Jinsi nilivyopigia simu mwanamke mmoja niliyekuwa namdai fedha zangu

sky walker

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
1,160
Reaction score
831
Nilimpigia simu mwanamke mmoja niliyekuwa namdai fedha zangu, lakini hakupokea simu yangu.

Nilipiga mara 10 zaidi, akagoma kupokea. Nikitambua mumewe alikuwa safari, nikaamua kumtumia meseji hii:

"Halo dada, ninakupigia siyo kukukumbusha deni langu. Nilitaka tu kukwambia kwamba wasichana wawili walikuwa wakipigana kumgonbea mumeo leo hapa mjini. Ulikuwa ugomvi mkubwa na yeye alikuwa akitazama tu, mpaka mmojawao alipofanikiwa kuchopoka kutoka gari la mumeo na wale wawili yaanimumeo na msichana mwingine wakaondoka."

Baada ya dakika chache akanipigia lakini sikupokea. Aliendelea kupiga karibu mara 21 kisha akatuma meseji hii:

"Ugomvi umetokea wapi?
Wameelekea wapi?
Umewatambua hao wasichana? Tafadhali niambie, nimechanganyikiwa."

Nilisoma ujumbe wake nikaupuuza. Akapiga tena, karibu mara tano na sikupokea, kisha akatuma meseji nyingine:

"Ninazo pesa zako, tafadhali tunaweza kukutana, ili unieleze zaidi?"

Mimi nikamjibu, "Sawa, unaweza kunitumia pesa kwa simu ili nipite kituo cha mafuta niongeze wese, halafu nitakupitia na kukupeleka nyumbani kwa msichana kwa sababu namjua aliko."

Dakika mbili baada, nikapokea ujumbe wa salio langu kwamba amenilipa pesa zangu zote.

Nimeizima simu na sasa nimejilaza kitandani nipate usingizi... Sipendi ujinga. mwaka huu wa jpm lazima ujiongeze Ututapelew kirahisirahis ivyo wadada

 
January hipi?

Jf vilaza wengi.

Nimeku quote maksudi usije bisha kilaza wa vilaza wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…