JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Orodha ya wapiga kura kwa kila kituo itabandikwa siku nane (8) kabla ya Siku ya Uchaguzi ili wapiga kura walioandikishwa wapate fursa ya kutambua vituo watakavyopigia kura.
Vilevile, Tume imeandaa utaratibu utakaomuwezesha mpiga kura kukagua taarifa zake zilizomo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kutambua kituo atakachopigia kura. Mpiga kura anaweza kujua kituo chake cha kupigia kura kwa kufuata utaratibu ufuatao:-
1. Kuhakiki kwa kutumia mfumo wa Voters’ Interaction System (VIS) ambapo mpiga kura atafanya yafuatayo:-
(i) Atabofya namba *152*00#.
(ii) Atachagua namba 9 (Uchaguzi Mkuu).
(iii) Atachagua namba 1 (Uhakiki wa taarifa za mpiga kura).
(iv) Ataingiza namba ya kadi ya mpiga kura bila kuweka herufi “T” wala alama “- “.
(v) Ataona ujumbe unaosomeka “ombi lako limepokelewa na linashughulikiwa, utajulishwa kwa ujumbe mfupi (SMS) hivi punde”.
(vi) Atapokea ujumbe mfupi utakaonesha taarifa zake na kituo cha kupigia kura.
2. Kuhakiki kwa kupitia kituo cha huduma kwa wapiga kura (Call Centre) ambapo wapiga kura watapaswa kupiga simu Na. 0800112100 na kupata usaidizi wa kuhakiki taarifa zao.
3. Kuhakiki kwa kutumia tovuti ya Tume ambayo ni www.nec.go.tz ambapo mpiga kura atafanya yafuatayo:-
(i) Ataona sehemu iliyoandikwa”Uhakiki”.
(ii) Atabofya sehemu iliyoandikwa “mfumo wa uhakiki taarifa za mpiga kura”.
(iii) Itatokea sehemu iliyoandikwa ingiza namba ya mpiga kura na ataingiza namba yake kama ilivyoandikwa kwenye kadi ya mpiga kura. Kwa mfano T-1400-0073-149-0.
(iv) Akikamilisha atabofya sehemu iliyoandikwa “tafuta” na taarifa zake zitaonekana.
Upvote
6