barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,880
Utenguzi wa Mkurugenzi wa NIMR unahusishwa na tamko lake juu ya "status" ya ZIKA Tanzania.Alipotamka Dr Mwele na Ummy Mwalimu akakanusha.Watu wanaiogopa Zika na Zika huwachanganya watu kila itangazwapo.Imekuwa Dar es Salaam na ilikuwa Vatican.
Kanisa Katoliki limewahi kutikiswa na kauli ya Papa juu ya Ugonjwa wa ZIKA.Katika safari yake toka Mexico Papa alitolea kauli juu ya ugonjwa wa ZIKA,kauli iliyotikisa kidogo kanisa na mafundisho yake.
Papa Francis alikumbana na swali juu ya hatari ya ugonjwa wa ZIKA kwa wanawake,na ni nini msimamo wa kanisa katika kutumia njia za kisasa kwa wanawake kuzuia ugonjwa huo.
Kuna kanuni katika kanisa katoliki inasema "The Principle of the lesser of two evils".Yaani panapokuwa na vitu viwili vyenye "utata" unachukua kilicho na unafuu wa utata.
Kanuni hii iliwahi kutumika miaka ya 1960 huko Zaire(DRC ya leo).Papa Paul VI "aliruhusu" watawa wa kike waliokuwa Zaire kutumia "contraceptives" sababu walikuwa wanabakwa sana na kupata mimba wakati wa Civil Wars.Hali hii ilifanya watawa wengi kupata mimba wasizozitarajia.
Tatizo hilo lilikuwa kubwa kiasi cha Pope Paul VI kuchukuwa kanuni ya "Lesser of two evils".Kwamba ni kuwaacha wabakwe na kujazwa mimba,au kuwaruhusu kutumia vidonge vya majira ili kuepukana na mimba zisizo na hiyari.
Mtihani huu kwa kanisa umekuja tena baada ya ZIKA.Papa alitanabaisha kuwa "Abortion is absolute evil than Contraception and Condoms,avoiding pregnancy is not an absolute evil".Hii ilikuwa ni kama kasema "indirectly" kuwa ni bora mtu akatumia kondomu au vidonge vya majira ili kuepuka kuwa na mtoto mwenye virus vya ZIKA .
Kauli hii ilizua taharuki ktk viunga vya Vatican,ikamuibua msemaji wa Vatican wakati huo Pd.Federico Lombardi na kukanusha kuwa kauli ile haimaanishi kanisa limelegeza msimamo na sasa watu wanapaswa kutumia kondomu na vidonge vya majira;ambavyo kwa mujibu wa kanisa mambo haya hayaruhisiwi na ni mizizi ya dhambi.
Kauli hii iliwapa tabu sana Vatican,kuikanusha na kuirekebisha.ZIKA inazua mengi,laiti kama ingelikuwa ndio Pope "anatumbulika" kama Dr Mwele,jua lisingetua Vatican tumgesikia mengine.
Kauli za Zika si Tanzania tu,hata Vatican iliwahi kutikisika kwa mmoja kuizungumzia Zika.Zika imezika watu na vyeo vyao.