DOKEZO Jinsi Ifakara ilivyotekwa na kukithiri magenge ya uhalifu na matapeli wa mtandaoni maarufu kama halo-haloo

DOKEZO Jinsi Ifakara ilivyotekwa na kukithiri magenge ya uhalifu na matapeli wa mtandaoni maarufu kama halo-haloo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Ndarakishe

Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
6
Reaction score
8
Habari wanajamvi,

Wilaya ya Kilombero eneo la Ifakara limekumbwa na wimbi la MATAPELI WA MTANDAONI maarufu kama halohaloo. Tumejaribu kila njia kuripoti katika vyombo vya usalama lakini hakuna hatua zozote zinachukuliwa dhidi ya MATAPELI Hawa..

Cha kusikitisha polisi wilaya ya Kilombero haswa OCD wamewageuza kama vitega uchumi, wanawakamata na kuwaachia bila hata kuwafikisha mahakamani kwa kuwachaji fedha Kati ya elfu 80 Hadi 100,000.

Vijana Hawa wakiongozwa na kiongozi wao maarufu wa biashara hiyo ya utapeli kwa jina MAISHA, amekuwa akijitapa kuwaweka mfukoni polisi na vyombo vyote vya usalama hawana cha kuwafanya.

Hawajifichi wala hawaogopi yeyote, ni wengi mnoo kiasi kwamba ni kama vile hakuna serikali wilayani Kilombero.

Maeneo yaliokithiri ni LUMEMO, MAHUTANGA, KIKWETA, NA HASWA MAKAO YAO MAKUU NI ENEO LA LUMEMO KIJIWE CHA MADUKA MATATU AU KWA SAMSAM

Wamekuwa wakibaka, kupora na kutishia usalama wa wananchi katika maeneo hayo. Cha kushangaza vijana wote wanafahamika na wote wanaoendesha genge Hilo na uhalifu likiongozwa na kijana aitwae MAISHA, Udindo, Libao na wengine wengi sana.

Kama wananchi tunaomba msaada Serikalini ktk ngazi za mkoa au taifa maana kwangazi hii ya wilaya wameshindwa.
 
Huku kanda ya ziwa watu kama hao wakikamatwa mara ya kwanza polisi wakawaachia, wakirudia mara ya pili polisi watafata maiti zao,,
 
Hii
Uliyosema ni kweli mtupu, pia Minarani karibu na Asante lodge, kuna kijiwe cha boda kwa mbele. Aisee wapo weeengi sana boda zao km tatu tuu kazi ni hiyo ya halo halo.
 
Vijana Hawa wakiongozwa na kiongozi wao maarufu wa biashara hiyo ya utapeli kwa jina MAISHA, amekuwa akijitapa kuwaweka mfukoni polisi na vyombo vyote vya usalama hawana cha kuwafanya.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🫢
 
Habarini jamvini,

Bado Hali ni mbaya mnoo na ya hatari Kwa wakazi wa vijiji vya LUMEMO, MAHUTANGA KIKWETA, IFOZA, KATINDIUKA IFAKARA kutokana na MAGENGE ya uhalifu wa MTANDAONI walioweka makazi ya kudumu katika kata nilizozitaja hapo juu.

Wahalifu hao hawajifichi na wanafanya uhalifu wao wazi huku kukiwa na askari kata haswa MAKAO YAO MAKUU LUMEMO, askari kata anazo taarifa zote za matokeo ya kiuhalifu lakini amekalia kimya, hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa dhidi ya wahalifu hawa.

Wananchi wamechoshwa na vitendo vinavyofanywa na vijana Hawa maarufu kama halo haloo,wanabaka watoto,ukabaji na biashara ya MADAWA ya kulevya hadharani.

Tumetoa taarifa Kwa OCD wilaya, Mkuu wa wilaya, na viongozi wote wanazo taarifa wa wilaya lakini hakuna hatua wanachukua.

Cha kustaajabisha wahalifu Hawa wanajitapa kuwa na mahusiano mazuri na jeshi la polisi kuanzia askari kata Hadi OCD Kwa kuwapa mgao. Wamekuwa wengi na ngumu mnoo Kwa wananchi kujilinda dhidi ya vitendo vyao.

Jamii imekumbwa na taharuki na hakuna msaada wowote wa vyombo vya ulinzi na usalama ktk kukomesha Hali hii.

Wako wazi na vijiwe vyao vinafahamika,makao makuu Yao ni LUMEMO,mtaa wa Kwa mnola KIJIWE CHA samsam au maarufu maduka MATATU.wanauza bangi hadharani na uporaji.

Na hata kumpiga na kumchezesha kipigo askari wa kata ya LUMEMO.je sisi wananchi nani wa kutusikuliza?nani wa kutuondolea kero hii kama vyombo vya usalama vimeshindwa?

Tunaomba kilio cheti hiki kimfikie Mama Raisi Samia halihii ikomeshwe. Hatuishi Kwa raha,hatutumi watoto dukani bila usaidizi imekuwa kama darfur ndogo wanavyoiita. Viongozi wa serikali ifakara ni mzigo, to they are rotten to the core,vyombo vya usalama ndio vimepwaya wazi kabisa.

Wanawakamata wanawachaji fedha na sku mbili wamesharudi mtaani huku wakijitapa serikali na vyombo vyote vya usalama viko mikononi mwao.usalama wanafanya kazi Gani? Kama mimi mkulima na mlalahoi wa TAC nimeuona udhaifu huu?!?hatuna amani viongozi wa juu tusaidiane Hawa wilayani ni mzigo mkubwa
 
Hao matapeli wa "Haloo Haloo" wanatapeli vipi, elimu kidogo.

Ila Ifakara mna road barabara nzuri sahivi ya kufika Kilombero (Ruaha). Mji wenu utakua sana.
 
Back
Top Bottom