Aikasia James
Member
- Jun 21, 2024
- 5
- 1
Kwa nchi kama India, Korea, na Marekani, sanaa imekuwa ni moja wapo ya kazi inayoongeza uchumi kwa taifa. Kwa mfano, Korea wako vizuri kwa kuonyesha utamaduni wao na hata kuonyesha historia mbalimbali ya nchi yao. Lakini sisi pia tunayo historia mbalimbali kuhusu nchi yetu, mfano jinsi tulivyopata uhuru wetu, utumwa tuliokuwa tunaupitia kutoka kwa watu weupe, vita ya Kagera, na maisha ya raisi wetu wa kwanza.
Ni moja pia ya njia ya kuenzi historia yetu maana kielimu, wanafunzi wanapata kujifunza na kiuchumi tunakuwa. Tuna watu waliosomea sanaa ambao, tukiwatumia vizuri, tunaweza kukuza sanaa yetu. Achilia mbali hivyo, tazama umoja wa Wahindi na Wachina; kwa umoja wao, wanatengeneza sinema nzuri. Ni sisi tu kutambua vipaji vya watu wetu. Ingawa teknolojia yetu haijakuwa, lakini kwa teknolojia tuliyonayo, tuna uwezo wa kutengeneza sinema nzuri.
Yamkini sina utaalamu kwenye maswala hayo, lakini tukitaka kukua, tujaribu kuakisi uhalisia tuliotoka nao kutoka kwa mababu zetu. Msiseme kuwa tunazo sinema kama hizo, hapana, si kweli, na wala hazivutii na hazipo katika ustadi mkubwa. Kama ni sinema za kihistoria, kama kuigiza kwenye majumba ya historia, ruhusa itolewe na kama wanahitajika mfano wa wakoloni, watumike watu wenye rangi ya wale wakoloni ili kuleta uhalisia wa historia yetu.
Si kuigiza kama vile tunasoma kwenye kitabu bali kitu kinachovuta hisia za watu na hata kuleta burudani kwa watu. Vijana waweze kuigiza kwa uhalisia; ongea, muonekano, na onesho analofanya liwe sawa na hisia anazofanya, wasiiigize ilimradi tu wanajua watu wataangalia hata iweje. Kwa imani, hata hiyo pia inaweza kusaidia.