Jabeir_simba
New Member
- Aug 29, 2022
- 1
- 0
Sensa ya watu na makazi ni zoezi la kutambua takwimu za watu wote na makazi Tanzania ambapo hufanywa kila baada ya miaka kumi mara ya mwisho imefanywa kuanzia tarehe 23 mwezi wa nane mpaka tarehe 1 mwezi wa tisa 2022.
Ambapo zoezi lilifanyika kwa ufanisi likiacha athari chanya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Tanzania zoezi zima la sensa lilianza kwa kutangaza nafasi kwa vijana watakao wiwa kujitolea muda wao kwa hali na mali kufanikisha zoezi zima la sensa ambapo mfumo wa kieletroniki ulitumika kutuma maombi na mchujo ukafanyika kuwapata wenye weredi wa kazi ambao watakaopitia mafunzo na mitihani baadae kufuzu kuwa moja ya rasilimali watu kwenye kazi nzma ya sensa.
Sensa imeweza kugusa maisha ya watu moja kwa moja na kuleta athari chanya kwa mtu mmoja mmoja, kaya na jamii kwa ujumla ningependa kuelezea jinsi gani zoezi la sensa lilivyobadilisha maisha ya rafiki yangu wa karibu sana aitwaye UTUBURE UJINGA HASARA.
Rafiki yangu UTUBURE UJINGA HASARA alimaliza form four miaka miwili nyuma na kupata alama ambazo zilimfanya ashindwe kuendelea na elimu ya sekondari na kutokana hali ya maisha ikashindikana hata kwenda chuo cha kati wala cha ufundi hivyo ikamlazimu kubaki nyumbani kufanya kibarua chochote kinachomjia mbele, ninakumbuka siku nilikuwa naperuzi mtandaoni nikaonana na tangazo la NBS kuhusu kutangaza nafasi kwa wanao hitaji kuwa makarani na wasimamizi wa maudhui pamoja na wasimamizi wa TEHAMA nikaamua kizuri kula na mwenzako kwakuwa rafiki yangu alikuwa amekidhi vigezo vyote akaamua kwenda internet cafe na kuomba baada ya wiki kadhaa jina lake likatoka miongoni mwa waliopita mchujo na kwenda kwenye interview huko pia akafuzu na kufanikiwa kuhudhuria semina ambazo zilimfumbua mawazo yake na kumwonyesha mwelekeo mwengine mpya wa maisha.
Wakati anahudhuria seminar walianza kulipwa kidogo kidogo na bwaba UTUBURE UJINGA HASARA akaamua kwanza kufungua akaunti ya benki na kuhifadhi pesa zake huku akiwaza atafanya kazi gani baada ya kumaliza zoezi la sensa.
Hivyo ikamlazimu rafiki yangu kuongea na kufata watu mbalimbali wenye ujuzi ili kupata maarifa kuhusu biashara mbalimbali faida na hasara zake ili mara tuu baada ya kumaliza sensa asikae na pesa pasi na kukosa biashara ya kufanya.
Mara baada ya zoezi la sensa kukamilika rafiki yangu aliaamua kwanza kutumia baadhi ya pesa kujiongezea ujuzi hivyo akaamua kwenda kusomea udereva wa magari makubwa na matrekta na kufanikiwa kumaliza hivyo ikamlazimu kutafuta leseni na kupata kiasi kilichobakia akaamua kwenda kukifanyia biashara huku akiwa anatafuta kazi kutokana na ujuzi aliousomea maana wahenga wanasema kazi hupatikana ukiwa kazini hivyo huku anaendelea na biashara zake UTUBURE UJINGA HASARA akawa anatafuta sehemu ya kufanyia kazi ujuzi wake aliojifunza ili kuongeza vyanzo vya mapato mwishowe mola amtumpi mja wake rafiki yangu alipata ajira kwenye kampuni kubwa ya ujenzi na kuwa dereva wao wa matrekta na hapo ndipo maisha ya rafiki yangu yalipoanza kubadilika kutoka kuwa kijana wa mtaani mpaka kuwa dereva wa mkataba wa kampuni kubwa ya ujenzi nchini pia ana miliki pia biashara yake mwenyewe.
Huu ni mfano wa kijana mmoja tuu ambapo vijana kibao kila pande ya Tanzania walijitokeza kwenye zoezi la sensa na kufanikiwa kubadilisha maisha yao kwa namna moja ama nyingine. Vijana wote hao wanatoka kwenye familia tofauti tofauti hivyo jamii kwa ujumla imeweza kubadilika kwa kuwa ukibadili vijana umebadili jamii vijana wameweza kuanzisha biashara zao na kupata kitu cha kuwaongezea kipato chao hivyo sensa imeweza kugusa maisha ya jamii moja kwa moja kwa takwimu zilizopatikana serikali inaweza kupanga mipango kibao ya kimaendeleo pia vijana wameweza kujipatia pesa ambazo wakiweza kuzitumia vizuri kimaendeleo zitawatoa kimasomaso naweza kumalizia kwa kusema asiyeshukuru kidogo kamwe hawezi kushukuru kikubwa.
Hii sio stori tu ya kusoma bali kuna kitu cha kujifunza tukizingatia na kutilia manani.

Upvote
1