N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Unaposoma Bayographia ya Mwalimu iliyotayarishwa na wanazuoni watatu ukurasa wa 125 hadi 126 kuna simulizi fupi ifuatayo
Mwanzoni mwa miaka ya 80 kulikuwa na tatizo la baadhi ya wamiliki wa maduka kuhodhi bidhaa kisha kuja kuziuza baadae kwa bei juu baada ya kuadimika.
Kwa kuliona hili Baraza la Mawaziri wakati huo chini ya uongozi wa Baba wa Taifa wakaazimia watafutie ufumbuzi suala hili.
Basi Waziri wa Kilimo wakati huo hayati Joseph Mungai (ambae hata sie vizazi vya baadae tulimkuta huyu bwana kwenye utawala wa bwana Ben) akatoa wazo kwa wenzake chini ya Mw/kiti baba wa Taifa kwaamba "tutaifishe maduka yote nchini" ili kukomesha hii tabia ya kuhodhi bidhaa madukani.
Tafsiri yake kwamba, maduka yote sasa yangemilikiwa na serikali ili tatizo la kukosekana kwa baadhi ya bidhaa liishe.
Mwalimu Nyerere hakulikubali kwa haraka wazo hili, ingawa wenzake kwenye kabineti almost wote walikuwa wameunga mkono hoja ya Mungai.
Na kwa kuwa Ministers walikuwa wameshakubalii, basi ikasalia uamuzi wa mwisho wa Mwenyekiti Rais J.K.N ambae bado hakukubaliana na wazo hilo kiurahisi.
Itaendelea...