Jinsi hofu inavyochakaza mwili na roho

Jinsi hofu inavyochakaza mwili na roho

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,317
Reaction score
1,320
Wana jf wote ninawasalimu.

Moja kwa moja kwenye mada, siku za hivi karibuni baada ya kuzuka kwa tetesi zilizohusisha afya ya raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. JPM na HABARI nyingi kuandikwa mitandaoni na watu wengi kuchangia kwenye mada hizo nikiwemo na Mimi pia.
Watu walijiachia vya kutosha kwa kuonyesha hisia zao za ndani, wachache walionyesha kufurahishwa taarifa hizo feki na wengi walihuzunishwa sana.
Ila Mimi nami niliziingia kichwa kichwa HABARI hizi na kujimwaga kwelikweli kama wengine walivyofanya sasa NINAJUTA maana hofu niliyonayo sasa inanichakaza nimekuwa kama mgonjwa.

Hofu imeongozeka sana baada ya kwamba taarifa hazikuwa sahihi bali ni uzushi na pia matamko ya viongozi kuashiria kukasirishwa sana na uhuni huo wa kimtandao, jeshi la polisi kuanza kuwasaka na kuwakamata wazushi au wasambazaji na hata wale wote walioonyesha kufurahia kutokuonekana hadharani kwa amiri jishi mkuu.
Wana jf hofu yangu itapunguzwa sana kwa kujibiwa maswali yafuatayo
(1) je jf yetu bado iko salama au imeshadukuliwa na taarifa zetu zipo kwa kayafa
(2) Ni mbinu gani nitumie ili kuepuka kutumbukia mikononi mwa watesi wetu wakati wote ninapotumia jukwaa hili
(3) Nitamtambuaje na kumkwepaje adui anayefuatilia nyendo zangu humu jf
Jamani nisaidieni kupunguza hii hofu inayoendelea kunitafuna sina amani kabisa
Ahsanteni sana ni mm mdogo wenu kutoka ikhanoda, ninatakia jioni njema wote
 
Acha uoga japo ata mm uwa siiamini JF mtu unaandka Uzi,Comment aafu mods au mtu mwingne anauwezo wa Kuedit uzi/comment au ata kuufuta c ufala uo?? Naamini ata uko PM mods wanaweza kuingilia faragha ya wana JF bila shda yoyote chakufanya...

1.Washa VPN mda wowote unapotumia internet iwe fb,twita,IG,JF n.k n.k ndio silaha ya kwanza yaani

2.hapa JF lock PM au uwe na ID tofauti na Mods wasikujue utakula Ban takatifu

3.Tumia code/Tafsida ktk kuelezea mambo yako usipende kujielezea yaani

4.Kama ni Fb fungua acc nyngne na usiweke picha yako
 
Ahsanteni sana ila 2 kulock pm ndio sielewi kabisa
 
Back
Top Bottom