Jinsi jamaa alivyomkomesha mchawi

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Mzuqa,

Hii niliipataga Chuga kijiweni miaka ya nyuma.

Jamaa huko Shinyanga ghetto kila akianza kulala kuna mchawi tena jirani yake anaanza kumpiga juju kwa kumbughudhi kwa kelele za sauti za ajabuajabu. Kugongagonga mlango na madirisha.

Akifungua mlango kumfukuza mchawi anamwonyesha mbwembwe kwa kuruka mipapai. Mara nyingine huyo mchawi anajigeuza anakuwa mtoto mchanga kabisa na kwa muda wa dakika tano anakua kutoka kichanga mtoto, teenager, kijana, makamo hadi mzee. Na baadaye kurudi umri wake wa kawaida.

Yani ilikuwa kero. Hii ilikuwa kwaanzia saa tatu hadi saa sita usiku. Yani mida hii huyu mchawi alikuwa akipasha kabla hajakutana na wenzake kupangiana majukumu mengine ya kuwanga. Alichagua kwa jamaa ndio pakupasha.

Ikifika saa sita usiku kabla hajaondoka alikuwa anajitawaza kwenye kona ya kuta baada ya kujisaidia hovyohovyo kwa kujikwaruza kwa fujo juu chini juu chini. Jamaa akiamka asubuhi anauzika kweli kuta imetapakaa mabaki ya mavi.

Wazo zuri likamjia. Akaamua kuchukua vipande vya nyembe na chupa na kuvibandika kwa kuvigongelea kwa ustadi anapopenda kujitawaza.

Jamaa ilipofika saa tatu akazima taa nakujifanya analala. Mara ghafla mchawi akafika. Kampiga juju ya hatari siku iyo tena mfulululizo masaa matatu.

Ilipofika saa sita kasorobo usiku akaanza kutandaza marvi hadi mlangoni. Msela akawa nasubiria kwa hamu muda wa kujitawaza.

Saa sita ilipofika wizard akaenda kwa fujo kujitawaza kwe kona ya ukuta.

Kilichofuatia hapo ni kelele ya hatarii na matusi juu . "Wee ngesay umenikatakata marinda yangu kwa uchungu namna hii bila huruma"?

Asubuhi watu kuamka damu zimetapakaa kwenye kuta
 
Du hiyo noma
 
Hii chai kabsaa tena inamechanganywa na tangawiziπŸ˜€
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahaaa ila jamaa hakuwa mchawi huyo alitaka kumtisha tu mwenzie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…