Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Wote tunaishi dunia hii, lakini kwa namna gani tutaiangalia sayari yetu ya dunia, itategemeana na hisia au feelings tulizo nazo katika wakati husika.
Iko hivi, ukiwa na hisia hasi au kuwa na hasira au huzuni, hakika utaiangalia dunia katika namna mbaya sana,mtu kama huyu atalaumu kila kitu ambacho kiko mbele yake, si ajabu mtu huyu atalaumu hata hali ya hewa, kukiwa na mvua kwake ni shida, kukiwa na jua nako ni shida.
Watu hawa huanza kuilaumu serikali kwa kila kitu, hata kama hicho kitu kipo ndani ya uwezo wake, watalaumu chama tawala hata kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wao, na hata usishangae akisikia mtu amebaka atasema inatakiwa katiba mpya!
Kwa kifupi mtu ambaye amekata tamaa na maisha hakuna jema analoona mbele yake, kwake yeye maisha hayana thamani tena, kwahiyo kila kitu au kila jambo ni baya, kwahiyo wakati mwingine tuwaelewe tu hawa watu.
Kinyume chake, watu ambao wana hisia nzuri wako positive, huiangalia dunia katika namna nzuri sana,pamoja na changamoto ambazo wanakutana nazo haziwafanyi kuona dunia ni sehemu mbaya ya kuishi,bali hukabiliana nazo na kusonga mbele.
Watu hawa hawailaumu serikali kwa kila kitu, ila wanajua wana wajibu wa kuwajibika ili maisha yapate kusonga mbele, badala ya kuilamu serikali kwa kila jambo, wao hutoa mawazo mbadala nini kifanyike ili wahusika wapete kuyafanyia kazi mawazo yao.
Kwa kuhitimisha ni kwa namna gani tutaiona hii dunia ni sehemu nzuri ya kuishi, itategemeana na hisia zetu tulizo nazo ima ni chanya au hasi, ambao wana hisia chanya wanaona kila kitu katika mtazamo mzuri sana na ambao wana hisia hasi kwao wao, kila kitu ni kibaya na hakina thamani
Ni hayo tu!