JInsi Mshahara wa Mkenya utakavyopigwa panga kuanzia Julai 1, 2023

JInsi Mshahara wa Mkenya utakavyopigwa panga kuanzia Julai 1, 2023

Lukumba

Member
Joined
May 24, 2023
Posts
35
Reaction score
91
JIRANI ZETU WATAENDELEA KUKIONA CHA MTEMA KUNI , HAPO BADO ISSUE YA DOLA KUPOTEA HAIJAINGIA..

Huku Wakenya wakiendelea kukumbwa na hali ngumu ya maisha kutokana na ongezeko la gharama ya juu ya maisha, hakuna matumaini ya afueni kupatikana hivi karibuni. Hatua hii inajiri baada ya serikali kutangaza kuongeza ada ya Hazina ya kitaifa ya Bima ya afya (NHIF) na Ile ya Hazina ya kitaifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Viwango vya sasa, ambapo wafanyakazi wanaolipwa hulipa kati ya Sh 150 na Sh 1,700 kulingana na malipo yao ya kila mwezi, vinaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kiwango kisichobadilika cha asilimia 2.7 ya mshahara wao. Ingawa wafanyakazi wote wataona mshahara wao ukipunguzwa na mabadiliko haya, watu wanaolipwa kiwango cha juu cha mshahara watalazimika kulipa asilimia 35 ya ziada ya kodi ya PAYE (Pay As You Earn) kwenye mapato ya zaidi ya Sh 500,000.

Hii itawafanya wale wanaopata Sh 600,000 kwa mwezi walipe Sh 22,904 kutoka katika mshahara wao, huku serikali ikitafuta nyongeza ya Sh 350 bilioni za kodi katika mwaka ujao wa kifedha. Katika Bajeti ijayo ya Fedha inayoanza Julai, mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya KRA inalenga kukusanya Sh 2.89 trilioni, ikiwa ni ongezeko kutoka kiwango cha sasa cha Sh 2.53 trilioni.

Serikali inatarajia makusanyo ya kodi ya mapato ambayo ni pamoja na PAYE na kodi ya mapato ya biashara inayolipwa na wafanyabiashara kuongezeka kwa Sh 194.2 bilioni hadi Sh 1.2 trilioni katika mwaka wa fedha unaoishia Juni mwaka ujao yaani 2024. Mabadiliko ya hivi punde katika Muswada wa Fedha, 2023, yakiidhinishwa na wabunge, huenda yakaongeza shinikizo la mfumuko wa bei unaohisiwa na Wakenya kwani gharama ya juu ya maisha inapunguza uwezo wao wa kununua.

Serikali ya Kenya Kwanza inasema kwamba ongezeko la akiba kupitia NSSF litasaidia sio tu kuwapa wafanyakazi faida katika maisha yao ya uzeeni bali pia kuiwezesha serikali kupata fedha za ndani iwapo inataka kukopa.

Jirani zetu wanaendelea kukiona cha mtema kuni.
 
Wakenya wapo both, smart and aggresive mbaya zaidi pia wapo hopeless.

Ni watu ambao wapo tayari kuichoma moto mchi yao ili wakose wote. Hawaoni shida kurudi enzi za Maumau ili tu Odinga apate atakacho.
 
Back
Top Bottom