Jinsi Mimba inavyomlinda mwanamke mjamzito

Jinsi Mimba inavyomlinda mwanamke mjamzito

Madwari Madwari

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
1,825
Reaction score
3,085
1716983200089.png

Mama anapokuwa mjamzito, chembechembe za mtoto huhamia kwenye mkondo wa damu wa Mama na kisha kuzunguka tena ndani ya mtoto, hii huitwa “fetal-maternal microchimerism”.⁠ Kwa muda wa wiki 41, seli huzunguka na kuungana kwenda nyuma na mbele(i.e kwenda kwa mama na kurudi).

Baada ya mtoto kuzaliwa chembe chembe hizo hukaa katika mwili wa mama, na kuacha alama ya kudumu katika tishu, mifupa, ubongo na ngozi ya mama.

Mara nyingi hukaa humo kwa miongo kadhaa. Kila ujauzito ambao mama atapata baadaye utaacha hizi chembe chembe kwenye mwili wake. Hata kama mimba haifikii muda kamili au ikiwa umetoa mimba, seli hizi bado huhamia kwenye mkondo wako wa damu. Utafiti umeonyesha kwamba ikiwa moyo wa mama utajeruhiwa, seli za ujauzito zitakimbilia mahali palipojeruhiwa na kubadilika kuwa aina tofauti za seli ambazo zina utaalam wa kurekebisha moyo.

Mtoto husaidia kutengeneza afya ya Mama, wakati Mama hujenga mtoto. Inapendezaje? Hii ndiyo sababu mara nyingi magonjwa fulani hupotea wakati wa ujauzito.

Inashangaza jinsi mwili ya Mama unavyomlinda mtoto kwa gharama yoyote, na mtoto humlinda na kumjenga tena Mama - ili mtoto akue kwa usalama na kuishi. Fikiria juu ya hamu ya ghafla ya kula aina ya chakula fulani ?. Je, mama alikuwa na upungufu gani kwa kuwa mtoto anamfanya awe na hamu hiyo?

Uchunguzi pia umeonesha seli kutoka kwa ujauzito katika ubongo wa mama miaka 18 baada ya kujifungua. Inashangaza kiasi gani?” Ikiwa wewe ni mama unajua jinsi unavyoweza kuhisi mtoto wako kwa njia ya angavu hata wakati hayupo.

Sasa, kuna uthibitisho wa kisayansi kwamba akina mama huwabeba kwa miaka na miaka hata baada ya kumzaa.
 
Back
Top Bottom