Jinsi nilivyothibitisha Uchawi, hutoamini nakwambia!

Sikio ulilosikia kwalo ni sikio la mtu wa ndani Si la nje.

Macho pia uliyoonea ni macho ya ndani Si ya nje.
 
Mkuu unachosemani kweli asilimia 100 uchawi upo mi mwenyewe nina ushahidi wa kumuona mchawi ndani ya chumba changu usiku na taa ilikua inawaka ushahidi mwingine nimewahi kumshika mkono mchawi akiwa kitandani kwangu na kuna siku miaka ya 90 nilijifunika shuka gubigubi nilishtuka usingizini nikafumbua macho ghafla shuka ikafunuliwa usawa wa uso wangu nikakutana na macho yananianglia na ilikua giza ila yale macho yalikuwa yana ng'aa usiku huo sikugeuka kwa hofu mpaka kumekucha..ila yule mama niliyemuona ndani akiwa uchi nilim hamfahamu na mwanae alikua rafiki yangu..
 
Ni wapi na how umepambana naye? Wakati unasema alikuwa anarudi nyuma nawe ukarudi ndani? Ni wapi ume fail kudanganya?
 
Mimi ya kushikwa mkono niliwahi Ile nashtuka hivi akapotea aise siku za mbeleni niliumwa
 
Uchawi upoo!!!!


Mimi Kuna siku ilikuwa mida kama ya saa SITA usikuuu HIVI, ghafla nikashtuka nasikia sauti ya paka mfululizo "nyau nyau nyau".....

Nikaingiwa hofu paka Gani HUYO asiyetulia ila nikaona isiwe KESI nikavuta blanket mpaka KICHWANI mara paaap Kuna kitu kizitooh kikakaa kifuani kwangu "PUUUH" daaah aisee mtu kakukaliaaa unahangaika Ile mbaya afu hatoki.

Nikajaribu kupiga kelele lakini sauti haitoki daah dadekii nikasema hapa Leo nimeyakanyaga nikatamka maneno matakatifu, sauti ikawa haitoki nikajitahidi sauti ikatoka,

Mchawi yule aliposikiaa tu Yale maneno ule uzito kifuani ulitoka na ni kama alijigonga kwenye kitanda maana kilipata mtikisiko wa maana na sauti ilitoka kama ya mtu aliyejigonga ikasikika sauti Tena kwenye paa la nyumba kama mtu amekanyaga hivi na Ile sauti ya paka kulia lia ikawa imetoweka

basi mpaka hapo nikawa nimeamini kuwa uchawi upoo na tunaishi nao miongoni mwetu
 
ni kweli uchawi upo,na ndo manake BIBLIA au MUNGU anasema"usimwache mwanamke mchawi kuishi" na ata QURAN tukufu inasema "acheni USHIRIKINA!!!,,,,,,,,,,okay ata mimi nilishawai kukutana na jirani yangu mwanamke shambani saa nane usiku!!! akiwanga,juu kavaa kaniki nyeusi,chini kavaa kaniki nyekundu,huku akirukaruka!!
 
Mhhh! Mkuu, wewe ulienda shambani muda huo kulikoni???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…