Jinsi tunavyotengeneza kizazi dhaifu kijacho pasipo kujua

Jinsi tunavyotengeneza kizazi dhaifu kijacho pasipo kujua

briophyta plantae

Senior Member
Joined
Feb 18, 2017
Posts
117
Reaction score
132
Habari wana jamii..
Kwa ufupi tu ningependa tuongelee hii changamoto ambayo wengi pia waaifahamu na wanajua inaathiri vp jamii.

Tangu hapo mwanzo jamii imekuwa ikibadilika kizazi hata kizazi katika namna tofauti kulingana na nyakati nanamna ya kuishi katika nyakati husika. Kubadilika kwa vizazi hivi huwa na matokeo chanya na matokeo hasi pia kwa wakati mmoja.

Wanadamu ana uwezo wa kubadilika namna ya kuishi kutokana na mazingira na nyakati husika ili aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Kwa ulimwengu unapoelekea inahitaji watu wenye uimara,afya bora ya mwili na akili, na jamii hii ya watu inatokana na kizazi kilichopo kwa sasa. Ili uweze kuwa na kizazi bora basi inahitaji kizazi kilichopo kiwe kina maono ya kule tunapoelekea.

Familia bora inajenga kizazi bora,malezi bora yanajenga kizazi bora, mitazamo bora kwa wazazi wa sasa inaenda kujenga kizazi chenye mitazamo bora zaidi.. hivyo basi,matokeo ya kizazi kilichopo sasa hivi,iwe katika matokeo chanya au matokeo hasi basi yanatokana na matokeo ya kizazi kilichopita.

Je kwa uelewa huu wa kawaida nilioielezea ambao najua upo katika ufahamu wa wengi wetu tunaweza kujiuliza masuala haya?!

1.Tunafamilia zilizo bora, zitakazoenda kutupa matokeo a kizazi bora kijacho?

2. Malezi ya mzazi mmoja single mothers au single father ambayo yemekuwa fasheni kwa sasa je yanaenda kutengeneza watoto waliotimamu kukabiliana na changamoto zijazo?

3. Jamii inatimiza wajibu wake sawa sawa kuandaa kizazi kijacho chenye nguvu kitakachoenda kutuletea mabadiliko na kufanya mapinduzi katika mambo makubwa huko mbeleni?

4. Kizazi kilichopo sasa kina madhaifu gani tuliyoyabeba kutoka kizazi kilichopita nyuma yetu?

5. Nini tunapaswa kufanya?
Mchango wenu wa mawazo ni muhimu.

FB_IMG_1728109472428.jpg
 
Back
Top Bottom