SoC02 Jinsi nilivyopata Kisukari kutokana na kutokuwa na utayari wa kusomea utabibu na Uzembe wa matabibu na manesi katika Afya

SoC02 Jinsi nilivyopata Kisukari kutokana na kutokuwa na utayari wa kusomea utabibu na Uzembe wa matabibu na manesi katika Afya

Stories of Change - 2022 Competition

Faith Athanas

New Member
Joined
Sep 8, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Habari,

Afya ni sekta nyeti sana ambayo sekta hiii ikiyumba ,sekta zingine zote zimeyumba.Tujiulize tuna matabibu wanaotegemea nadharia au tunamatabibu wanafanya kazi kwa moyo.?

Mwaka 2003 mama Yangu mzazi alienda katika hospitali moja, njiani iringa ,ilikuwa hospitali nzuri tu ,alienda kujifungua mimi, alipofika alipokelewa alipata shida sana kujifungua kwasababu nilikuwa na uzito Mkubwa, alijikaza na kujifungua.

Nilizaliwa vizuri tu, shida ilianzia pale kulipokuwa na viashiria vya ajabu katika mwili wangu, mwili ulikuwa na mafuta hata kwa nje lakini pia nilikuwa na uzito uliopitiliza wa kilo 4.6, ambapo manesi waliishia kumpa mama yangu hongera kwa kunilisha vizuri kwa kigezo like walichoamini kuwa ni Afya hawakupima chochote zaidi ya kunipa chanjo. Mama yangu akakamilisha siku za kukaa hospitali, akaondoka

Nilivyofikisha miaka mitatu niliumwa malaria tu nikadondoka na kuzima, kwasababu wao sio matabibu hawakuelewa, walinipeleka tu hospitali, nikapatiwa dawa za malaria wakamwambia mama yangu malaria imepanda tu kichwani

Nilipofikisha miaka kumi hali ilizidi kuwa mbaya uzito ulipungua, nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa na kilo 28, ni kitu ambacho sio kizuri sana kuangalia na kilo nilizaliwa nazo, mama na baba wakanipeleka kwa tabibu wa familia katika hospitali aliyokiwa akifanya kazi, aliwaambia "mbona mmemchelewesha mtoto"hakukata tamaa na mimi kwasababu alikuwa ni mtu wa karibu na familia akanibeba na kunipeleka hospitali nyingine kubwa zaidi.

Nilipofika walinipima magonjwa yote na kunipeleka chumba cha wagonjwa mahututi(ICU), nilikaa kule, manesi wakasema huyu kupona sidhani walikata tamaa kutokana na hali yangu. Akatokea Daktari mmoja aliyetoka katika mafunzo ya utabibu akanitibu kwa kadri ya uwezo wake mpaka nikaanza kuwa Sawa, nilipatiwa dawa na baada ya siku tatu nikatolewa katika chumba hicho nikapelekwa kwenye wodi zingine,Nilifunzwa kujichoma sindano, nikafanya kwasababu nilitaka kwenda nyumbani, kweli nikirudi nyumbani nikamuuliza Baba, nitakuwa sawa baada ya hizi sindano 60 za mwezi? Baba aliniangalia kwa uchungu na masikitiko kama vile amefiwa ,nikielewa nikajua kwamba haya ndio yatakuwa maisha yangu mpaka kufa, nilihuzunika sana

Nilipoenda shule wanafunzi wenzangu waliniita teja kila wakiniona nachoma zile sindano, nilinyimwa nafasi ya kuwa dada mkuu kwasababu walihofia Afya yangu kuzorota, nilitengwa kwasababu nilikuwa ni kitu kipya sana kwangu na hata pia kwao ,lakini kwa akili zangu za udogo nilidhani wananitenga nikawa nalia katika kila kitu.

Nilijiunga na wenzangu wenye tatizo hilo hilo na wengine walishakata tamaa pale hospitali, nikawa nalia tu makosa Natumaini,kuna siku nilikaa nikasema sidhani kama kulia ni suluhisho,nikaanza kusoma kwa bidiii nikiumwa narudi nyuma ,nikipona nasonga mbele ,nilifaulu vizuri msingi na sekondari ,na sasa Niko chuo nasomea utabibu, sisomi Ili niwaumize wengine kwa nilivyotendewa ,lakini nasoma Ili niokoe maisha ya watu wengine wenye matatizo kama ya kwangu au zaidi.

Swali ni kwamba ,tunadhani wale manesi wangekuwa na moyo na kazi waliokuwa wanaifanya ningeumwa hivi leo takribani miaka kumi sasa?

Je, kungekuwa na somo la utu na ubinadamu ,kujali watu wengine je tunadhani yaliyonikuta yangenikuta?

Je, unadhani wangekuwa makini na kazi zao wangeshangilia mm kuwa na mafuta vile mwilini na uzito uliopitiliza?

Na je, kwangu mimi ilikuwa hivyo na sijakata tamaa ,watoto wangapi wenye Kisukari kama cha kwangu(type 1) wamekata tamaa wameshindwa kuendelea?

Je, wangapi wenye magonjwa mengine kama ukimwi walizaliwa nao kutokana na Uzembe wa kumpa mama mjamzito elimu ya kujifungua? Wangechukua hatua ni dhahiri kuwa ningekuwa na Afya njema au ingeshindikana hata ningelijua hili tatizo zamani nisingelia kwa uchungu vile endapo ningeitambua hali yangu mapema pamoja na wazazi wangu.

Haya yanatokana na kutokuwa na moyo wa kufanya kazi flani na kusomea kazi hio kwasababu ya kupata pesa,je ni watu wangapi tunapoteza kama taifa au dunia kwasababu ya kutokuwa na moyo(dedication) katika kazi, Uzembe na kukosa ubinadamu?

Na je magonjwa mengine kama kansa,pumu,shinikizo la damu ,ukimwi kutokana na kuwekewa dam isiyopimwa vizuri na mengineyo mengi tunasemea nimi juu ya hili?ni dhahiri kuwa tunapoteza watu wengi sana sio mmoja.

HITIMISHO.
Serikali pamoja na Jamii kwa ujumla tuangalie kwa jicho la tatu Katika kozi hizi za Afya tusifundishe tu nadharia(theoretically), na kuamini kuwa mtu ameelewa, tusome kwa vitendo lakini tusiishie hapo tufundishe na tuongeze somo la utu na ubinadamu na kujituma bila kushurutuswa, kuwa na moyo wa kazi pia, Ili tunaposoma tuelewe kuwa watu wanapoteza maisha ambapo walitamani kuishi kama wengine ila Uzembe na kukosa utayari unasababisha maisha yao kukatikizwa ghafla.

Mwisho.
Ahsante.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom