Jinsi Tundu Lissu Alivyojikaanga Kwa "Mafuta ya Taaluma Yake!!"

Suala sio hati bwana mdogo....suala ni uhalali wa hiyo hati!!!umemsikiliza msekwa alichoongea leo lakini?
 
Akili ndogo kutawala akili kubwa ni shida kweli! Ngoja nilale nidamkie fukwe za bahari ya hindi kutafuta birth certificate yangu!
 
Usitoe majibu ya jumla kama hivi, hutaeleweka!

argument yako umetumia poor reasoning...
fallacy yako ni that of distraction ume fail kuprove conclusion kwasababu ya irrelevant evidence instead u've let your emotions do your argument
u've come about the fallacy intentionally to manupulate us! well that might be due to your carelessness au IGNORANCE chagua
 

Mkuu, umeua, harudi tena na kama akirudi hatatoa jibu la kueleweka zaidi ya povu na hasira za kufukuzwa umod.
 

Sidhani kama hili ni sahihi kihistoria. Nyerere anelezea vizuri juu ya sababu za kujiuzulu kwake kwenye andiko lake la "Why I Resigned" na linapatikana katika "Uhuru na Umoja" Ukurasa wa 48-52. Sababu kubwa ya Nyerere kupinga ni suala la kanuni; alipokubali kuteuliwa kuingia kwenye baraza lile alitarajia kuwa kungekuwa na majadiliano na kukubaliana baadhi ya mambo katika kile alichokiita 'spirit of give and take'. Ameelezea kwa kirefu jinsi mambo mbalimbali ambayo aliyapinga mwanzoni alijikuta anakubali ili kukutana na Serikali "half way". Hakuhoji uhalali wa Bunge lenyewe wala utawala wa kikoloni; hakupinga kwa sababu lilikuwa ni baraza lililoundwa na Mkoloni bali kwa sababu akiwa ni kiongozi mkuu wa TANU alishakubali mambo mengi ili kuonesha imani lakini hakupata lolote alilotaka kutoka kwa serikali. Mwenyewe anasema ilikuwa ni "complete surrender" (interestingly alirudia lugha hii wakati anazungumzia kusurrender kwa viongozi kwenye suala la Tanganyika katika kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania).

Viongozi wa sasa huko Bungeni kama wanaamini katika principle hawapaswi kuendelea kukaa huko kwa sababu wakati mwingine inabidi ujiuzulu on principle. Binafsi nitawashangaa watu wakiamua kutoka Bungeni endapo Serikali Mbili zitapitishwa kwa njia ya kura! Nyerere hakusubiri awe anaendelea kuwa defeated Bungeni ili ajiuzulu; alielewa mara moja kuwa serikali haikuwa na nia ya kushirikiana naye katikahoja zake na hivyo asingekuwa na unafiki wa kuendelea kupokea posho.

Mwenyewe anasema:

 

Bado umejibu jumlajumla japokuwa umeongeza tu idadi ya maneno!
Jibu hoja kwa hoja kama nilivyoandika hapo juu! Kama unadai hakuna logic, elezea ni kitu gani exactly hakina logic na ili kiwe na logic kinatakiwa kiweje!
 
Mkuu, umeua, harudi tena na kama akirudi hatatoa jibu la kueleweka zaidi ya povu na hasira za kufukuzwa umod.

Jifunze kwa Mzee Mwanakijiji au Mchambuzi wanavyojibu hoja kwa hoja na wala si kwa kejeli na dharau kama zenu! Tuheshimiane hata kama hatukubaliani. Sio lazima watu wote tuwe na mawazo sawa, ndivyo Mungu alivyotuumba!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzee Mwanakijiji,
Nadhani tunachopishana hapa ni tafsiri tu. Ebu tuangalie ujumbe wa msingi katika nukuu hiyo:


Kazi ya Mbunge ni ipi? Ni pamoja na kushiriki katika kutunga sheria mbalimbali zinazo affect maisha yao kijamii, kisiasa, na kiuchumi. That carries a large portion ya mbunge kuonekana ana mchango useful au useless. Kwa mwalimu kuhisi "useless", msingi wake sio kula posho za bure bali kuwa ndani ya chombo ambacho hawezi kuwa na influence katika kubadili maisha ya wananchi walio wengi (weusi katika Tanganyika), moja wapo ikiwa ni suala zima la challenging the government lakini pia jadili miswada ambayo ilikuwa inaenda kwa gavana kupata saini ya kuwa sheria. Mimi tafsiri yangu ndio hiyo, ingawa inawezekana kabisa upeo wangu katika hili ni finyu. Hivyo ndivyo nilimaanisha nilipotoa mfano wa Mwalimu na bunge la kikoloni.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Jifunze kwa Mzee Mwanakijiji au Mchambuzi wanavyojibu hoja kwa hoja na wala si kwa kejeli na dharau kama zenu! Tuheshimiane hata kama hatukubaliani. Sio lazima watu wote tuwe na mawazo sawa, ndivyo Mungu alivyotuumba!

Samahani kwa kuchepuka nje ya mada yako dhoofu. Hao uliowataja nawasoma kila mara michango yao humu lakini sijaona hata chembe ya wewe kurandana nao ktk utoaji/ujibuji wa hoja. Mara nyingi umekua ukijibu wengine humu kwa kejeli na dharau kubwa. Isitoshe mimi sijakunukuu wala sijakutaja mahali popote ila nashangaa wewe umekurupuka na kuninukuu. Tusameheane bure, tuvumiliane.
 
