Afterthought 2:
Biashara na uchawi.
Kule nilivyoingia uziguani, wale wazee wa ofisini wakanitahadharisha siku ya kwanza tu - kijana kuwa makini sana, umejiandaa lakini?
Sikuelewa maana yake, ama either nilijifanya sijaelewa ili walieleza kiundani. Mzee m1 akaniita pembeni akanieleza. Akanitisha sana suala la uchawi, ushirikina, husda za watu, akaniambia inabidi nijilinde. Mimi nikamweleza wazi yule mzee kuwa siamini juu ya uwepo wa hivyo vitu, akasema kama mimi siamini basi nimpe yeye elfu 30 ataenda kujua jinsi gani atanilinda, bila mimi kuwa involved. Mimi kiukweli nilimgomeshea tukaachana, akasema nisubiri nijionee.
Nilivyoanza kazi nilifata protocols zote za utunzaji wa chombo, kila tukimaliza kazi tunapiga grease ya kutosha, nikanunua oil litre 40, kila baada ya heka 40 napiga chini oil, filter ya oil na diesel nabadilisha kila wiki. Yani sikutaka utani, mtu angeweza kusema vile ni vyombo vyangu japo nilivikodi.
Pale tulifanya kazi bila itilafu za nje ya technical issues, kuna kitu kilizingua nikamwita fundi kutoka Moro, hatukufanya kazi kwa siku 3, lakini lilikuwa tatizo la kiufundi.
Mchawi wa mafanikio ni umakini, kujituma na kuipenda kazi yako. Hakuna ndumba, unachoma tu pesa zako.