Jinsi tumbua na Uhamisho unavyofuja pesa za Serikali, unnecessarily

Jinsi tumbua na Uhamisho unavyofuja pesa za Serikali, unnecessarily

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Kwanza kabisa lazima tujiulize je serikali hii ina mpango wa kupunguza matumizi yasiyo na ulazima wowote au yenyewe Haina huruma na pesa za walipa Kodi, Kwasababu action za serikali zinaitia hasara serikali pakubwa sana. Jamani hasara za riba ya mikopo ningedhani yatosha , kumbe bado tuna hasara zisizo na umuhimu.

Serikali Kwa ujumla wake Kila mwaka inafuja zaidi ya Bilioni 50 ikiwa ni gharama za uhamisho wa watumishi , mabalozi ,wakurugenzi na wafanyakazi mbali mbali wakiweno wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, etc, kuhamisha watumishi watumishi ni jambo zuri kiutendaji lakini linapaswa kuangalia, imekuwa Sasa ni mitindo ya kupiga pesa za Serikali huku wananchi wakikosa huduma za muhimu.

Pili serikali na tumbua tumbua inaongeza bili ya mishahara mamilioni Kwa mamilioni ya Kodi ya wananchi yanapotea, mfano Kwasasa Kuna wakurugenzi zaidi ya 160 waliotumbuliwa na hawana Tena vyeo vya ukurugenzi lakini wanakula mshahara wa ukurugenzi, huku nafasi zao Tena Kuna wakurugenzi wanaohudumu. Hisia za chuki ndani ya watumishi wa serikali na Siasa za chama zisiingizwe na kuiletea serikali hasara ya mabilioni ya Fedha.

Hii nchi lazma tuipende, hata sisi wananchi tungetamani Kila mwaka tuweke serikali mpya , lakini itakuwa ni hasara Kwa taifa. Kila siku tumbua tumbua , ni kama vile serikali Ina Rais tu na Waziri , na spika wengine wote inabidi kujaribu Leo weka huyu, kesho yule, keshokutwa huyu.

Sasa imefikia hata mtu kutenguliwa imekuwa ni desturi na jambo la kawaida tofauti na wakati Wa Nyerere ukitenguliwa kweli uliharibu mno
 
Back
Top Bottom