Joshboney
New Member
- Sep 2, 2022
- 1
- 0
Machozi yakimbubujika Zakia (KE: Sio jina halisi) kamavile mpira wa maji ya kumwagilia bustani, yakidondoka mpaka kwenye kona ya kidevu! jicho jekunduu...akashusha simu kutoka sikioni kwa haraka nakutaka kuitupa ukutani! lakini kwa kuishiwa nguvu aliishia kuigonga gonga kwenye mapaja yake akiwa amekaa chini pembeni kidogo ya jengo la maabara pale mtaani kwetu.
(Nikajisemea moyoni) Kuna nini tenaa... kakutwa na virusi au vipi.. wacha nimsogelee, geto kwenyewe sina la kuwahi mneshadaka kiepe changu ntajipoza taratibu.
Ndipo kumkuta Zakia katika ile hali.. (Siunajua uGentleman) chap kwa haraka nkatoa leso nikampa bidada yule walau afute machozi.
Kumtia moyo na kumfuta machozi na pole kedekede halikua suala la kujiuliza...
Mambo yasiwe mengi.. baada ya kupata wasaa wa kuzungumza nae.. haya yalitoka kinywani mwake.
Huku kwikwi na kuvuta kamasi kukifuata kila baada ya neno moja alosema
"Yaani huyu J, nadhani hata nikisema nimpige juju haitoshi, yani nlimwambia mapema kabisa, niko siku ya hatari na kijiti cha uzazi wa mpango sijaweka! bhas walau yeye avae ndomu (kondomu), kajitetea wee! mwishoe akavaa, tunaenda round ya pili khaaa eti hakuvaa tena.. namwambia basi hata tolea nje! Nyiiee inakera, si katoa akati ameshamaliza kila kitu... (machozi yakimwagika tena..akaendelea kuongea kwa uchungu)..
Wiki mbili zimepita leo nakuja kuchek hali ikoje naambiwa ni mjamzito.. nampigia simu ananijibu kwa kejeli na kunijia juu eti. kwanini hukwenda kununua P2 (Kidonge cha kuzuia mimba baada ya tendo) pale famasi, kaongea shombo kibao.. kakataa ujauzito na kanikatia simu... (akifuta kamasi, machozi yakitoka huku kwikwi imemkaba)... inauma sana kaka angu acha tu.."
Hili jambo likafanya kumbukumbu... ije akilini mwangu, ambapo sikumoja nikiperuzi nikakutana na habari kwamba, wastani wa kati ya mimba 100 (Kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Nchi yetu) 34 zote hazikutarajiwa na 11 wahusika hawazihitaji kabisa.. Aiseee! eti 13 hutolewa!.Rejea Hapa.
Takwimu hizi ni wale tu ambao wamepata nafasi kushiriki kutoa takwimu, achana na lile kundi kubwa linaloamua kuzichinja chini kwa chini au kula P2 mapema sana🥹.
Enewei, tusitoke kwenye jambo la msingi...
Hebu ndugu yangu vuta kiti tutete! naongea nawewe msomaji...
Vipi ingekua wewe ungefanya nini katika mazingira hayo?
Au basi, unadhani shida yote iko wapi hapo na tunafanyaje kuitatua changamoto hii?
Nisiwe mtabiri wa jadi katika kujua jibu lako, lakini nakumbuka baada ya kumshirikisha mtu fulani akasema kwamba "ayo ni mambo ya mabachela na masponsa/majimama tu! sie wa kwenye ndoa hilo halituhusu bwana mkubwa.."