Last edited by a moderator:
Kama Muungano hauna uhalali wowote maana yake nini?

1. Ni kwamba Tundu Lissu alifanya makosa kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano "BATILI," kwa hiyo Ubunge wa Lissu mpaka sasa ni "BATILI!"
2. Kwamba, hata mchakato huu wa kuandika Katiba Mpya ni "BATILI" kwa kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano" BATILI,"
3. Kwamba, Tundu Lissu amechangia kutunga Sheria "BATILI" za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Bunge nalo ni "BATILI,"
4. Kwamba CHADEMA nacho ni chama "BATILI" kwa kuwa kimeundwa kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo imetungwa na Bunge "BATILI" la Muungano,
5. Kwamba, shughuli zote za kisiasa za Tundu Lissu hazina uhalali wowote wa Kisheria kwa kuwa zimefanywa kwa kufuata Sheria za Muungano "BATILI,"
6. Kama Lissu ana vyeti vya Shule za Tanzania navyo ni "BATILI" kwa kuwa vimetolewa na Serikali "BATILI,"
7. Kama Tundu Lissu amezaliwa baada ya Muungano na kupewa Cheti cha Kuzaliwa ahesabu kuwa ni "BATILI" mpaka sasa,
8. Kesi zote alizoshinda Tundu Lissu mahakamani ajue kwamba ni "UBATILI" mtupu maana" MUUNGANO HUU NI BATILI," kwa hiyo hata mahakama za Muungano ni "BATILI,"
9. Kama Tundu Lissu ameoa baada ya Muungano ajue kuwa ameumia, ni ndoa "BATILI" hiyo!!!
10..................

Ths is shallow analysis mkuu,watu tunajengwa na mazingira yaliyopo na pale tunapopata nafasi tunaitumia kubadilisha kama mifumo inaruhusu mabadiliko,leo umetuletea uchambuzi wako kuhusu mtazamo wa tundu lissu,na hukuleta uchambuzi wa mtu mwingine yoyote wa mtaani,hii inatokana na nafasi aliyonayo. Tatizo tu watu huwa tunasahau mambo mengi yanayobackfire saiv yaliwahi kutolewa maangalizo na watu mbalimbali,sema ubshi wa system iliyopo.
 
Hakugombea ubunge wa bunge. Aligombea ubunge wa Jimbo ili kuliwakilisha kwenye Bunge.
 
Sitabomoa hiyo nyumba, yaani kwa upande wa Muungano sitauvunja bali "nitapigilia msumari!" Kwa "Mwanasheria Nguli" atakuambia hiyo nyumba ni BATILI tuivunje!

Hapo ndipo upotoshaji unapoanzia. Kuwa na serikali Tatu hakufanyi kuwa muungano umevunjika. Kuwa na serikali tatu ni njia ya kupunguza kero zilizotokana na serikali mbili ili kuwa na muungano imara wenye uwazi na unaokubalika na wote huku kukiwa na equal bargaining kati ya Watanganyika na Wazanzibari.
 
Nimegundua ata we uelewa wako NIBATILI maana hujaelewa Lisu aliyokuwa anaongea! mi nakubaliana na hotuba ya Lissu kwamba muungano wetu ni batili maana kama usingekuwa batili Nyerere angepeleka hati ya muungano umoja Wa mataifa

Umoja wa mataifa wanaifahamu nchi inayoitwa TANZANIA.Naomba unifahamishe ndugu yangu, pale umoja wa mataifa JINA TANZANIA ,Walilitoa wapi, kama sio Nyerere na Karume kulipeleka?
Vitu vingene ni vya kiutendaji serikalini,hivyo huwa havitangawi,kuwa leo tarehe fulani mwezi fulani mwaka fulani tumefanya hivi.
Wanachofanya wakina Tundu Lissu ni kutafuta UMAARUFU WA KISIASA,lakini, kama msoni na mwana taalum tena ya sheria,anajuwa ukweli wa HOW THE GOVERNMENT WORKS.
 
Haya bhana mimi napita siasa kidogo kushoto kwangu....😀:banghead:😡
 
Safiria jahazi lako. Hili la lisu litakuacha kila mara lenda mrama. Hujashtuka 2
 

kweli wewe ni batili, unaleta revision za sheria ndo unasema ni mwanzo wa sheria, kwa kuwa hauelewi chochote kwenye historia ya sheria za nchi hii naona tuishie hapo...nikudokeze tu kuwa baadhi ya sheria za nchi hii kabla ya kuwa ratified na bunge la tanganyika na Tanzania zilikuwa zinaitwa ordinaces, hizi zilitungwa na mkoloni na baadhi yake bado tunazitumia mpaka kesho,zipo hata tulizoletewa na wahindi na waingereza .... kuna vitu vichache tulikuja kubadilisha na kuziita sheria, ila kwa kuwa wewe na lissu ni vitu viwili tofauti na apo mmoja ni batili, basi kama uelewa wako ni kuwa sheria ulizozitaja zimeanza miaka ya 70 basi inawezekana watu wengi wana mawazo batili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…