Jinsi kuwa milionea kabla ya miaka 30

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Mambo yako;
Najua title inavutia ila kabla sijakupa ubuyu nikuchane live kuwa mafanikio hayaji bila,mipango na bidii.

Mambo ya kwanza kwanza!!,kwa mwanamke njia rahisi zaidi ila sio kbaisa ya kuupata utajiri na kutafuta kijana tajiri mwenye bidii na maarifa ili akuoe na kwa wanaume ni kuhakikisha wewe ni kijana tajiri mwenye bidii ili umuoe msichana huyu mrembo anayetaka mwanaume tajiri.

Maisha ni mipango ni mipango yenyewe ni hii:

  • WEKEZA KWENYE ELIMU/UJUZI: Ninaposema wekeza kwenye elimu kuna watu wanawaza Sup na Disc hapana sio kukusanya vyeti nini kukusanya maarifa.Pita JF,tembe sehemu tofauti,zungumza na watu angalie videos soma vitabun.k.Tumia muda wako wa ziada sio kulalamika na kulaumu bali kuongeza maarifa na ujuzi wako.Utafiti unaonyesha kuwa kadiri mwanadamu anapokuwa maarifa sahihi huwa kujiamini kwake kunaongezeka na mtu anayejiamini ni rahisi kufanikiwa.
  • USIOGOPE KUJARIBU: Usiogopa kujaribu hasa kwa sababu ya hofu ya kushindwa au kukosea.Kila mara unapofanya jambo jipya jipe muda ujifunze hata kama utakosea fahamu kuwa kukosea ni njia bora zaidi ya kujifunza.Ninapozungumzia kujaribu namaanisha jaribu kufanya mambo ya maendeleo sio ya kipuuzi k.v.ulevi,uzinzi n.k.
  • KUWA HURU NA MAONI YAKO:Ninaposema kuwa huru namaanisha kuwa na fikra huru.Usiwe mtu wa kufuata mkumbo na kuburuizwa na mawazo ya watu na mitazamo ya watu.Usiwaze watanionaje?Watasemaje?Itakuaje na vitu kama hivyo vinavyoondoa hama.Wewe kama mtu una uhuru wa kifikra na kimtazamo na usipoteze muda wako kufuatilia watu wengine iwapo hawaongezi thamani katika maisha yako.
Tuendelee kujuzana mambo mengine ya kufanya ili uweze kuwe milionea chini ya miaka 30.NB:Nina zaidi ya miaka 30

Karibuni
 
Safi sana naamini Prince anaweza kuwa tajiri soon.
 
pendelea kujifunza kutokana na mazingira kwa maana ya kifursa,unapotembea mahal popote usitembee tu mrad umetembea,jarib kuchunguza mazingira nin kinapatikana nin kinakosekana,pia petendelea kujua/kuchunguza fikra za wenzako/jamii inayokuzunguka,pia watu waliofanikiwa weng hutumia mda mwing kufikiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…