Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Baada ya kuufuatilia mgogoro wa Mashariki ya Congo-DRC sasa ninaweza kusema mgogoro huo umegawanyika katika robo nne.
1. Robo ya kwanza ni siasa kabisa-hapa kuna tatizo la siasa za uraia wa mipakani, ukabila na genocide ya Rwanda. Hili tatizo ni la muda mrefu tangu uhuru, limezungumziwa sana na Nyerere, Mandela, Mbeki na Kikwete.
2. Robo ya pili ni maslahi ya kiuchumi-Hapa iko Rwanda, DRC, Uganda, mafisadi wa serikali ya DRC na makampuni ya madini ya nje kila mmoja akipigania maslahi yake huku majeshi yakitumika kama nyenzo tu. Pia yapo maslahi ya uchumi ya raia wa DRC mashariki ambo ardhi yao inaporwa na kila pande kwa ajili ya uchimbaji madini.
3. Robo ya tatu ni udhaifu wa serikali ya DRC kushindwa kudhibiti nchi nzima(weak state). Sehemu yoyote isiyo na udhibiti au yenye ombwe lazima itajazwa tu na wadau wengine wawe wazuri au wabaya.
4. Robo ya nne ni udhaifu jumuiya za kikanda za SADC, Africa Mashariki pamoja na AU kushughulikia matatizo ya wanachama wake sio DRC tu lakini karibia kote Africa.