Jinsi Habari Muhimu za Tanzania Zinavyopatikana kwa Bei Kubwa





Wazee kama mmesoma post yangu hapo juu mtaona kuwa niliona bora ni widhraw ile hoja yangu ya awali ya JF kuchangia kununua hizo articles kwa sababu ambazo hapo awali sikuziona wakati na post

Vile vile naweza kusema kuwa hii ilikuwa inachangiwa zaidi na ile vision yangu ya awali ya kutaka kuona JF inakuwa jaidi ya FORUM bali inakuwa ni ONLINE NEWSPAPER ambayo forum ni kama part yake.


Hvyo kwa sababu naona kuwa hiyo idea kidogo itakuwa labda iko too ambitious lakini nikaonelea bora niingize hoja ya pili ya kutaka members ambao walijiandikisha na hawachangii au tuseme wamekuwa DORMANT au kwa jina lingine wanaitwa ma LURKERS wafutwe uanachama kwa sharti kuwa WAKITAKA KUINGIA KWENYE MAIN FORUMS KAMA ZA SIASA BASI ITABIDI WALIPIE lakini haimaanishi hawatoweza kuingia kwenye forums zingine..ila wawe na limited access


sababu hiyo ilikuwa ni kama njia mojawapo ya kuongeza revenue kwa hii website na njia ya pili ambayo inaweza ikawa efective ni ile ya kuwa na ONLINE ADVERTS KWENYE MAINPAGE kwa hii siongelei matangazo haya ya google bali nazungumzia BANNERS kubwa ambazo zinaweza kusaidia katika kufanya malipo madogo madogo kama ya kuongeza nafasi ya server iliyopo ambayo kadri mda unavyozidi inazidi kuwa kubwa kutokana na watu wengi wanavyooingia pamoja na ukubwa wa mafaili

Vile vile tusisahu kuwa watu kama INVISIBLE nao wanahitaji kuishi na sioni ubaya kama na yeye akawa anapata walau vijisenti vya kununulia siagi badala ya kula mkate mkavu


Najua kuna baadhi wanaogopa kuwa mamabo ya kulipia yakianza watu watataka kupata nafasi zaidi lakini nadhani haya ni mambo ambayo yanaweza kuwa ironed out tuuu kwani umoja wetu ni muhhimu zaidi kuliko utengano wetu lakini zaidi ya yote ni kuwa TUSIJIDANGANYE, hii webite haiwezi kurun ki mungumungu, ni lazima iwepo Business Plan na ndio maana nikaona bora nitumie nafasi hii kueleza kuwa ile hoja ya awali si muhimu sana lakini hii ya kuendesha hichi chombo kama biashara ni muhimu zaidi.Nimeona sikuhizi hata blog mbili tatu zina matangazo sasa sembuse hii webiste yenye members zaidi ya miatatu na traffic isiyo na mfano?

anyway tuendelee ku brainstorm mwelekeo na mawazo zaidi
 
Vile vile naweza kusema kuwa hii ilikuwa inachangiwa zaidi na ile vision yangu ya awali ya kutaka kuona JF inakuwa jaidi ya FORUM bali inakuwa ni ONLINE NEWSPAPER ambayo forum ni kama part yake.
Mkuu Theory

Heshima mbele mkuu, ila nilii-overlook hii point ya kuwa Online Newspaper, anyway great thinking keep it up!
 

Hata mimi siliungi mkono hili wazo la kuchangia kwa sababu linaweza kusababisha kupoteza wanachama wengi ambao hiyo dollar 10 ni pesa nyingi sana. Hili watu kusoma habari hapa JF bila kuwa wanachama lisituumize vichwa kwani wengi huanza hivyo na hatimaye huamua kuwa wanachama rasmi.
 
Ndugu wa nchi hii ya kuelekea kusikojulikana,

Mimi nakubali kuchangia ila iwe tu kwa wanaoweza. Binafsi nipo tayari kutoa hiyo dola 10 kwa mwaka sina tatizo. YES Invisible lazima ale mkate kwa siagi. Hiyo ni very true!

Ila mchango uwe wa hiari. Wenye moyo wachache wanaweza kuiendesha hii forum bila tatizo, ninaamini tupo na tunaweza kufika 100 kama tukichanga 10 kila mtu itakuwa ni dola 1000 sio mbaya itakuwa imesaidia kwa kiasi fulani.

Ninahitisha HARAAAMBEEEE!

Invisible andika

1. FD .............USD 20
2.
3.
4.
5.
6.
.
.
1000.

Asanteni
 
Binafsi kama ikinza michango itakuwa ngumu kuhuddhulia hapa. Nauli yenyewe mzozo, internet natumia ya ofisi na makolokolo kibao mengine.

Mimi tuendelee kukata ishuz tu kama mwenye kutaka kuchangia ruksa lakini sio hao luckers wafutiwe uanachama. Hao luckers ndio akina Nchimbi na Karamagi wanasoma nao humu
 
Unajua hii JF is what it is because of people like you in London, DC, Detroit and we in Buguruni, Sinza kwa Remmy nk! Ni kweli Invisible ana haki ya kula siagi (hata kama wengine huo mkate mkavu hatuupati) lakini kikubwa ni kujiuliza, hii FORUM ilianzishwa kwa malengo gani? Maana kwa uelewa wangu hii forum haibagui kabisa mwenye nacho na asiye nacho, mkuu kulipa dola kumi kwa mtu ambaye hana uhakika na nauli ya dala dala ni kuumizana. Nawafahamu watu wanao jinyima ili waingie Internet cafe kuchungulia humu JF tuu.

Hapana wewe ongea na invisible na wenzako huko majuu muanzishe forum nyingine ya kudiscuss mambo ya kikubwa..sisi tunakuja humu kuchungulia na kupata busara za akina Kyoma, Mkandara, MKJJ, Dua, Kada. FMES nk, ukisema tulipe basi utakuwa umefukuza wengi na JF haitakuwa JF unayoiona leo. Sio kwamba napigia debe vitu vya bure, hapana, najaribu kuangalia upande wa pili wa shilingi. Kama mkuu hujui kwa bongo internet ni lulu unaweza kulipa mpaka elfu kwa dakika kumi na tano na huko mikoani ndo balaa! Wakati majuu net mko nazo mpaka vyumbani.

Naomba ubuni mradi mwingine wa kusustain hii website au vingenevyo invisible abadirishe madhumuni ya kuanzishwa kwa hii kitu. Na wewe hujui hao unaosema walipishwe ndo tunawatafuta kila siku waje humu,

Mseveni aliwahi kuulizwa na Benki ya dunia kwa nini wakaramajong hawalipishwi gharama katika hospital za serikali? akawajibu, "nchi yangu ni maskini, lakini kabla ya kumlipisha huyu mtu, ni vema kwanza ukamuelewesha umuhimu wa kwenda hospitali na hii ni pamoja na kumtibu bure kusudi aelewe umuhimu wa kwenda hospitali".

Kwa hiyo sisi hapa JF tunataka wananchi waamke, watoke usingizini, sasa lazima tukubali kubeba hizo gharama, kwanza tushukuru kuona siku hizi mawazo yetu yameanza kuwa na impact na JF inakuwa source of info. for different news media..ni hatua kubwa na nzuri... Labda ndo mchango wa invisible katika hili la kuhabarisha umma. na wewe jitoe pale unapoweza. MKUU INTERNET KATIKA NCHI YETU BAAADO SANA Sasa ukianza kuwambia watu walipe kuaccess some info. utakuwa unarudi nyuma.
 
Masanja nakubaliana nawe kabisaaaaa

yakianza mambo ya kuchangishana hapa hii Forum itakuwa ya wachache kama ccm ilivyo ya matajiri na wezi wachache
 

..haya mawazo,yametulia!
 
Hata hivyo tatizo la kuchangia ni kuwa italazimisha watu kudisclose their identinty in a certain way na hivyo itaondoa utamu wa forum yenyewe!

..ukaitwa mzee mwanakijiji!

..kijijini mtu hawezi kufa njaa kirahisi...hata mizizi atakula!

..busara za kijijini zidumu!
 

..hawa wanaoingia hapa bure na wako wengi ndio wanaoifanya forum iwe melting pot ya nguvu!

..sasa,kuchangia ni muhimu. kuwalazima watu kuchangia ni kitu kingine tofauti!kwani,wengine weshachangia kwa nyeti wanazozi-post hapa!
 
..hawa wanaoingia hapa bure na wako wengi ndio wanaoifanya forum iwe melting pot ya nguvu!

..sasa,kuchangia ni muhimu. kuwalazima watu kuchangia ni kitu kingine tofauti!kwani,wengine weshachangia kwa nyeti wanazozi-post hapa!

..Naona nimedandia mkuki ktk motion, anyway nimevutika na texts nilizoquote hapo juu.
Naamini kuwa labda bila JF pia leo mawaziri wasingezomewa huko waendako kuupaka uongo rangi. Na bila JF wengi wasingekuwa wadadisi kujua nini kinaendelea. Cha msingi ninachoshauri wakuu wa Jf ni kushirikiana na wanaJF makini ktk kutafuta wadhamini ili hatimaye sie walalahoi tusiokuwa na uhakika wa mlo mmoja tusitozwe. Au labda sijamwelewa dasilamu kuwa kuchangia huko ni kwa namna gani??

JF idumu na iendelee kukomboa fikra za watanzania watoke ktk mzingo wa kutofahamu yanayotokea.....
 
Masanja Chukua Tano(ongea kwa lafidhu ya kisukuma)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…