Ubishi sio hulka yangu, ila udadisi ni tabia niipendayo, chap kwa haraka nikatumia teknolojia kiganjani kuperuzi, nachokikuta hutaomini, kwamba Afrika yetu hii...wanawake walio katika ndoa inaonesha kuwa wameripoti kuwa na mimba zisizotarajiwa mara 6 zaidi ya wale ambao hawajaolewa😳! Ndio, habari ndio hiyo. Rejea hapa
Kuendelea kufatilia kuhusu shida iko wapi kwa wengine na kwa mitandao ilikua njia niliochagua kama ambavyo nakuuliza wewe leo.. nikujuze tu wenzio walinambia sababu hasa ni kuanza ngono mapema, msukumo wa dini, hali za kiuchumi, kutokufahamu njia za uzazi wa mpango, hali ya ndoa, makazi ya watu n.k, lakini binafsi nilivutiwa na jibu mojawapo ambalo alisema "wanaume tuna njia chache (3) za kupangaza uzazi, ni aidha utumie kondomu ambayo kiukweli inapunguza utamu wa tendo na pia kwa unayempenda sio shwari kutumia kondomu, ila pia kumwaga nje! daaah! hiyo njia ngumu balaa, na mwisho ni kukomesha uzazi kabisa... hivi kweli hata wewe njia hiyo ungeitumia, aah! hilo halipo damu inachemka mkuu"
Kama ilivyo ada utafiti ni mpenzi wa moyo, kujihusisha naye sina budi, Mapema mwaka huu (23 March 2022) wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Minnesota US, walifanya utafiti wa vidonge vya uzazi wa mpango vya wanaume ambavyo uwezo wa kuzalisha (kutungisha mimba) unarejea ndani ya mwezi, zina ufanisi mkubwa na hazina maudhi (side effects) yenye kuhofiwa, si hivyo tu, bali utafiti kwa wanyama umekamilika na mwisho wa mwaka huu (2022) wanataraji kuanza majaribio kwa wanadamu. Rejea hapa
Swali ni Je! jamii ya wanaume iko tayari kutumia? kuwajibika kupanga uzazi?
Baadhi ya sababu kubwa hasa zinazosababisha shida na changamoto hii ni kwamba ufahamu bado ni mdogo kuhusiana na kupanga uzazi, sauti za wanandoa juu ya hili suala iko chini sana na KUBWA zaidi ni kwamba, Wawanaume hawaoni kuwa wa wajibika katika kupanga uzazi pia na kuwa na utayari wa kuchukua hatua katika kupanga uzazi.
USISAHAU: Njia hasa ya upatikanaji wa mimba ulimwenguni, inahusisha wote mwanaume na mwanamke! Mwanaume! AMKA!, kupanga uzazi, ni wajibu wa pande zote.
Kwanini mkazo uwepo,
Ulimwenguni, 44% ya mimba zote zilikuwa zisizotarajiwa. 56% ya mimba hizo zilitolewa (Abortions). Takribani 4.7% – 13.2% ya vifo vya mama wajawazito vimetokana na utoaji mimba usio salama. Huku mwaka 2012 pekee, takribani wanawake Millioni 7 walitibiwa magonjwa yatokanayo na shida zifuatazo baada ya utoaji wa mimba. Rejea hapa
Kuanza maisha katika hali ya kutokutarajiwa (Watoto wanaozaliwa katika hali hiyo) yaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kufikia malengo ya taifa ya kielimu na kiuchumi.
MAPENDEKEZO:
Kabla ya utafiti huo kukamilika, tufanye haya, pindi utakapokua tayari, ushindi wa kishindo uweze kuwa wa hakika.
- Wewe unayesoma chukua hatua
- Vyombo vya habari nchini na vitangaze habari hii
- Shuleni/vyuoni jambo hili lifundishwe na kuelekezwa
- Vituo vya afya ushauri utolewe
- Mabango yatumike kufikisha ujumbe huu
- Kampeni na hadhara na mitandaoni zitumike kufikisha habari.
Wajibika! Jinsi zote zi wajibike! Ushindi ni hakika.
#KupangaUzaziNiWajibuWaJinsiZote
Muda ni sasa!
Kalamu chini, mwaga wino wako hapo chini..
Upvote
0