee.
Hii ndio namna ya kumwosha maiti ambayo utaratib huo kwa kisheria unaitwa "ALGHUSL AT-TAR-TIBI" na inambidi kwa kila mwenye Janaba pia akitaka kuondo (kuoga) Janaba au mwanamke mwenye hedhi au nifasi au kuoga ghusli za sunna lazima waoge vivyo hivyo kama tulivyoeleza katika kitabu chetu cha Sala (mlango wa ukurasa wa 33).
Kwa kuoshwa ghusli tatu hizo, tena haina haja kumwogesha, ghusli ya janaba au hedhi au nifas ikiwa maiti alikuwa katika hali ile.
Ikiwa SIDRI (majani ya mkunazi) au KAA-FUR (Kafuri maiti) zote mbili au mojawapo haipatikani, basi maiti ataoshwa kwa maji haya ya kawaida kwa nia ya badala ya Sidri au Kafuri mradi lazima maiti aoshwe Ghusli tatu tu (mara tatu).
(a) Ikiwa maji hayapatikani au maiti ameungua au alikuwa na maradhi fulani na akitiwa maji nyama au ngozi itatoka, basi badala ya maji atafanyiwa Tayamamu mara tatu kwa Ghusli tatu.
(b) Tayamamu ni lazima ifanywe na yule hai, na kumpaka maiti, na kama inamkinika kutayamamu kwa mikono ya maiti pia ifanywe - (Namna ya Tayamamu angalia kitabu chetu cha 'Sala' ukurasa wa 44 Mlango wa 8).
MAMBO YA FARADHI BAADA YA KUOGESHWA MAITI HADI KUZIKWA KWAKE
Haifai wakati anapooshwa maiti kuweko moto au kiteso cha kufukiza wala wakati wa mazishi hadi mwisho.
AL-HUNUUT: Kupakwa maiti kafuri mahali maalum ni faradhi kwa Waislamu baada ya kumwosha na
kupanguswa (afutwe vizuri kwa nguo kavu) maiti kabla ya kusaliwa na kuzikwa apakwe 'Kafuri' laini sehemu
saba (viongo vya kusujudia) navyo ni kipaji, viganja viwili, magoti mawili, ncha za vidole gumba viwili. Na sunna
kupakwa kwenye pua, vile vile sunna kuwekwa pamba kwenye utupu wa maiti na kila penye tundu. Wakati wa
kupaka HUNUUT ni baada ya kuogeshwa na kupanguswa na kabla ya kuvikwa sanda au wakati wa kuvikwa sanda.
Ikiwa Kafuuri haikupatikana hatakumwoshea maiti, basi hapo faradhi ya HUNUUT inaondoka, na kama amekogeshwa na Kafuuri lakini haikuzidi kwa ajili ya HUNUUT basi si kitu.
AL-HUNUUT: Kupakwa maiti Kafuri ni faradhi kwa kila maiti mdogo, mkubwa mwanamke, mwanamume, huru
au mtumwa isipokuwa maiti yule aliyekufa hali yuko katika Ihramuni haramu kumpaka Kafuri. Kafuri lazima iwe
mpya si kukuu yenye kupotea harufu yake, na pia lazima iwe laini iliosagwa.
SANDA YA MAITI ILIYO WAJIBU
Ni faradhi kuvishwa maiti mwanamume au mwanamke mkubwa au mdogo vipande vitabu vya nguo:
(1) Kanzu (2) Shuka (3) Shuka
(1)
Kanzu: Bila kuishona, itobolewe sehemu ya shingo tu halafu kitumbukizwe kichwa. Kuanzia begani hadi nusu ya miguu kupita goti.
(2)
Shuka:Kama anavyovaa mwanamume kutoka kitovuni
hadi magotini, na ni bora si wajibu kuanzia kifuani hadi chini ya magoti.
(3)
Shuka:Kitambaa kikubwa cha kumfunika mwiIi wake wote mzima mbele na nyuma kwa urefu hata uweze kufunga pande zote mbili (upande wa kichwa na upande wa miguu) na kwa upana, ncha moja iweze kuja juu ya ncha va pili
SUNNA: Si wajibu bali ni sunna (a) Kuvishwa mwanamume kiIemba, mwanamke sidiria na ushungi (b) Nguo nyeupe isiyokuwa na rangi yoyote (c) Nguo iwe ya pamba (d) Ni bora kama aliwahi kuhiji basi 'IHRAMU' itumiwe au nguo za kusalia ambazo akisali nazo.
SANDA: Kwa kiasi kilichofaradhi lazima gharama yake na gharama ya vitu vya kumwoshea maiti, maji, Sidri, Kafuri, ardhi pa kuzikiwa na gharama zake zote haya hutoka katika asili ya mali ya maiti kabIa ya kulipwa deni
au kufuatwa wasia wake. Na yako mambo ya sunna katika sanda ikiwa ameusia sanda itolewe katika theluthi (1/3) ya mali yake, au ameusia theluthi ya mali atumiliwe yeye basi sanda itatolewa humo, na kama hakuusia
theluthi (1/3) basi kiasi kilichowajibu kitatolewa katika asili mali.
Sanda ya mke juu ya mumewe hata ikiwa mke anayo mali ya kutosha, na vivyo hivyo yule mke aliyeachwa kwa
mara ya kwanza au ya pili na bado yupo katika eda, mume lazima atoe sanda. Ikiwa mtu mwingine yoyote
ametoa sanda ya yule maiti (mwanamke) basi faradhi humuondokea mume.
Ni sunna kwa kila mwislamu kutayarisha SANDA yake na kuiweka nyumbani, pia ni sunna kuiangalia hiyo sanda
kila mara. Mtukufu ,Mtume (s.a.w.) amesema, "Mwenye kutayarisha sanda yake, huwa kila siku zipitazo kila
huandikwa thawabu kila apoiangalia, na kwa kufanya hivyo hatahesabiwa miongoni mwa waliomsahau Mwenyezi Mungu.
NAMNA YA KUMKAFINI (KUMVISHA SANDA MAITI)
Baada ya kukatwa mapande hayo, kwanza utatandika ile shuka kubwa ya Namba 3: Na ndio ya kwanza, baadaye utatandika Kanzu Kanzu kwa kuikunjua upande mmoja, (na hii ni ya pili), baadaye utaliweka shuka
kwa upana kwa kukunjua. Ukisha tandika yote hayo vipande vitatu vya vitambaa vilivyo wajibu, basi sasa atalazwa maiti juu ya mapande yote ya sanda.
- Kwanza utamfunga shuka na kuondoa kile kitambaa ulichotumia wakati wa kumwoshea kuficha utupu wake.
- Utaurejesha ule upande wa kanzu ulioukunjua kwa kupitisha kichwa cha maiti kwenye shingo.
- Ikiwa umeshafanya mambo ya 'AL-HUNUUT' basi utaikunja hiyo shuka kubwa kwa kuiweka ncha moja juu ya pili, na kama bado hujampaka AL-HUNUUT na mambo yake basi fanya, ndipo umalize kumfunika.