Jinsi Ninavyopata wateja wa kazi za freelancing

Jinsi Ninavyopata wateja wa kazi za freelancing

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,319
Reaction score
3,097
Jinsi Ninavyopata wateja wa kazi za freelancing.

Hizi njia ukiweza kuzitumia zitakupa matokeo ndaninya miezi mitatu.

Pia unaweza kuzitumia kwenye biashara yoyote
-5xclyh.jpg

Kwanza kabisa wateja wa uhakika wapo LinkedIn,

LinkedIn mteja anakufata mwenyewe inbox kama ni interview anakupangia tarehe mnafanya interview.

Ila tu lazima uwe unashare kazi zako zinaonekana.

Njia ya pili ni youtube video

Watu wengi huwa wanahisi wakiweka video zao youtube watakuwa wanafundisha bure.

Kuna client anataka akuone unafanya kitu live ndo akupatie kazi.

Kila kazi yako unayoifanya ipost youtube. Watu wa kukulipa wapo bize hawana muda w kujifunza.
Njia ya tatu kutafuta wateja ni

Kutumia freelancing job marketplace.

Hizi ni sehemu ambazo tayari watu wanajua ukienda unapata mfanyanyakazi.

Weka kazi zako kwa bei kibwa, subiri wateja watakuja.

Njia ya nne ni blogging.

Blogging kuandika article na kuzipost medium na linkedin.

Wazungu wanapenda sana kusoma hasa Articles. akikutana na kitu kizuri lazima atakutafuta umfanyie kazi.

Kwenye kila article yako weka call to action.
20250314_000430.jpg

Blogging inafanya na watu wa affiliate marketing, unaweza kutumia njia hizohizo kwenye Freelancing.

Njia ya tano ni kufanya outreach

Hapa huwa natuma meseji kwa mtu mmoja mmoja dm.

Hii inahitaji utumie Automation tools maana inachosha sana, ukiwa na offer nzuri utapata wateja.

Njia ya sita ni paid ads,

Kuna jamaa zangu wanafanya kazi kama za matangazo, academic writing, huwa wanarusha matangazo kwenye nchi zenye Clients wanaolipa vizuri.

Lakini wanapata consistent clients wanaolipa vizuri.


Njia ya mwisho ni content.

Content ndo njia rahisi ya kupata wateja.

Njia ambayo haina gharama na inaleta matokeo ya muda mrefu.

Content hapa namaanisha short form contents, za tiktok, reels na shorts

Jambo la. Msingi ni lazima uweze kufanya hivi

Tengeneza offer
Fanya marketing
Close clients
Toa quality nzuri ya kazi
Screenshot_20250313_165535_WhatsApp.jpg

Kama una swali lolote kuhusu freelancing
Niulize hapa wa.me/+255693880325
 
Back
Top Bottom