Jinsi nilivyothibitisha Uchawi, hutoamini nakwambia!

Hilo la uwepo wa Uchawi NALIKATAA KATAKATA. Halipo ila lipo kwenye vichwa vya wajinga.
Labda nikusaidie kwa ushauri tu wa namna nzuri ya kuthibitisha haya mambo

Nenda mikoa inayoaminika kuwa na waganga/wachawi) wa kutisha ( nenda kijiji kimojawapo ni lazima utakutana na mzee au wazee maarufu wa hayo maswala hapo kijijini ukakutane nao )

Then wape ombi lako, Ninaamini utatuletea mrejesho mzuri hapa
 
Umesema ukitaka kumficha muafrica muwekee maarifa kwenye vitabu, Inawezekana upo sahihi kabisa

Kwani hata vitabu vya mambo ya kishetani vipo, vitabu ambavyo vimejaa maneno ya kichawi "sigil" jinsi ya kufanya rituals, Jinsi ya kuita majini

Na mambo mengine meengi mengi....Je wewe umewahi kusoma hivyo vitabu ?
 
Walozi lazima mpingane na maandiko......vitabu vitakatifu vya dini vinakiri uwepo wa uchawi
 
Hakuna kitu kama hiko broo.. Siku hizi kuna simu mawasiliano nje nje. Sio lazima usafiri hadi mbali huko. Nipe mwongozo nijithibitishie hilo. Vinginevyo hiyo uwepo wao ni Myth i.e. hakuna uchawi.
 
Hakuna kitu kama hiko broo.. Siku hizi kuna simu mawasiliano nje nje. Sio lazima usafiri hadi mbali huko. Nipe mwongozo nijithibitishie hilo. Vinginevyo hiyo uwepo wao ni Myth i.e. hakuna uchawi.
Muongozo wa kwanza ni lazima ufike hizo sehemu nlizozitaja

Kama una nia ya kuthibitisha haya mambo utafika, Ila kama lengo lako ni kubishana tu kwenye mitandao bila sababu za msingi hautoweza kwenda huko
 
Walozi lazima mpingane na maandiko......vitabu vitakatifu vya dini vinakiri uwepo wa uchawi
Mkuu; mbona vitabu vya dini vimeandikwa na watu (binadamu) tena sio muda mrefu i.e. sio zamani na viliandikwa kwa kukusanya maandiko kutoka vyanzo mbalimbali vya zamani kutoka maeneo na mataifa tofauti kisha wakachambua humo ni kipi kiandikwe na kipi kiachwe na mbaya zaidi maandiko hayo yalitafsiriwa e.g. Bible kutoka lugha original na ukizingatia muda uliopita hadi imetufikia huku Umasaini- ujue wajanja wameichakachua mpaka baas. Usiyashupalie sana maandiko. Akili za kupewa changanya na za kwako.
 
Nimewahi kuona kuku anatamkiwa maneno mpaka anakufa bila kuguswa na au kuchinjwa
 
Nimewahi kuona kuku anatamkiwa maneno mpaka anakufa bila kuguswa na au kuchinjwa
Hatare.
Kuna wale jogoo anarushiwa punje za mchele.

Anakula then anachinjwa zinahesabiwa kafara zipo za aina nyingi Sana..

Ila watu ni wabishi Sana hasa hasa wabongo walio MAJUU.
 
Muongozo wa kwanza ni lazima ufike hizo sehemu nlizozitaja

Kama una nia ya kuthibitisha haya mambo utafika, Ila kama lengo lako ni kubishana tu kwenye mitandao bila sababu za msingi hautoweza kwenda huko
Umemsoma Nyani ngabu hapo juu? Sasa unataka ni mpaka waende huko wangapi? Huyo mmoja si anatosha na zaidi ya hapo ametoa kibali/idhini kwa yeyote anayejidai ni mchawi amroge; tena ametoa na Ofa ya Usafiri. Labda mm nakuahidi soda /maji ya njiani. Unatakaje zaidi mkuu??
 
Mimi nmekujibu wewe,
Jibu wewe kama wewe ambaye unapinga uwepo wa maswala ya uchawi, Simama wewe kama wewe

Yeye pia atasimama yeye kama yeye.
 
Hata Kama maandiko yameandikwa na watu Kama sisi Basi hao watu walikua na upeo mkubwa Sanaa wa uwezo wa kufikiri na akili kubwa Sanaa 😊
 
Lakini pia umuulize huko alikoenda kutafuta wachawi alitoa kibali cha wao kumroga ? akijibu alifanya hivyo atupe na uthibitisho
 
Nimewahi kuona kuku anatamkiwa maneno mpaka anakufa bila kuguswa na au kuchinjwa
Inafikirisha. Je, huyo kuku aliwekwa mahali gani ili kuondoa mashaka ya visababishi vingine vya kifo zaidi ya Uchawi???(ceteris paribus). Kuku mgonjwa? kuku amelishwa sumu in advance, kuku amenyimwa hewa n.k.
Hata hivyo kuku anaweza kufa kwa mshituko mkubwa na wa ghafla kama inavyokuwa kwa binadamu.
 
Lakini pia umuulize huko alikoenda kutafuta wachawi alitoa kibali cha wao kumroga ? akijibu alifanya hivyo atupe na uthibitisho
AaaH! Mbona amesema waziwazi Hakuwaona? i.e Hawakuwapo; Hawapo na hawatakuwepo -tunajilisha matango pori tuu hapa.
 
Hata Kama maandiko yameandikwa na watu Kama sisi Basi hao watu walikua na upeo mkubwa Sanaa wa uwezo wa kufikiri na akili kubwa Sanaa 😊
Ndiyo, ni kweli kabisa. Hata sio wao tu walikuwa na upeo mkubwa sana na uwezo wa kufikiri bali hata leo 2025 watu hao wenye akili kubwa na uwezo wa kufikiri wapo e.g. Wanasayansi mashuhuri, watu Wanaovitumia vitabu hivyo vitakatifu kupiga hela n.k..
 
Hapo kwenye KUPIGA HELLA 😊
 
AaaH! Mbona amesema waziwazi Hakuwaona? i.e Hawakuwapo; Hawapo na hawatakuwepo -tunajilisha matango pori tuu hapa.
Ina maana nyinyi mnaopinga ndio mpo sahihi sana ? Kwanini yeye umemuamini haraka haraka kuwa hakuona

Ila mtu mwingine akileta kisa chake namna alivyoshuhudia jambo la ajabu unampinga

Why ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…