Sendliver mzee
Member
- Jul 31, 2012
- 9
- 6
Katika karne tuliopo, teknolojia inatumika kwa kiwango kikubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya biashara. Teknolojia imekuza sekta hii kwa kutoa huduma kwa haraka, ufanisi na kwa gharama nafuu.Pamoja na faida lukuki za teknolojia katika nchi yetu, katika upande wa kibiashara, sekta hii inakumbana na changamoto kubwa ya UTAPELI hasa katika biashara zinazofanyika kwa njia ya mitandao.
Sekta ya biashara inatumia teknolojia kwa kiwango kikubwa hasa wakati wa mawasiliano ya kibiashara na wakati wa malipo ya huduma/bidhaa kupitia miamala ya simu na miamala ya kibenki pale inapotokea mtoa huduma/muuzaji wa bidhaa yupo mbali na alipo mteja.
Wafanyabiashara wa bidhaa hutumia njia ya mtandao kutangaza biashara zao kwa wateja wao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram nk.
Pamoja na kuwa teknolojia kuongeza wigo wa matangazo ya kibiashara kwa njia ya matangazo ya mitandao ya kijamii, kumekuwepo na wimbi kubwa la MATAPELI WA BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO wanaotangaza biashara mitandaoni na anapopatikana mteja, matapeli humlaghai mteja kwa kumtaka alipie kwanza bidhaa kabla ya kutumiwa mahali alipo. Mteja baada ya kufanya malipo, matapeli hawa hukata mawasiliano na mteja na kusababisha hasara kwa mteja. Hii hupelekea kupunguza imani na kasi ya kufanya biashara mitandaoni.
NAMNA TEKNOLOJIA ITAKAVYOTUMIKA KUONDOA CHANGAMOTO YA UTAPELI WA KIBIASHARA MITANDAONI.
WAHUSIKA
1. MTEJA WA BIDHAA2. MFANYABIASHARA
3. WATOA HUDUMA ZA MIAMALA (MITANDAO YA SIMU AU BENKI)
4. MSAFIRISHAJI (MABASI YA ABIRIA/NDEGE)
Mambo anayopaswa kufanya mnunuzi wa bidhaa ya mtandaoni (Mteja)
Kwa kuwa njia za malipo ni kupitia miamala ya simu na benki, watoa huduma za miamala (simu na benki) wataongeza kipengele cha ‘biashara mtandaoni’ katika ‘menu’ za malipo kwa njia ya simu au benki. Kipengele hiki kitafanya kazi kama ifuatavyo.
i. Mteja ataingia katika ‘menu’ ya kutuma pesa kwa mtandao husika kisha atachagua kipengele cha biashara mtandaoni,
ii. Ndani ya kipengele cha biashara mtandaoni atakutana na kipengele kingine cha fanya malipo ya bidhaa.
iii. Ndani ya kipengele cha ‘fanya malipo ya bidhaa’ atakutana na kipengele cha Ingiza namba ya mpokeaji na hapo ataingiza namba za muuzaji wa bidhaa hiyo anayonunua.
iv. Mteja baada ya kuingiza namba ya muuzaji wa bidhaa kipengele kitakachofuata kitakuwa Weka kiasi na hapa mteja atatakiwa kuweka kiasi cha fedha ikiwa ni pamoja na gharama za kutuma mzigo kama walivyokubaliana na muuzaji.
v. Baada ya kuweka gharama za usafiri mteja atathibitisha malipo kwa kuweka namba za siri ila fedha hazitaingia moja kwa moja kwenye simu ya mpokeaji (zitawekwa pending na mtandao husika) ila muuzaji atapokea ujumbe kupitia simu yake unaoonesha kiasi cha pesa kilichoshikiliwa na watoa huduma ili ahakiki kiasi atakachopokea pindi mteja atakapopokea bidhaa yake.
vi. Baada ya mteja kuthibitisha muamala mteja pamoja na muuza bidhaa watapokea ujumbe mfupi (sms) wenye nambari (CODES) zinazofanana ambapo mteja atatumia ‘codes’ hizo kama utambulisho wa bidhaa yake wakati wa kuchukua katika ofisi atakayopokelea bidhaa yake. Muuzaji naye atatumia ‘codes’ hizo kuziandika katika box/bahasha au mfuko wa bidhaa hiyo katika ofisi za kutuma bidhaa (ofisi za mabasi) kama utambulisho wa bidhaa ya mteja wake.
vii. Mteja (mtuma fedha) pia atapokea ujumbe mwingine wenye ‘codes’ ambazo zitatumika na ofisi za mizigo kuidhinisha fedha zilizoshikiliwa (pending) wakati wa kutoa mzigo wa mteja ofisi za mizigo.
