Jinsi kalio la jirani lilivyozua kizaazaa leo

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Dunia ina mambo na vijimambo nami nashukuru nimefanikiwa kushuhudia vituko vingi mno maishani mwangu. Ni majuzi tu hapa nimeshuhudia kisanga cha aina yake baada ya kalio la jirani yangu kuzua balaa.

Jina lake aliitwa Sakina. Ni jirani yangu kwani kwangu na kwake wala si mbali. Kama walivyo waswahili wengine, naye hajawahi kuweka wazi umri wake. Hata hivyo, kwetu sisi wenye jicho la tatu, tuna uhakika lazima atakuwa na miaka 26.
Alijaaliwa sura nzuri sana na rangi ya maji ya kunde, nywele zake zilikuwa habari nyingine, hakuhitaji kuvaa wigi jirani yangu huyo. Japo alikuwa mzuri katika kila idara, alikosa kitu kimoja, hakuwa na kalio kabisa. Yaani huko nyuma palikuwa ‘flat’ kama chapati vile. Basi jambo hilo lilimkosesha raha. Vijana wa mtaani waliomtongoza akawakatalia walimuumiza zaidi walipomwambia, “mwanamke mwenyewe tako huna… una ringa nini?”

Baada ya muda jirani yangu Sakina alipotea hata tukaogopa kwa kudhani labda alitekwa na watu wasiojulikana. Kumbe alikwenda sehemu kutafuta suluhisho la matatizo yake. Alihitaji kuongeza kalio lake, hivyo akampata rafiki mmoja aliyempeleka kwa mtaalamu ambaye alimpatia dawa za kichina tayari kabisa kwa kuyajaza maumbile ya nyuma!
Basi bwana, baada ya miezi kadhaa, Sakina akarejea akiwa kafungasha kwelikweli, kalio lilijaa vyema na kutengeneza shepu ambayo sijawahi kuiona kokote mie!

Kwa kuwa watu walimcheka ‘hana kalio’, akaamua kuuonyesha mtaa mzima kuwa, masikini kapata matako na sasa anayaliza mbwata!
Alikodi ngoma kwa lengo la kupita mtaa mzima kuonyesha umbile lake hilo la kununua.

Akiwa na vijana wapiga ngoma na tarumbeta aliowakodi, alianza kupita kila sehemu akitikisa kalio ili watu waone! Alimaliza chochoro zote akiwatambia watu kuwa sasa yuko juu na ametimia kwa kila kitu. Hatimaye sasa akafika katika kijiwe nilichokaa mimi na masela kibao ambao mpaka leo hatuna ajira japo tuna degree kubwa kubwa kutoka vyuo vinavyoeleweka.

“Semeni tena sina tako, oooh mwanamke mkia huna unaringa nini?” Sakina alisema akitutazama, wapiga ngoma wake wakashangilia, “Oyoooooooh!”
Alipoona hatuna cha kujibu ila tunamtolea macho tu, akaanza kuzungusha kiuno chake kama mnenguaji wa bendi, watu wake wakashangilia, sisi tukabaki tukitoa macho na kujiramba kwa sinema ya bure! Alipomaliza kukata mauno, akaanza kutikisa makalio. Likitikisika hili, linafuata lile hata ikawa kama gari inawasha ‘indiketa’.

Alizidisha visa alipoona watu wanamshangilia. Sasa akaanza kurukaruka juu. Kila aliporuka kalio lilinesa isivyokawaida, watu wakashangilia, sisi tukatoa macho na kujiramba. Aliruka kalio likanesa! Akaruka tena kalio likanesa zaidi, aliporuka mara ya tatu, oooooh… salaleeeeeeh! Kalio likapasuka kwa kishindo kikubwa, “pwaaaaah!” Sakina akadondoka chini akiwa kapoteza fahamu!

Kwa sasa tumegawana majukumu. Sisi tumembeba jirani yetu Sakina tunampeleka hospitali, na wale wapiga ngoma wake, tumewaacha wanavikusanya vile vipande vya kalio la kichina.
 
Ujumbe maridhawa umefika,hii tunaita unamkejeri MTU,pasipo yeye kujua,sakina asiye na tako kubwa wapo wengi sana nchii,wakipata kario tu,mtaa mzima utajua,
Wahenga waliyaona zamani,"mswahili akipata matako ulia mbwata",
 
Hahahahahahah toka.hapa daaaah umeanza vizuri unamaliza kwa kamba staili..

Kama vipi weka picha ya vipande pande vya kalio LA kichina.
 
Kama naliona jinsi yalivyokuwa yakipishana kutikisika kama disco lights zinavyowakaga[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Angalau hii imenifurahisha...maana toka asubuhi Nina hasira moyoni maana habari zilienea kuwa nimeteuliwa kuwa waziri
 
Hakika watavikusanya vipande popote vilipo na hatuvikanyagi ng'o!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…