Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 180
FP, IPTL is being liquidated lakini kinachoniacha gizani mimi ni hayo mengine kuhusiana na hiyo akaunti na huo mkwanja
Mkuu, mdeni mkubwa wa IPTL ni tanesco (sidhani kama kuna mdeni mwingine). Mihela hiyo ni jumuiko la malipo ya capacity cahrges ambazo serikali iligoma kulipa baada ya kugudua ujanja wa IPTL. Kimkataba nadhani serikali ilitakiwa kuweka fedha hizo katika hiyo account wakati wa mgogoro. Sasa hapa ndipo nataka kufahamu modalities za liquidator kudhibiti hiyo account wakati kimsingi mgogoro haujamalizika. na sijui kama kweli serikali ilishaweka fedha hizo kwenye account baada ya kugoma kuwalipa IPTL.Mpita njia,
Nilivyoelewa mimi,hiyo Escow Acounti ilifunguliwa BOT ikiwa chini ya udhibiti wa RITA (Kama Liquidator).
Huo mkwanja 138bil ni madeni ambayo IPTL inawadai wateja wake...hopeful tanesco....lakini kati ya hayo medeni, kuna mengine yana mgogoro na mengine hayana mgogoro.....yale yenye mgogoro malipo yake yanatakiwa kulipiwa kupitia Escrow account wakati yale ambayo ni clean yanalipwa kwenye account ya IPTL!
Mimi maswali yangu on this ni kama kny post yangu hapo juu tu!
Wakuu,
Na huu ndiyo wakati mwanana wa kujua ECONOMIC RESCUE PACKAGE yetu ambayo nayo imetangazwa hivi karibuni itaelekezwa wapi.
... Sasa hapa ndipo nataka kufahamu modalities za liquidator kudhibiti hiyo account wakati kimsingi mgogoro haujamalizika. na sijui kama kweli serikali ilishaweka fedha hizo kwenye account baada ya kugoma kuwalipa IPTL.
Hii account imefunguliwa kutokana na matakwa ya mkataba. Kwa nini liquidator asifanye reference ya mkataba kuhusiana na management ya account na anakwenda mkoja kwa moja kwenye sheria? na sheria yenyewe anatumia kifungu controversial
Samahani mkuu, ina maana IPTL ndo inaishia? Je aliyeandika si ndo yule mmbongo wao? Mbona barua imekaaa kidesign?
Jamani,
Mimi nadhani huu ndio ushindi mkubwa. IPTL kufilisika maana yake ni vyema kwetu.
Mfilisi wowote lazima atafute mali za hiyo kampuni popote zilipo maana ndio kufungasha virago hivyo ati.
Hata ngeleja amesema issue ya IPTL iko mbioni kuishia.
Mkuu hakuna anayepinga wala kuchukizwa na kufilisika kwa IPTL, macho yetu ni hizo 138billion. Hizo si fedha kidogo mkuu, ni nyingi kuliko zilizoibiwa EPA.
Based on the scale of business hela wala sio nyingi.. watu wanafikiria in personal terms.. BOT inaliwa vipi sasa.. hizi hela ni mali ya IPTL walionayo kihalali kutokana na mikataba mibovu yakina Mary Ndossi na Chenge.. That is how they became billionaires.. Nothing new here...
...good point,watu wanasahau wanaotia hasara Taifa ni hao walio madarakani walafi wa 10% & wasiojua kitu,ukiangalia vizuri hao IPTL hawajavunja sheria yeyote zaidi ya kutumia incompetence ya viongozi wetu,hakuna haja ya kulaumu IPTL dawa ni kuwashughulika hao waliotuingiza kwenye hiyo mikataba!
Sasa rafiki yangu wewe ukichaguliwa kuwa mfilisi, utaanza na nini, accounts zote za kampuni husika na asset zake au sio? Au wewe utaanza na kufuatiliwa wadeni wa kampuni husika?
Sasa hizo hela lazima kimahesabu ni za IPTL otherwise Mfilisi asingekurupuka na kusema hivyo.
Alafu kumbuka mara nyingi mfilisi anakuwa mtu aliyekubaliwa na wadau wakubwa wa hiyo kampuni.
This is typical normal procedures za ku-close down business... cha ajabu nini? hela nyingi? sasa unadhani IPTL isikuwa inafanya biashara ya kuuza ukwaju?
Mwaka huu tutaona mengi, ... Kumbuka tunaelekea 2010 na zinatafutwa pesa mapema.
Hawa jamaa wa sasa hivi ni smart kidogo kulinganisha na watangulizi wao, mwaka 2005 jamaa walichelewa ku-fundraise na pesa ikatoka mwishoni sana na kusbabisha Sumaye & Co. kushindwa kukampeni sawasawa.