Mambo anayopaswa kufanya muuzaji wa bidhaa ya mtandaoni (Mfanyabiashara).
Baada ya mfanyabiashara kupokea ujumbe mfupi (sms) wenye kuonesha jina la mteja, nambari za simu za mteja, pamoja na kiasi cha pesa kilichotumwa na mteja wake, mfanyabiashara atafanya yafuatayo.
i. Mfanyabiashara atafunga bishaa/mzigo wa mteja kisha ataandika juu ya mzigo taarifa zifuatazo,
a.‘Codes’ za utambulisho wa bidhaa ya mteja alizopokea kwa ujumbe mfupi wa sms.
b. Nambari za simu za mteja zilizofanya malipo
c. Nambari zake za simu zilizotumika kupokea fedha
d. Jina la ofisi za basi pamoja na mahali (mkoa) ambapo mteja atakapopokelea mzigo.
ii. Baada ya kuandika taarifa hizo juu ya kifurushi/bahasha yenye bidhaa ya mteja, mfanyabiashara atapeleka bidhaa/mzigo huo katika ofisi za basi walilokubaliana na mteja wake na kulipia gharama za usafirishaji wa bidhaa hiyo. Ikumbukwe gharama za kutuma mzigo, mteja alishazilipia katika muamala aliofanya hapo awali.
Mambo anayopaswa kufanya mtoa huduma katika ofisi za kupokelea mzigo wa mteja (Ofisi za mabasi).
i. Mtoa huduma katika ofisi za mizigo atamtaka mteja kutaja nambari za mzigo wake ili kujiridhisha kama mzigo ni wa mtu sahihi. Baada ya hapo mhudumu ataingia katika ‘menu’ ya miamala ya simu na kuingia katika ‘menu’ ndogo ya biashara mtandaoni kisha atachagua kipengele kinachosema idhinisha muamala wa kibiashara.
ii.Baada ya kuchagua ‘idhinisha muamala wa kibiashara’ kipengele kinachofuata atachagua ingiza nambari (codes) ya mzigo na hapo mtoa huduma ya mizigo ataingiza zile ‘codes’ zilizoandikwa kwenye mzigo wa mteja.
iii. Kipengele kinachofuata ni ingiza namba zilizotuma fedha. mtoa huduma ataziingiza namba zilizotuma fedha zilizoandikwa kwenye mzigo wa mteja kisha kipengele kinachofuata ni ingiza nambari zitakazopokea fedha na hapa mhudumu ataandika nambari za mfanyabiashara zilizotumika kutumiwa fedha.
iv. Kipengele cha mwisho ni kumtaka mteja kutoa nambari (codes) za kukamilisha muamala uliokuwa haujakamilika baada ya mteja kukagua mzigo wake na kujiridhisha. Mtoa huduma ya mizigo ataingiza nambari hizo kisha mfumo wa mtandao wa simu/benki utajiridhisha kama taarifa zote ni sahihi na baada ya hapo mfumo utaruhusu pesa kuingia katika akaunti ya mfanyabiashara na mteja atachukua mzigo wake.
Endapo mteja baada ya kukagua mzigo wake na kugundua kiasi/idadi ya bidhaa haipo sahihi au sio bidhaa walizokubaliana na mfanyabiashara, mteja hatatoa nambari za kuruhusu muamala bali ataingia kwenye simu na kusitisha muamala kwa kuingiza zile nambari kwenye kipengele cha kusitisha malipo ya kibiashara. Mfanyabiashara atalazimika kulipia usafiri wa kurudisha bidhaa yake katika duka/ofisi yake.
Faida za kutumia mfumo biashara mtandaoni
1. Iinamalliza changamoto ya utapeli mitandaoni na kuondoa hofu ya kutapeliwa mitandaoni kwa wateja na wafanyabiashara hivyo kuongeza kasi ya biashara mitandaoni.2. Itasaidia serikali kupata kodi mpya kutoka katika biashara za mitandao kwa kukata angalau asilimia moja (1%) ya fedha zinazotumwa kwa njia malipo ya biashara mtandaoni.
3. Itasaidia mteja kupata bidhaa halisi iliyo na ubora waliokubaliana na mfanyabiashara kwani mfanyabiashara ataogopa kutuma mzigo ‘fake’ kwani endapo mteja ataukataa mzigo, mfanyabiashara atalazimika kuingia hasara ya kutuma na kurudisha mzigo uliokataliwa na mteja.
Upvote
1