Jinsi gani ya kutoa mzigo bandarini mwenyewe bila Wakala?

Bonobo

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2017
Posts
364
Reaction score
670
Habari wakuu?
Naomba niende kwenye hoja ya msingi,

Kuna mzigo nimeagiza kutoka china, sasa umekaribia kufika... wakati nafikiria jinsi ya kuutoa bandarini, nikakumbuka kuna kipindi lilitoka tamko kuwa mtu mwenyewe(nikimaanisha mwenye mzigo) ana uwezo wa kufanya clearance ya mzigo wake mwenyewe bila ya kutumia agent...

Ishu ya msingi inakuja hapa, je hyo ishu ni kweli inafanyika? Na kama inafanyika, je hatua ni zipi?
Na kama haifanyiki, je niangalie vigezo gani kumchagua agent?

Naombeni msaada wenu katika kujua hili...

Asanteni.
 
huwezi kuingia bandarini kama sio Clearing Agent.
 
mtafute member anaitwa Mwl.RCT huyo atakupa msaada kamili kwa sababu ana uzoefu na hayo mambo
 
Nadhani kama mzigo nikwa matumizi ya kawaida inawezekana kwakuwa uliandika adress ( namba ya simu na posta) ukifika utaambiwa uende ukachukue na ukifika utakutana na wafanyakazi wa TRA Customs watakupigia kodi then ukilipa unapewa mzigo wako.
 
Mimi nimewahi kuagiza memory card,cameras, laptop etc sema ilikuwa ni enzi za JK kilichofanyika mizigo nilikuta posta na sikutumia agent wa aina yeyote nikalipia ushuru nikachukua vitu vyangu sijafahamu siku hizi utaratibu ukoje
 
Mkuu ulisikiliza bunge la bajeti 2019/2020?

Na ile taarifa ndo imenipelekea kuweka hili bandiko... lakin inaonekana watu wamelitazama kama nimeandika kitu cha ajabu mno...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…