Jinsi MBS anavyoipaisha Saudia kiuchumi nje ya Mafuta

Jinsi MBS anavyoipaisha Saudia kiuchumi nje ya Mafuta

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,307
Reaction score
47,210
Inakuwaje wanajamvi!

Bwana mdogo Mohammed Bin Salman mwana wa mfalme wa Saudi sasa hivi anaipaisha nchi yake kiuchumi nje ya Mafuta kwa kasi ya ajabu na hatarii haijawahi kuonekana.
. Viwanda vinachipuka kama uyoga. Wa saudia sasa hivi bidhaa nyingi hawanunui au kuagiza kutoka nje zinazalishwa ndani.

Mfano vyakula, nguo, vinywaji zamani waliagiza kutoka nje lakini sasa hivi kwa wingi vinazalishwa nchini Saudi Arabia.

Miezi iliyopita Dogo alisitisha mara moja uagizwaji wa nyama ya Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku kutoka Brazil na turkey na kuanzisha viwanda hivyo nchini Saudi Arabia.

Kwa mfano Brazil ilipata hasara kubwa sana na kutuma waziri wao wa mambo ya nje kwenda kumuangukia bwana mdogo. Ilikuwa kampuni kubwa ya nyama Brazil mahsus tu kwa kupeleka nyama Saudia ambayo walikuwa wakichinja kiislam.

Dogo akaiwekea vikwazo Uturuki kutopeleka bidhaa saudia kwasababu ya tofauti zake na Rais Erdowan. Uturuki ikaathirika sana kiuchumi. Hadi sasa hivi wafanyabiashara wa Uturuki wanabadilish nembo za bidhaa na kudanganya zimetoka Oman nakuziingiza kwenye ardhi takatifu kinyemela.

Pia akaiwekea Lebanon vikwazo kwasababu ya kuweka madawa ya kulevya kwenye bidhaa nakuziingiza saudia. Lebanon hoi kiuchumi sasa hivi Imebidi ujumbe mzito uende Riyadh nakumuangukia bwana mdogo.

Sasa hivi bidhaa za Saudi Arabia kwaanzia nyama, maziwa, biskut, juice, matunda n.K vinapatikana kwenye shelves za supermarket ulaya kitu ambacho miaka ya nyuma haikuwepo.

Wasaudia sasa hivi wanachakarika vibarua ni wao kwenye makampuni kazi nyingi wanahodhi wao.

Pia utitiri wa vijana wa Saudi Arabia wamepelekwa nje kusoma Canada, Marekani, Australia na ulaya katika fani mbalimbali.

Kuna order za ndege nyingi MBS amefanya anataka saudia iwe na shirika la ndege kama Qatar na emirates.

Bwana mdogo anategemea sana ushauri wa kiuchumi kutoka kwa Tony Blair, David Cameron na wamagharbi wengine. Ametenga fungu kubwa la hela kwa hawa wa shauri na wamemuwezesha kufanya mageuzi makubwa katika uchumi wa ardhi takatifu. Ila hawa watu wa haki za binadamu wanawaandama sana.

Mwisho ni huu mji wa kipekee wa aina yake Neom ambao ujenzi unaendelea utaisha 2030. Yani utakuwa wa aina yake.

Sasa huku mafuta huku viwanda na huku utalii. SAUDI Arabia inachanja mbuga kiuchumi kila kukicha chini ya bwana mdogo mwenye maono na mchapa kazi Mohammed Bin Salman MBS!
IMG_20211024_205730.jpg

Saudi Arabia begins construction on the Line, 105-mile car-free 'linear city' of the future | Daily Mail Online
 
Eeeeeeeeh,huo mji utaisha mwaka 2930,kweli balaa
 
wawaachie uraiani wale akina mama wakisaudia bwana tujimwage nao....utalii uongezeke maradufu, maana dah pagumu kweli ile depo japo sasa hivi naona wanaachia hela kwa wageni..
 
Saudi Arabia begins construction on the Line, 105-mile car-free 'linear city' of the future | Daily Mail Online
 
Mtu anapigwa hapa hawakuvua viatu kwenye zulia wazungu sio bure aisee
Wenye Akili Tunajua Hapo Siyo Bure Atalia Mtu
Hiyo Alkasus Mujarab Wanakunywa Hawajavaa Msuli
Hao Wanawatengeneza Waarabu
 
Mabeberu Yatawazunguuka Soon, Ngoja Uone Sasa
Kamwe haitatokea. Katika nchi ambazo mabeberu kamwe hawawezi kuwazunguka ni ni hizo za GCc Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, UA na Kuwait ni close na Trusted allies ndo maana unaona mambo yao yananyooka.
 
Back
Top Bottom