Jinsi tunavyoendelea kuliwa kupitia BoT!

Yaaani pamoja na mafisadi kibao kukalia joto ya jiwe, pamoja na kuwa jamii sasa imeanza kufumbuka macho, yaaani bado kunawengine wanaendeleza libeneke la ufisdi, kweli wanachama wa ufisadi wanaroho ngumu. Lakini najiuliza wanajidaia kitu gani hasa?
 

J.B.R. ni mwekezaji wa kitanzania, hatari sana. Ndie alieileta TRITEL na IPTL na ndie aliekuwa partner wao hapa TZ. Pamoja na kuwa partner, hakuwa na pesa zozote za ku-invest. Alipewa shares kutokana na % za uwekezaji wa nje unaohitajika nchini. Baada ya kutakiwa kuendelea ku-invest na kushindwa, alizipeleka zote mahakamani na kudai pesa nyingi. Alisababisha TRITEL kutoroka baada ya kuona kuwa wanashindwa kesi na kupoteza kila kitu.
 


Ninachopendea wahaya wanajua namna ya kupata hela chapuchapu kwa deal. Rwega, Lukazas....you name all!!! I salute you man.
 
Kama Kikwete ana uhakika wa kushinda kwa "kishindo" kwenye uchaguzi ujao, inakuwaje tena anarudia sinema ya 2005?
 

Na sasa mmesikia leo huko Dodoma .....inakuja EPA in the making......Stimulus Package kwa vyama vya ushirika etc ....! Sasa itakuwa ''Jinsi tunavyoendelea kuliwa kupitia STIMULUS PACKAGE as well!
 
Ukweli uko wazi ila wahusika wameziba masikio,ngoja 2010 ifike nitakula pesa yao na siwapi kura mafisadi.
 
napandwa na kichaa.
ina maana mabilioni wanayolipwa monthly yalikuwa noti feki??

Lakini kwa kuwa WATANZANIA wenzetu wameamua kwa dhati kabisa kuisaliti nchi kwa kukubali kuingia mikataba inayokula kwetu, basi tutajua hopw to cane them kwani ni watoto wetu, vijana wetu na wazee wenzetu....

Tutakula nao sahani moja hadi zirudi. kama si leo ni kesho na ikishindikana itawezekana tu!
 
Order ya Mahakama imetoka jana IPTL iwe wound up, RITA wanatakiwa kupata agent wa ku-liquidate IPTL haraka sana.

This means, assets za IPTL zitagawanywa kwa lenders na tunaweza kubaki na mtambo kama mali yetu (taifa).

Kuna taarifa kuwa Mechmar ambao ni wabia kwenye project hii wanataka ku-block, uharaka wa RITA utatusaidia katika hili.

Kuna kama 207bil Central Bank ktk escrow account, sehemu yake inaweza kutumika kuugeuza mtambo wa IPTL kuwa wa gesi.
 

Hivi aliyekuwa msimamizi wa RITA si walimbadilisha?
ni kwa nini?
 
Kibanga, swali lako gumu (over RITA) lkn tuna mtu amefuatilia na nimemwomba afuatilie sababu ya kubadilishwa kwa msimamizi
 
RITA ina uzalendo wa kuifanya iwe na 'uharaka' unaohitajika?! Isiwe ni mazingaombwe yao kama kawaida.
 
kumbe ndo maana Dr. Slaa hawamuwezi hawa jamaa.

Hivi liquidation ya IPTL ndo salama ya mafisadi waliotajwa kwenye saga zima?
 
Kibanga, swali lako gumu (over RITA) lkn tuna mtu amefuatilia na nimemwomba afuatilie sababu ya kubadilishwa kwa msimamizi

Fafanua kidogo ni kipi wanachotakiwa kufanay ho RITA ilizoezi likamilike, na ni Kipi kikifanyika zoezi halitakamilika?
 
Hii kitu mbona inafanywa underground sana. Inamakusudi ya kuponyesha watu flaniflani ama?
 
Sasa ndio nini , si fedha za watu hizo? mbona kichwa cha habari na habari yenyewe vitu tofauti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…