Jinsi makabila yalivyoyumbisha ubongo na saikolojia za Mbongo

Jinsi makabila yalivyoyumbisha ubongo na saikolojia za Mbongo

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Ni vizuri wakuu turudi kwenye defaults za binadamu katika ubora wake.

Kwa nini anasema hivi, kuwa mnazi wa kikabila unaweza kujikuta umechakachuliwa akili vibaya sana na ukadhani huo ndio ubinadamu kumbe ni UJINGA.

Mfano:
1: Nimekaa na jamaa Wawili kutoka sehemu tofauti Mbeya. Hawaja jamaa wakikasirika wanaanza kuvibrate kama nyigu usoni pua zinachezacheza. Nikajiuliza walianza kwanza nje, mbona wengine wakikasirika wanareact tofauti katika uso. Nikagundua ni urithi wa kikabila.

Nimekaa na jamaa wa same. Hawa jamaa ubahiri mwingi. Hata mwenye pesa anataka aende sawa na masikini. Nikajiuliza mbona wao tu ktk makabila yote hapa. Nikafuatilia nao wamerithi tu. Tena chanzo cha ubahiri wakipare cha ajabu kabisa. Wakijua watacheka sana.

Nimekaa karibu na gereza la Ukonga nashangaa BODABODA flani. Wakati wengine wamezubaa, mmoja yuko makini kichwa kinazunguka juu kama kobra, kusaka mteja. Ghafla akatoka mbio Kali sana nikashtuka, akafika akamuhug mama flani anashuka kwenye daladala kisha akabeba Mizigo kupeleka kwenye boda yake. Wenzake wameshangaa tu. Kumsikia anaongea lafudhi ya kichaga. Nikawakumbuka wachaga Wawili wafanya biashara nikasema sawa sawa. Hawa nao wanarithi. Wale wengine waliozubaa nao ni UJINGA wamerithi kujiona bora kuliko wateja.

4: Tumekaa na Dada mmoja mchonganishi balaa. Kila kesi ukiitrace utakungua chanzo niyeye. Nilipofika Eneo jipya katika taasisi nyingine nikakuta kesi marumbano. Kila kesi kamama flani kanatajwa. Nilipokachunguza nikagundua ni std 7, kuongea Vzri hajui, hata kuandika shida ila kako vere powerful kuvuruga mambo na watu. Kuja kugundua ni Kabila moja na yule wa kule. Nikauliza nikaambiwa hao huwa wako hivyo. Wanatokea kusinikusini Kabila nimesahau. Huu UJINGA nao ni wa kurithi tu wala sio tabia za kibinadamu.

Nilivyogundua upana na unene wa hili shambulizi la ubongo kikabila nikagundua kila Kabila linatabia flani hivi za hovyo au nzuri ambazo wahusika wanaona kama ni grobal culture sio UJINGA wao tu hapo Kijijini.

Kwa nini nimeandika haya.

Wewe mwanaJF ni mtu msomi. Hata kama hujaenda Shule humu umeingia au unafuatilia IQ yako kijamii iko zaidi ya mhadhiri wa prong yang university ambaye hana bandle wala internet ya kujifunza mambo nje ya Korea kaskazini.

Acha tabia za Kijijini, za kikabila, za kurithishwa rudi katika Viwango vya ubinadamu.

Yaani unakutana na msomi Mkubwa anaamini Tunda ni parachichi tu mengine hataki sio kwa sababu hajui bali eti kwao ndio wamekua hivyo.

Anza kidogo kidogo kuachana na maujinga ya kurithishwa uwe mtu wa maana. Ika vile Vzri komaa navyo.

Yangu ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom