SoC03 Jinsi ujenzi wa ghala la kisasa ulivyosababisha majonzi makubwa kwa wanakijiji

Stories of Change - 2023 Competition

EDOGUN

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2023
Posts
256
Reaction score
302
Ni majonzi makubwa yamekighubika kijiji kizima cha Mukalinze.Wanakijiji wote, wanaume na wanawake ni kama tumepoteza sababu ya kuyafurahia maisha kwa pigo lilokipiga na kukijeruhi vibaya kijiji chetu hiki kikongwe.

Kama sasa hivi akifika mgeni ghafla hapa kijijini kwetu,anaweza kufikiria pengine huenda kijiji chetu kimepatwa na msiba wa mtu maarufu na muhimu sana kijijini.

Pengine sasa hivi akifika mgeni ghafla kijijini kwetu,anaweza kufikiria labda kijiji kimepatwa na janga la kiasili kama vile ukame, uliokausha mazao yote ya wanakijiki na kuua maelfu ya mifugo yao.

Pengine kama sasa hivi akifika ghafla mgeni hapa kijijini kwetu anaweza kufikiria kuwa kijiji kimevamiwa na kundi kubwa la nzige waliokula mazao yote kwenye mashamba ya wanakijiji.

Kama sasa hivi akifika mgeni ghafla hapa kijijini kwetu,anaweza kufikiria kuwa kijiji kimekumbwa na mafuriko yaliyosomba mazao yote toka kwenye mashamba ya wanakijiji.

Lakini kumbe,leo kijiji hakijapatwa na msiba wa mtu yeyote yule,wala hakijakumbwa na janga lolote la asili,ila kilichofanya wanakijiji wengi leo tuwe katika hali hii ya majonzi makubwa ni kitendo cha ardhi yetu,tuliyoiandaa kwa muda mrefu,kwaajili ya ujenzi wa zahanati ,kuchukuliwa kirahisi rahisi kabisa na Halmashauri ya wilaya kwaajili ya ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia kahawa.

Ukweli kitendo hiki cha Halmashauri ya wilaya yetu kulibadilishia eneo hili matumizi kimetuumiza sana wanakijiji wengi wa kijiji cha Mukalinze kama sio wote.

Kinachotuumiza zaidi ni ukweli kuwa hapa kijijini hakuna mwanakijiji hata mmoja anaelima zao la kahawa kwahiyo hilo ghala tunaloambiwa kuwa litakuwa ni kubwa na la kisasa sana,litatumika kuhifadhia kahawa zinazotoka vijiji vilivyoko mbali sana na kijiji chetu .

Kila tunapojaribu kufikiria sababu ipi hasa ya ujenzi huu wa ghafla wa ghala hili la kuhifadhia kahawa hapa kijijini kwetu wakati sisi wanakijiji hatujishughulishi kabisa na ulimaji wa zao la kahawa ni ipi, hatupati majibu kabisa,ingawa zipo tetesi kuwa Halmashauri imekwepa ghalama ya kulipa fidia huko mjini hivyo wamefikia maamuzi ya kujenga ghala hilo huku kijiji kwetu ambako bado kulikuwa na hii ardhi kubwa ambayo bado haijamilikishwa kwa mtu/watu.

Pia licha ukweli kuwa kijiji chetu kimeporwa ardhi hii bure kabisa, kuna tetesi za wakubwa fulani wa Halmashauri kukwapua mamilioni ya fedha ya Hamashauru kwa kisingizio cha ununuzi wa ardhi hii hii waliyotupora.Pia kuna tetesi kuwa hata ile gari mpya ya gharama ya mtumishi mmoja mkongwe wa hii Hamshauri yetu ni zao la sehemu ya mgawo wake wa hizo pesa haramu walizojipatia kupitia uporaji wa ardhi yetu.

Kwa kweli,kijiji chetu kilikuwa na matumaini makubwa sana ya kuifanikisha ndoto ya kujenga zahanati kubwa kabisa kijijini ili kuepukana na adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kwenye zahanati ya kijiji jirani kufuata huduma za matibabu.

Kwa kweli,ujenzi wa zahanati hii ilikuwa ni ndoto ya kila mwanakijiji wa kijiji chetu hiki,ndio maana wanakijiji wote tulishirikiana bila kushurtushwa na yeyote yule,kufyatua tofali,kukusanya mawe,kuandaa kokoto na kusomba kiasi kikubwa cha mchanga tayari kwa kuanza ujenzi wa zahanati yetu lakini ghafla imekuja taarifa hii mpya ya ghafla kutoka huko mjini ya ujenzi wa ghala la kahawa kwenye kiwanja tulipokusudia kuijenga zahanati yetu.

Kibaya zaidi tunasikia kuwa tofali zote,mawe yote,kokoto zote na mchanga wote tuliokuwa tumeuandaa kwaajili ya ujenzi wa zahanati,vyote vitakwenda kutumika kwenye ujenzi wa hilo ghala la kisasa la kuhifadhia kahawa, kweli wahenga hawakuwa wajinga kusema :"akutukanae hakuchagulii tusi."Wanakijiji wa mukalinze tumetukanwa na watu waliotakiwa kutuheshimu sana.

Mpaka kufikia sasa,wanakijiji wote wa kijiji cha Mukalinze hatujui tufanye kitu gani kuuzuia huu ujenzi wa jengo tusilokuwa na uhitaji nalo kabisa.

Wanakijiji tunatamani basi angalau serikali wangetujengea hata shule ya sekondari kama wameona hatukutakiwa kujenga zahanati kijijini.

Wanakijiji tunatamani basi angalau serikali wangetujengea bwawa kubwa la maji litakalotusaidia kunyweshea mifugo yetu kama wameona zahanati haikuwa wazo sahihi.

Wanakijiji wa kijiji cha mukalinze tunajiuliza kwa nini mawazo yetu yamepuuzwa kirahisi namna hii, wakati sisi ndio tunaojua vipaumbele vyetu.Sisi ndio tunaojua adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya matibabu kijiji jirani.

Sisi ndio tunaojua adha ya wake zetu na binti zetu kujifungulia majumbani kwa sababu ya kijiji chetu kutokuwa na Zahanati.

Kwa sasa sisi kama kijiji inaonekana ni wazi kabisa hatuna mabavu ya kuzuia ujenzi wa ghala hili la kuhifadhia kahawa ingawa kuna tetesi kuwa baadhi ya wanakijiji wanapanga kuwashawishi wazee wa kimila, kufanya tambiko maalumu la kuiomba mizimu itusaidie kusitisha ujenzi huu unaoonekana kuwa haramu,kwa mtazamo wa wanakijiji wengi kama sio wote wa hiki kijiji chetu kikongwe.

Pia kuna tetesi toka huko kwenye vilabu vya pombe kuwa kuna kikundi fulani cha wanakijiji kimejiandaa kikamilifu kuiba vifaa vyote vya ujenzi wa ghala hili ,endapo mazingira yatawaruhusu kufanya hivyo,eti ili angalau kuonesha hasira zao kwa mawazo yao kupuuzwa

Vilevile kuna tetesi kuwa,wanafunzi wa shule ya msingi mukalinze, wameapa kuhakikisha wanayageuza mazingira yanayozunguka ghala hilo kuwa choo au basi angalau kufanana fanana na choo.

Wanakijiji hatuchoki kujiuliza kwa nini hatukushirikishwa kwenye maamuzi ya kubadili matumizi ya ardhi yetu hii wenyewe.

Kwa sasa imekuja taarifa kuwa, kesho asubuhi ,mafundi kutoka mjini ,wataanza rasmi kazi ya ujenzi wa hilo ghala la kifahari na pia kuna tetesi kuwa,
wataambatana na vibarua wao wenyewe kutoka huko huko mjini,hivyo sisi wanakijiji wa kijiji cha mukalinze,ngoja tu tulale, huenda labda utatokea muujiza wakati tukiwa usingizini, utakaobadilisha maamuzi ya wakubwa,waliopitisha ujenzi wa wa ghala hili kubwa na la kisasa lisilohitajika hata na wendawazimu wakao kijiji kwetu.
 
Upvote 4
Naombeni kura zenu wanajukwaa wenzangu
 
ni wapi na halmashari, habari y kujua vijiji vyenu , sema n8i mkoa upi, wilaya ipi na halmashauri ipi
 
Bandari ni ya watanzania wote na sio wa kijijini kwenu tu,this time keki hii itagawiwa Kwa watanzania wote na sio nyie wezi pekee
 
Back
Top Bottom