Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 487
- 1,287
Siku za hivi karibuni tumeona makatibu wa chama kwenye kata wakipewa pikipiki maeneo mbalimbali Tanzania
Hata hivyo mgao huo umejenga chuki na makundi kwa wanaccm wenyewe kwa wenyewe
Madai ya chuki
Wengi wanadai kuwa kitendo cha kuwapa baadhi yao pikipiki ni cha ubaguzi kwani na wao ni wanaccm tangu zamani na hawajawahi kupata chochote
"Kuna wanaccm wanaotambulika wengine hatutambuliki,kumpa mtu pikipiki bure yenye thamani ya milioni tatu na leseni juu huku wengine hatuna kitu ni ubaguzi na inaonesha hatutambuliki na sasa wakisema tunawahitaji wanaccm kwa jambo fulani waende waliopewa pikipiki na si vinginevyo: Alimaliza kuongea mwananchi huyo maeneo ya Rorya
Naye mwenyekiti wa ccm kata fulani hapa Rorya alisema" ccm imerudia makosa yale iliyokuwa inayafanya zamani kupitia mavazi na kanga kugawia watu fulani
kwenye chama na kuwaacha wengine ilileta ubaguzi na makundi ambapo wakaona sasa ina athari wakaamua kuuza badala ya kutoa bure na sasa wamerudi kule kule ngoja tuone"
mkazi wa Kijiji cha Sokolaboro Rorya yeye anashauri badala ya ccm kugawa pikipiki ingezileta kisha kutangaza kuziuza kwa wanaccm kwa bei nafuu isingeleta maneno mengi na nzuri zaidi ccm ingeleta vitanda kwenye zahanati zetu kwa kila kata ambapo mwanaccm angeenda angelala,CHADEMA angelala na asiye na chama angelala kuliko kuwapa watu fulani mapikipiki"