mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Ni hivi, haitajwi aliondokaje nchini, lakini alikimbilia Uingereza kupitia uwanja wa ndege nchini Kenya na serikali ya Tanzania ikatangaza baadaye sana.
Kuthibitisha hilo, Jumanne ya Januari 23, 1968, siku ya kwanza ya ufunguzi wa kikao cha Bunge la Muungano wa Tanzania kwa mwaka huo kilielezwa na Makamu wa Pili wa Rais, Rashid Mfaume Kawawa hivi: "Kambona ameikimbia nchi mwishoni mwa mwaka jana (1967) na kwamba kabla hajaondoka, shilingi 500,000/- ziliingizwa kwenye akaunti yake mjini Dar es Salaam kutoka benki moja ya Uingereza," (Hansard haielezi hiyo ilikuwa ni benki gani).
"Pesa hizo ziliingizwa katika akaunti hiyo Desemba 6, 1966. Hiyo ilikuwa ni miezi miwili kabla ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha." Kawawa aliyasema hayo alipokuwa akijibu swali kutoka kwa Mbunge wa Rombo, Bw. Maskini.
Aliongeza kuwa miezi mitano baada ya Azimio la Arusha, Julai 1967 kiasi kikubwa cha pesa kilikuwa kikiingia katika akaunti ya Kambona ambaye pia alikuwa anamiliki majumba katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Songea ambazo kwa pamoja zilikuwa na thamani ya shilingi 485,612/-
Rashidi Kawawa alisema kulingana na uchunguzi uliofanywa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) baada ya Kambona kuikimbia nchi, uligundua kwamba kati ya Juni 1965 na Desemba 1966, Kambona aliingiza katika akaunti yake mjini Dar es Salaam kiasi cha shilingi 896,800/=.(Haikuelelezwa akaunti hiyo ni ya benki gani.)enzi hizo zilikuwa pesa nyingi sana
"Kambona alikuwa akimiliki majumba mengi katika maeneo kadhaa ya nchi kabla hajatorokea Nairobi, Kenya, kisha London, Uingereza," Kawawa aliliambia bunge.lakini baadhi ya watanzania waliokuwa wakiishi nchini uingereza walisahangaa kumuona kambona akiishi uswahilini na akiwapiga mzinga na kufanya vibarua vya watu wa hali ya chini na kuhoji tuhuma za ufsadi
Kambona nae hakubaki kimya akadai Nyerere ana akaunti ya fedha za kigeni nje ya nchi japo hakuwahi kuthibitisha
Ikumbukwe enzi zile kuna kampuni kubwa ya magari toka india ikijulikana kwa jina la TATA ,kwa mikoa mingi ya kanda ya ziwa na baadhi ya makabila yenye asili ya Bantu neno TATA lina maana ya Baba ,basi akazusha kuwa hiyo ni kampuni ya Nyerere kwa sababu ni anajiita baba wa Taifa.
Hata jarida la Newsweek liliwahi kudai nyerere ana akauti ya nje ila mwandishi mwingine wa kimataifa alitoa dau sikumbuki kiasi ila zilikuwa nyingi enzi hizo kuwa kama kuna mwenye ushahidi autoe na angempatia kiasi hicho au shut up ahahah,mpaka leo hakuna aliyetoa ushahidi,mpaka wote wanakufa Kambona na nyerere walikufa wakiwa na maisha ya kawaida tu